Mtatiro: Africa does not need strong people, it needs strong institutions! mlitubeza juu yakufukuza watumishi wa std 7

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
KUHUSU WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MSHAHARA KWA KUKOSA SIFA YA CHETI CHA KUFAULU MTIHANI WA ELIMU YA KIDATO CHA NNE;

"...Watumishi wote ambao na Ajira za Kudumu au Ajira za mikataba (Kwa Watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za muda (Employment on Temporary Terms) ambao walikuwa kazini kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ulipoanza kutumika Waraka wa utumishi( Establishment Circular) Na. 1 wa mwaka 2004, Warejeshwe kazini Mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria..."

"...Watumishi wa Umma Elfu Moja mia tatu sabini (1370) waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/P/13 ya tarehe 30 Juni, 2011, warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria..."

[HASHTAG]#KAULI[/HASHTAG] YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA BUNGENI LEO.

_________________________

#MY_TAKE;

Mwenye hasara hii kubwa ni mwananchi mlipa kodi. Mlipowafukuza kazi tuliwaambia kuwa ni UPUUZI, UHUNI, KINYUME NA SHERIA na KUKIUKA HAKI ZAO ZA MSINGI, lakini mkaziba masikio na kutetea uamuzi huo. Wapiga makofi wakawapigia makofi.

Leo mnawarudisha kazini (mnawapa haki yao) bila kuujibu umma wa watanzania kuwa hela ambazo watumishi hawa watalipwa huku hawakufanya kazi kwa mwaka mmoja hadi miwili zinatoka mfukoni kwa nani?

Je, zinakatwa kwenye mshahara wa aliyeamua wafukuzwe kazi bila kufuata utaratibu wala sheria? Au zinakatwa kwenye hazina ya taifa inayotokana na kodi za wananchi?

Kila siku tunawakumbusha kuwa AFRICA DOES NOT NEED STRONG PEOPLE, IT NEEDS STRONG INSTITUTIONS! Kama mambo yetu yangelikuwa yanaamuliwa na taasisi imara, serikali isingelifanya uamuzi ule wa hovyo kabisa wa kuwafukuza kazi watumishi waliodumu miongo kadhaa kazini, kwa sababu zisizo na mashiko na zisizozingatia hali halisi.

Baada ya uamuzi huu wa leo nilitegemea watu kadhaa wawajibike, lakini badala yake tunaendelea na sherehe.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
 
Hapo pekundu sijaelewa. Walifukuzwa kazi mwaka 2011 kabla ya mheshimiwa kuingia madarakani?
 
Back
Top Bottom