Mtanzania yalalama na kauli za Chiligati, Nape dhidi ya JK....90DYS or else...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania yalalama na kauli za Chiligati, Nape dhidi ya JK....90DYS or else......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Apr 13, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mtanzania la leo linalomilikiwa na mmoja wa vinara wa ufisadi ndani ya CCM na anayeshukiwa kuwa yumo kwenye orodha ya kutimuliwa ndani ya chama hicho......................gazeti hilo limedai kauli za hotuba za Nape na Chiligati za kuisafisha CCM huku wakimlenga JK awajibike zinalenga kumkashifu Mwenyekiti na Raisi wa chama hicho.....................................
   
 2. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwani wamekosea nini? Si kuna thread hapa inayotaja majina ya watuhumiwa wa ufisadi kwani JK hayupo akipinga left wing? Nadhani pointi hapa sasa ni kuitanua list hiyo huku tukichambua pia katika CC nani ni nani na wamepataje nafasi hizo na kama ni wasafi ama wanaendeleza makundi yaokuelekea 2015.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Maono yangu ni kuwa JK na CCM katika mkakati wao wa kutununua kwa hoja nyepesi za kujivua gamba huku kichwa cha nyoka huyo kikiwa hakijavuliwa gamba kwa maana ya JK kuendelea madarakani na maswahiba wake akina Dr. Mwinyi, Ms Zakhia Hamdani Meghji, Abdallah Kigoda, Dr Maua Daftari N.K ni ushahidi tosheleza ya kuwa nyoka hata akijivua gamba bado ni nyoka usimsogelee kwani atakung'ata.........................................

  Baadhi ya mapungufu ambayo nimeyabaini katika zoezi feki linaloendelea la mageuzi ndani ya CCM ni kama ifuatavyo:-

  a) Kama ilivyokuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja, uongozi wa juu wa CCM bado unaendelea kuwadharau wanachama wake kwa kutowashirikisha katika kuona ni mageuzi ya namna gani wangelipenda kuona yanatokea ndani ya chama chao. Hivyo mageuzi haya ni ya kukidhi kiu ya madaraka ya viongozi na wala hayana uhusiano na kero za wanachama walalahoi ndani ya chama hicho......................................

  b) Usidanganyike na vyama vya upinzani kusifia au kukejeli mageuzi tajwa kwa sababu navyo siyo bunifu na ndiyo maana kimuundo wameiga mabaya yote yaliyomo ndani ya CCM. Hivyo, basi nyani hawezi kuona na kucheka au kusifia kundule...............................

  c) Jinsi ambavyo baadhi ya wajumbe wa CC walivyorudishwa kuendelea na nafasi zao na wale wapya walivyoingizwa ndani ya CC hakuna demokrasia pale na hivyo kuwafanya wale walioondolewa kuona kuwa wameonewa kutokana na kudhoofu kwa mahusiano yao binafsi na JK ambaye anaiendesha CCM kama shamba la bibi.................Kumbuka wakati wa Kampeni za 2010 alitoa ushuhuda wa ya kuwa URAISI ni suala la kifamilia hakuona kuwa ni dhamana kwa umma.......................kutoka na hisia hizo za kuonewa migawanyiko ndani ya CCM sasa imeongezeka badala ya kupungua kwa sababu vigezo vya kutimuana au kupeana ugali haviko wazi...............................na wala siyo shirikishi..................

