hustler Tz
Member
- Mar 16, 2018
- 8
- 21
Habari zenu wanajukwaa la Story of change.
Katika uzi huu nataka kuelezea ulazima wa kujifunza lugha ya kiingereza kwa mtanzania hata asie na elimu kubwa. Hili suala huwa haliongelewi kabisa na kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu lugha ya kiingereza.
JE, HUO UPOTOSHAJI UPOJE?
Hapa nchini Tanzania, hasa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu lugha ya kiingereza. Hasa viongozi wakubwa serikalini ndio wamekuwa wahusika wa hili. Watanzania wameaminishwa kuwa lugha ya kiingereza ni ukoloni na kujifunza lugha hiyo si uzalendo na hata kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa "hata mwanafunzi akimaliza form four na hajui kiingereza ni sawa kabisa kwani hatukwenda kumfundisha kiingereza bali tumeenda kumpa elimu" . Sasa swali ni kwamba, elimu gani hiyo aliopata wakati lugha ya kufundishia haijui??
Lugha ya kiinereza kwa sasa haihusiani tena na ukoloni bali ni njia kuu ya kuwaunganisha watu duniani kote. Lugha ya kiingereza inatumika katika biashara na kijamii pia. Mitandao karibia yote ya kijamii inatumia lugha ya kiingereza.
KWANINI KIINGEREZA SI UKOLONI KWASASA?
Kwa karne ya sasa ukisema kuwa kujifunza kiingereza ni ukoloni basi wewe utakuwa hujui hata dunia inaendaje kwasasa. Lugha ya kiingereza ndio Lugha kubwa na iliosambaa zaidi duniani.
Nchi kubwa na zenye ushawishi duniani kama Marekani, Uingereza, Canada, Australia na Afrika kusini zinatumia lugha ya kiingereza. Pia nchi nyingi za Afrika zinatumia lugha ya kiingereza.
Lugha ya kiingereza si ukoloni bali ni nafasi ya kuiunganisha dunia kwa lugha moja.
JE, TOFAUTI YA MTANZANIA ANAEJUA KIINGEREZA NA ASIEJUA KIINGEREZA NI IPI?
Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na upeo mkubwa wa kujua mambo mengi duniani ukilinganisha na yule asiejua. Hapa haijalishi elimu yao.
Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na akili iliyopevuka katika kuchambua mambo mengi zaidi. Mtu asiejua kiingereza hataweza kamwe kuendana na kasi ya dunia kwa sasa (Teknolojia).
USHAURI KWA SERIKALI
Serikali inatakiwa kuanzisha program mbalimbali za kuhamasisha watu kujifunza kiingereza ili kuwasaidia kuendana na kasi ya dunia ya kimaendeleo na teknolojia.
Kuna mambo mengi sana ya muhimu ya kujifunza kwenye mitandao lakini kwakua mengi yameandikwa kwa kiingereza na watu wengi hawajui kiingereza basi watu wengi huishia kufanya mambo yasiyo na manufaa yoyote.
Chaguo ni kujifunza kiingereza au kukubali kuishi katika zama za mawe ndani ya karne ya 21.
Nawasilisha.