Mtathimini wa Mradi wa Bandari Bagamoyo mikononi mwa TAKUKURU


Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Messages
4,563
Likes
930
Points
280
Age
39
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2009
4,563 930 280
Aliyekuwa mtathimini wa mradi wa ujenzi Wa Bandari ya Bagamoyo ambaye pia hata rais aliyepita JK alimtaka waziri mkuu pinda kumuhamisha kazi Patrick Sese atiwa mbaroni na TAKUKURU kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Tanuru Blog zinasema kuwa Patrick alishiriki kuongeza orodha watu waliopaswa kulipwa fidia kupisha mradi wa bandari hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Sese alishirikiana na wenyeviti wa serekali za mtaa kufanikisha mipango hiyo kwa kuwaingiza watu hewa ili kujipatia mamilioni ya fedha kwanjia ya udanganyifu.

Sese alikamatwa wiki iliyopita na kushikiwa na kuhojiwa kwa siku kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana..taarifa zinasema kuwa mmoja wa mwenyekiti wa serekali za mtaa slishiriki katika skendo hiyo alikutwa amejinyonga wiki mbili zilizopita maaeneo ya Bagamoyo.

Taarifa zimasema kuwa mradi huo umetoa fidia kwa watu ambao si wakazi wa maeneo husika ambao leo ni matajiri wakubwa kwani wamelipwa mabilioni ya fedha.

Rais Dk. Jakaya Kikwete akifungua pazia
kwa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa
ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Jana
Rais Jakaya Kikwete amemwagiza Waziri
Mkuu Mizengo Pinda kumuondoa haraka
katika kituo cha kazi Mthamini wa Ardhi
wa Wilaya ya Bagamoyo, Patrick Cecy,
kutokana na kubainika kufanya ‘faulo’
katika ulipaji fidia wananchi waliotoa
ardhi yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa
mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Wananchi walioondolewa katika vijiji ili
kupisha mradi huo ni kutoka Pande,
Mlingotini, Zinga na Kilomo.
Rais Kikwete akiwa katika picha na
viongozi mbalimbali baada ya kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya
bagamoyo jana.
Alitoa agizo hilo jana wakati wa hafla ya
kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi
wa Bandari mpya ya Bagamoyo
inayojengwa wilayani Bagamoyo, mkoani
Pwani, mradi ambao utagharimu Dola za
Marekani bilioni 10 hadi utakapokamilika.
Alisema wakati harakati za ujenzi wa
mradi huo zikiendelea, zipo taarifa za
manung’uniko ya wananchi walioanza
kulipwa fidia kwamba kiasi walicholipwa
ni kidogo kutokana na ujanja uliofanywa
na mthamini wa ardhi.
‘Wanalalamika baadhi ya fomu
zimenyofolewa, mtu ameandika ana
hekta 20 lakini zinakatwa anaandikiwa
hekta nane, minazi inaandikiwa 100
analipwa 50,’ alisema Rais Kikwete huku
akishangiliwa na wananchi ambao
wamedhulumiwa.
Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo
waliohudhuria shughuli hiyo.
Rais Kikwete, alisema hapendi kuona
mradi mkubwa wa ujenzi wa bandari
unatekelezwa huku watu wakiwa
wananung’unika, kwani serikali wakati
wote haiwezi kuwaumiza watu maskini.
Nasikia mtathimini ndio mkorofi, Waziri
Mkuu mbadilisheni, wathamini wapo
wengi katika nchi hii, kwani nchi hii yupo
pekee yake, alihoji.
Alisema mtathimini huyo kuanzia leo
(jana), atafute pa kwenda na akabidhi
ofisi kwani mambo anayoyafanya
yanafitinisha wananchi na serikali na
kwamba angependa kuona bandari
inakamilika kukiwa hakuna manung’uniko
ya wananchi.
Rais Kikwete alisema wananchi
walihamishwa kupisha mradi huo kwa
kuwa kuna makaburi ya ndugu zao,
kama itawezekana wawe wanapewa
nafasi ya kwenda kuzulu makaburi hayo
au yahamishwe.
‘Huyu kijana kama haeleweki na
wenzake apelekwe sehemu nyingine
ambako ataeleweka lakini hapa
haeleweki,’ alisema.
Naye Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta,
alisema wananchi walioondolewa katika
vijiji hivyo mbali na kulipwa fidia pia
serikali itawajengea nyumba za kuishi
zitakazojengwa eneo la Kindagoni.
Kati ya wananchi 2041 wanaodai fidia
2011 wameshalipwa hadi sasa na
waliobaki serikali inaendelea kuwalipa.
Mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo
la hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa
bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili
ya ukanda wa viwanda.
Eneo hilo litaendelezwa chini ya
makubaliano ya Serikali ya Tanzania,
Kampuni ya China ya Merchants
Holdings International (CMHI) na Mfuko
wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini ya ushirikiano huo, serikali
inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya
Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo
Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje
(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na
China CMHI.
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,216
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,216 280
Acha dola ifanye kazi yake.
 

Forum statistics

Threads 1,275,076
Members 490,894
Posts 30,532,146