  d) Kutokana na kampeni za Uraisi za 2015 wapo wengi ndani ya CCM wanaona JK anajenga mazingira ya kumrithisha amtakaye.......hivi yawezekanaje Meghji aonekane msafi huko ndiye aliyehusika katika kashfa ya EPA na majengo pacha? Hivi yawezekanaje Dr. Mwinyi AONEKANA NI SAFI HUKU USIMAMIZI WAKE WA WIZARA YA ULINZI NA JKT umezalisha maafa ya milipuko ya mabomu GONGO LA MBOTO na MBAGALA? Huku manunuzi ya helikopta na vifaa vingi vya jeshi kukuu yanatokea mikononi mwake na kusababisha maafa kwa raia wasio na hatia? Hivi inakuwaje Dr. Maua Daftari aendelee CC kuanzia wakati wa Mkapa na matatizo yatokee juu ya udhaifu wa CC kuisimamia serikali lakini yeye Dr. Daftari aonekane hana dosari? Vile vile Abdallah Kigoda amekaa kwenye nyadhifa za juu ndani ya CCM na hata kuna wakati alionekana anafaa kuwa Mweka Hazina lakini katika kujivua gamba aonekane ni gamba jipya? Wakati wa Dr. Kigoda kuwa Waziri wa Madini na huku akishikilia wadhifa wa Mweka hazina wa taifa wa CCM ndipo misamaha mingi mikubwa mikubwa ilitolewa kwa wawekezaji wa madini na fedha za misamaha hiyo ilielekezwa CCM isivyo halali na kinyume na sheria.................

  e) JK na urithi wa utawala wa kiimla..........proliferation of "DYNASTIES".............hivi CCM na hususani JK anapotaka kuwaweka vijana katika ngazi za juu ndani ya CCM ni lazima wawe watoto ambao baba zao walishawahi kuwa ndani ya CC kama Januari na Nape???????????????????????????????????????????????????????........................

  f) Muungano umekuwa unatumiwa kama kigezo ndani ya CCM kuwajaza waislamu katika CC bila ya kuzingatia idadi ya wanachama ndani ya CCM ambao wengi wao wako bara na ni wakristu. Kutokana na uwakilishi haramu asilimia hamsini hutoka Zanzibar na hivyo kufanya waislamu ni lazima wawe ni wengi ndani ya CC kwa sababu bara nako asilimia ishirini na tano au zaidi huwa ni waislamu na hivyo kufanya jumla ya waislamu ndani ya CC kutopungua asilimia 75 wakati waislamu ndani ya CCM ni asilimia 35 tu..........au chini ya hapo...................................Unapojivuna ya kuwa unajivua gamba ni lazima uondoe dhuluma hizi dhidi ya wakristu ndani ya CC kwa kufuta uwakilishi haramu wa waislamu ndani ya CC ambao hauzingatii idadi halisi ya wanachama waislamu wa CCM kutoka Zanzibar....................

  Kwa kifupi nyoka akijivua gamba bado ni nyoka na usimsogelee au kumgusa kwani aweza kukung'ata na kukusababishia upoteze uhai..............................my concerted advice to all TZ remains stay away from CCM circus.....................
   
 4. M

  Mbonafingi Senior Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  e) JK na urithi wa utawala wa kiimla.......................hivi CCM na hususani JK anapotaka kuwaweka vijana katika ngazi za juu ndani ya CCM ni lazima wawe watoto ambao baba zao walishawahi kuwa ndani ya CC kama Januari na Nape?????????????????????????????????????????????? ?????????........................

  Kwa kifupi nyoka akijivua gamba bado na nyoka na usimsogelee kwani aweza kukungata na kusababishia upoteze uhai..............................my concerted advice remains stay away from CCM circus.....................


  HILO NALO NENOOOOOOOO!!!!!!!
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Thumb up for CCM changes

  By DAILY NEWS Team, 12th April 2011 @ 20:00, Total Comments: 0, Hits: 174

  SOME Members of Parliament (MPs) and the general public on Tuesday hailed the leadership changes in the ranks of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), describing the move as brave and revolutionary.

  Kigoma North MP on Chadema ticket Kabwe Zitto said the elevation of the youths to the top leadership was testimony that the ruling party was for real changes.

  "I wish to extend my sincere congratulations to MPs Makamba and Nchemba for their elections to the party secretariat... we in Chadema started that move a long time ago and we are grateful that CCM has learnt a lesson," charged Mr Zitto, the deputy leader of opposition in parliament.

  January Makamba (Bumbuli --CCM), Mwigulu Nchemba (Iramba West -- CCM) and Nape Nnauye, the Masasi District Commissioner, were the three youthful politicians elected to the CCM secretariat on Monday.

  Debating the economic zones laws (miscellaneous amendments) Act of 2011, the legislator challenged the youths within the ruling party, as is the case with the opposition Chadema, to aim for even higher positions.

  Mr Titus Kamani (Busega -- CCM) said the party's leadership changes that saw almost all the popular personalities kicked out of the party secretariat and central committee signify the firm resolve to transform the party.

  Meanwhile, another view was expressed by Prof Palamagamba Kabudi of the University of Dar es Salaam who said the changes were a positive move. He added that there was still more to be done.

  "But we are in the right direction, it's a step forward," he said.

  He said that there is a Chinese saying that 1,000 mile walk starts with the first step. The preparations are good, the party has contributed a lot, not only in the country but also in other African countries.

  "You cannot mention South African independence without talking about TANU or CCM. Wilson Mukama is a perfect choice. I know him, he is an intelligent person and his background says it all," he said.

  Another reaction came from Mr Lucas Godwin, who is a student at the Dar es Salaam School of Journalism, said the changes could help revive hopes of the party members, adding that the reshuffle has revealed that there was a big problem within the party.

  In another development, Issa Yussuf in Zanzibar reports that Zanzibaris have thanked President Jakaya Kikwete for 'listening' to them.

  "We wanted these changes urgently," veteran politician Mr Hassan Nassor Moyo commented here yesterday on the New Central Committee and secretariat.

  "I know Mr Wilson Mukama, he is an intelligent CCM cadre. His deputies are also good and we hope for a stronger party that wins more trust from Tanzanians.

  CCM is still very strong and the party that can meet people's expectations. We need leaders with vision to work," said Mr Moyo, one of the founders of CCM. Mr Mansour Yussuf Himid said , "I am happy with the changes. I hope the changes will reinforce unity in the party. We need to show support for the reforms."

  Ms Khadija Omar, a CCM supporter, said although Mr Mukama "is said to be intelligent, I wish his position would have been taken over by January Makamba or Nape Nnauye because they are young and active."

  Mr Sultan Mugheiry, former Zanzibar minister for health, said: "I welcome the changes that will definitely revive the party so that more people can join." A Civic United Front (CUF)'s fan, Mr Hassan Mussa, commented, "What I need is peace and stability to prevail."

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) National Executive Council (NEC) which met in Dodoma under the chairmanship of President Jakaya Kikwete, last Monday, picked a new Central Committee and secretariat following the resignation of the former party leadership.

  The new Secretariat is headed by Mr Wilson Mukama as Secretary General and assisted by Captain John Chiligati (rtd) and Mr Vuai Ali Vuai as Deputy SG for Tanzania Mainland and Zanzibar respectively.

  The secretariat also comprises Mr January Makamba as the new Secretary for Political Affairs and International Relationship while Mwigulu Mchemba took over as Secretary for Finance and Economic Affairs.

  Ms Asha Juma Abdallah is the secretary for organization while Nape Nnauye takes over as Secretary for Ideology and Publicity.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  PHP:
  January Makamba (Bumbuli --CCM), Mwigulu Nchemba (Iramba West --  CCM) and Nape Nnauyethe Masasi District Commissionerwere the three  youthful politicians elected to the CCM secretariat on Monday
  CCM inakemea viongozi kujirundikia madaraka na hawa wabunge wawili Januari na Mwigulu wanaongezewa ugali....................doublespeak is the hallmark of CCM...........Nape watasema aatacha ukuu wa WILAYA....................
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Nnauye:Mafisadi wasahau kusimamisha maumuzi Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 20:53

  Midraji Ibrahim na Joyce Mmasi, Dodoma
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho, wanapaswa kusahau uwezekano wa wao kujipanga na kusimamisha hatua zilizoanza kuchukuliwa.Nnauye alisema chama kitashinda vita ya ufisadi na kwamba, kama kuna watu wanajifanganya kuwa wanaweza kufifisha moto uliowashwa, wajaribu.

  Akizungumza mjini Dodoma jana, Nnauye alisema kilichofanywa na Halmashauri Kuu ya CCM, ni mwanzo wa mapambano ya kufagia mafisadi ndani ya chama hicho kinachotawala."Chama kitashinda vita hivyo, kama kuna watu wanafikiri wanaweza kujaribu, Tumeanza tutamaliza,"alisema.

  Kuhusu madai kwamba tamko kuhusu watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi kupewa siku 90 kujiuzulu Nec alilotoa na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, John Chiligati, lilikuwa lao na kwamba si la Nec, alisema maamuzi yote ya kikao yapo kwenye maandishi."Maamuzi yako kimaandishi si yangu, yanasema wajiuzulu wenyewe wasipofanya hivyo chama kitawawajibisha chenyewe," alisisitiza Nnauye.

  Akitoa tamko hilo juzi usiku baada ya kumalizika kwa kikao cha Nec, Chiligati alisema "wenyewe wapime na kuchukua hatua za kuwajibika ndani ya chama kama tulivyokubalina hapa ndani, wasipofanya hivyo katika kipindi cha miezi mitatu, chama hakitasita kufanya hivyo kwa niaba yao."

  "Hata kama hatuna ushahidi, hisia tu kutoka kwa wananchi zitoshe kuwafanya wajipime wao wenyewe, na kama kuna hoja ya kuonewa kwa nini usemwe wewe tu." alisema.

  Nnauye aliwataka wanachama waliokimbia kwa hasira, kurejea CCM kwa sababu walichotaka kimefanyika na kwamba, tayari ana maombi mengi ya wanafunzi na wanachama kutaka kurejea.Kuhusu muda wa kufanya marekebisho kwenye chama ngazi zote, Nnauye alisema mpango wa kazi upo na utatekelezwa kwa hatua."Hata unapoanza kuoga huanzi mwili mzima, unakwenda hatua kwa hatua. Mpango kazi upo utatekelezwa," alisema.

  Alisema kufuatia uamuzi wa Nec, baadhi ya wanachama wameomba kukutana na sekretarieti na kwamba, itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara, Pius Msekwa.Nnauye alisema ziara ya kukutana na wanachama hao ilianza jana mjini Dodoma na leo, itaendelea mkaoni Morogoro.

  Kwa mujibu wa Katibu huyo, Aprili 16, mwaka huu, sekretarieti itakutana na wanachama wa Chalinze, Kibaha na Dar es Salaam na kabla ya kwenda Zanzibar, Aprili 17 mwaka huu.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Comments
  0 #4 MKWELI 2011-04-14 08:45 Hi Nape! Angalia usije ukaondoka na mtumbi wa vibwengo.Tuna imani nawe.Tuna ngoja utekelezaji na usipofanyika CCM itakuwa imejifia kwao
  Quote

  +1 #3 mkilima 2011-04-14 07:58 Hilo haliwezekani, watangaze kujiondoa kwenye nyazifa wakati mmewaondoa nawengine tayari wamechaguliwa,s asa kama mnasubili wajiondoe na hilo linalodaiwa kuwa mmelivua gamba gamba hilo ni akina nani? Nape uatumainiwa lakini nawe unakwenda pabaya
  Quote

  +1 #2 kushake 2011-04-14 04:25 Hata mafisadi walipokwapua BOT JK aliwapa siku 90 mbona hamna kitu? iko wapi Kagoda? chenga ya macho tu nyiye. Tz tunachotaka sasa ni kujiamulia mambo yetu upya bila mtu yeyote kutuingilia
  Quote

  +1 #1 vuvulzela 2011-04-14 03:41 ."Maamuzi yako kimaandishi si yangu, yanasema wajiuzulu wenyewe wasipofanya hivyo chama kitawawajibisha chenyewe," alisisitiza Nnauye". wajiuzulu uanachama wa CCM na Ubunge? au uongozi ndani ya CCM? hapa bado kuna utata tena ni usanii mkubwa
  Nape Mnauye vipi na wapambe wa mafisadi kama UVCCM na Sofia Simba na wengine you name? naona CCM imewapa muda mafisadi kukimbia nchi kutimiza ubashiri wa mtabiri wa CCM Yahya Husein
  Quote
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Tatizo CCM si sura wasema wapinzani Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 20:51

  Fidelis Butahe
  BAADHI ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini, wameponda mabadiliko ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa madai kuwa tatizo la chama hicho ni mfumo na si sura za watu.

  Kauli hiyo inafuatia hatua ya Halmashauri Kuu ya CCM,kuthibitisha safu mpya ya uongozi wa Kamati kuu na sekretarieti ya chama hicho. Hata hivyo safu hiyo haikujumuisha baadhi ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ambao wamepewa siku 90, wawe wamewaachie nafasi zao vinginevyo watawajibishwa.

  Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, viongozi hao wa vyama vya TLP, UPDP, NCCR-Mageuzi na DP, walisema CCM bado ina kazi mzito.Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila, alidai kuwa tatizo la CCM ni Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

  Mtikila ambaye alizuia kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kutokana na kutotimiza masharti ya wadhamini katika mikoa 10, alisema mabadiliko ya CCM si lolote kwa kuwa yamelenga kubadili sura tu wakati mfumo ni ule ule."CCM si chama cha wanachama, hakuna demokrasia pale. Katibu Mkuu wa sasa wa chama hiki amechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM, hata hiyo kamati kuu nayo imechaguliwa na mtu mmoja tu," alisema Mtikila.

  Mtikila alidai kuwa uozo ndani ya CCM unasababishwa na mtu mmoja na kusisitiza kuwa hata hao waliochaguliwa, hawataweza kubadilisha kitu kwa kuwa watafuata maelekezo ya mtu huyo."Sasa kama mtu kakuchagua unafikiri utashindwa kumfuata vile anavyotaka, akikanyaga mguu wa kulia na wewe utakanyaga hapo hapo," alisema Mtikila.

  Alidai kuwa mabadiliko ndani ya CCM, yanapaswa kufanywa katika maeneo nyeti zaidi ambayo hata huvyo hakutaka kuyataja.Katibu Mkuu wa NCCR, Samwel Ruhuza akitumia msemo 'imejivua gamba' unaomaanisha kuwa CCM imeanza ukurasa mpya na viongozi wapya alisema, "Nyoka akijivua gamba si anabaki nyoka, tatizo la CCM ni mfumo si sura za viongozi wa sasa na wa zamani."

  Alisema kuondoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba na nafasi yake kuchukuliwa na Wilson Mkama hakuwezi kukinufaisha chama hicho kama kikiendelea kutumia mfumo ule ule."Siwaombei mabaya kwa kuwa wakivurunda nchi nayo itayumba, sisi wote ni Watanzania, tatizo la CCM hawafuati miiko ya uongozi, Mkama anaweza kuwa kiongozi mzuri ila anaweza kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya mfumo wa uongozi ulivyo," alisema Ruhuza.

  Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, aliipongeza CCM kwa hatua hiyo lakini alionya kuwa isijaribu kuua upinzani kwamba vinginevyo, haitafika mbali.

  "Sawa wamefanya uchaguzi, nawapongeza lakini kamwe wasijaribu kuua upinzani wataishia pabaya sana, watizame maslahi ya taifa na kuacha ubinafsi," alisema kada huyo wa zamani wa CCM kabla ya kuhamia NCCR Mageuzi na baadaye TLP.

  Alisema hata hivyo mabadiliko hayo hayawezi kumfanya yeye arudi CCM.Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, alisema mabadiliko ndani ya CCM huenda yakawafanya wapinzani kuanza upya harakati za kuking'oa chama hicho madarakani.

  "Unajua uongozi wa CCM uliopita chini ya Makamba ulikuwa ahueni kwa wapinzani, ila tutatizama wa hao wanaokuja, Makamba ilikuwa rahisi sana kupambana naye, uongozi wa sasa ukifanya vizuri hali ya upinzani inaweza kuwa ngumu," alisema Dovutwa.
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  CCM: Graft war will be won

  From MASATO MASATO in Dodoma,
  13th April 2011

  THE ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), on Wednesday reiterated its firm resolve to fight corruption and all corrupt elements within its ranks, saying the war it has started will definitely be won.

  "The party will ultimately win this war (against corruption)... we are determined to win, we have started and we will sustain it to the end," said Mr Nape Nnauye, the newly elected publicity secretary.


  Addressing a news conference, Mr Nnauye welcomed CCM members who had defected to opposition parties in protest against the ruling party's alleged links with corrupt people.


  "The party has taken bold steps to cleanse itself. May I seize this opportunity to welcome back our members who were angry and resolved to protest misdeeds within our party."


  Mr Nnauye said the party's dismal performance in last October's general elections stemmed from dissatisfaction among party members.


  "It is obvious the party lost many constituencies whose majority voters were CCM members... they voted against the party to express their dissatisfaction of the way the corrupt people were worshipped."


  Asked to comment on a story published by a local paper that implicated President Jakaya Kikwete to corruption allegations, Mr Nnauye shrugged off the paper's content saying :

  "You all know the owner of the tabloid and the reason behind that story."

  He said the main suspects of corruption will attempt to clear their names but warned:


  "Let all corrupt elements be informed that this time we are serious... all escape routes are closed."


  Mr Nnauye urged Tanzanians to shun media opposed to the crusade against corruption in the country, adding:

  "Corruption knows no ideology... we are all affected in one way or the other."

  Meanwhile, the new CCM secretariat will, under its Vice-Chairman, mainland, Pius Msekwa, start a four-day tour to the central and eastern zones to introduce itself to party members and supporters.


  "We have received many requests from party members and supporters who would like to meet with us," said the party spokesperson, adding that the secretariat will this afternoon be at Nyerere Square in Dodoma.


  The secretariat will tomorrow receive congratulatory demonstrations in Morogoro before moving to Chalinze and Dar es Salaam on Saturday.


  It will end the first phase tour of the country on Sunday by holding a public rally in Zanzibar. "We will then retreat for plans for the next round of the tour... the intention is to go countrywide," he said.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  CCM waenda mikoani kuukana ufisadi


  *Wapeleka ujumbe wa NEC mkoa kwa mkoa
  *Nape asema watapambana hadi washinde


  Na Edmund Mihale, Dodoma

  CHAMA Cha Mpinduzi (CCM) kimeanza ziara mikoani kupeleka ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa wanachama kuwa kimedhamiria kupambana na ufisadi ndani na nje ya chama hadi kishinde.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye aliyasema hayo Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma jana, wakati akitangaza ratiba ya mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama na Sekretarieti ya chama hicho mkoani hapa.


  Alisema chama hicho kimeandaa ziara kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Halmashauri Kuu kwa wanachama wake kuanzia leo ambapo watafanya makutano katika Uwanja wa Nyerere Square na kesho Mkoani Morogoro.


  Alisema kuwa mapokezi hayo yataendelea katika Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibaha ambapo yatapokelewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Alisema kuwa siku hiyo hiyo yataendelea katika Mkoa Dar es Salaam na Aprili 17 mwaka huu yatakuwa Zanzibar.


  "Tutapambana na ufisadi hadi tushinde," alisema Bw. Nnauye.


  Alisema kuwa CCM haitavumilia kuona inachafuliwa na watu wachache na kuwataka wanachama waliohama kwa hasira kutokana na kashfa ya ufisadi kurudi kundini.


  Alisema uamuzi uliofikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa utafanyiwa kazi.Alisema uamuzi wa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ufisadi uko pale pale, hivyo wasidhani kuwa chama kimeishia hapo.


  "Ndugu zangu Halmashauri Kuu iliamua kuwa tutapambana na ufisadi hadi tushinde, hivyo kama alivyozungumza mwenyekiti, wanaotuhumiwa wajiandae, tumefunga milango na madirisha yote, ili kuhakikisha tunashinda," alisema Bw. Nnauye.
   
 12. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona unachangia wewe tu hii thread ama ndilo gamba lako ulilovaa? Kuna umuhimu nikuvue gamba kwani sasa unadata.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  'CCM bado imevaa mfumo wa ufisadi'

  *Kiongozi UVCCM adai utawasaidia waliotemwa kuibuka
  *Msekwa asema kinachowaumiza ni mbio za urais 2015


  SIKU chache baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya kile kinachoitwa ni kujivua gamba, imeelezwa kuwa hatua hiyo haitasaidia, kwani 'imeondoa watu badala ya mfumo dhaifu' ambao ndiyo jamvi la mafisadi ndani ya chama na serikali yake.

  Imeelezwa kuwa pamoja na CCM kutaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika kashfa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiitikisa nchi kwa muda mrefu sasa, wajirekebishe au kukaa kando, bado wanaweza kutumia mfumo dhaifu uliolea ufisadi kwa muda mrefu, hata kama wako nje, kwani 'watu hao wana vibaraka na mawakala wao katika maeneo mengi nchini'.


  Hayo yalisemwa jana na Mjumbe wa Mkutano wa Wilaya Umoja wa Vijana wa CCM, Moshi Vijijini, Bw. Paul Makonda alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua hiyo ya CCM, ya kuteua wajumbe wapya wa Kamati Kuu (CC) na sekretarieti, baada ya wale wa awali kujiuzulu.


  Alipobanwa na waandishi wa habari, wakitaka kujua kundi lipi analitumikia kati ya yaliyopo ndani ya CCM, alisema kuwa anatumwa na wananchi wasiokuwa na sauti, wanyonge, wasiosikika, walioko vijijini, baadhi yao wakiwa ni wana-CCM, ambao wakati mwingine si rahisi kuvifikia vyombo vya habari na kupaza madai yao dhidi ya matatizo yanayoikabili nchi na chama chao.


  Huku akitaja majina ya baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, Bw. Makonda alisema kuwa wametumia mwanya wa mfumo huo wa ufisadi kushawishi uteuzi wa mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na nafasi nyingine mpaka ngazi za chini ambao ni watiifu kwao, hivyo wanaweza kuwatumia kadri wanavyotaka, kwani 'ni mawakala na vibaraka wao'.


  Akizungumza kwa ujasiri, Bw. Mkonda alisema kuwa anatumia nafasi yake hiyo pamoja na ile ya Mjumbe wa Mkutano wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro kutoa maoni yake, ambapo alisema kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anastahili pongezi kwa uamuzi huo mgumu wa Dodoma.


  "Tumpongeze Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi mgumu, ambao kabla haukutarajiwa na yeyote awe mwanachama au si mwanachama. Uamuzi wa kuvunja sekretarieti ya chama siyo tu ulikuwa mgumu, bali athari zake hata sasa itakuwa ngumu kuchukuliwa na wahusika na washirika wao. Haya ndiyo maamuzi ambayo wanachama wanaweza kuandamana kuyaunga mkono.


  "Hata hivyo kilichofanyika ni mkakati wa kujinusuru, ambapo sasa Sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu Bw. Wilson Mukama inalo jukumu la kuhaulisha haiba ya chama iliyopauka machoni pa Watanzania na miongoni mwa wanachama na kuelekeza katika mkakati wa ushindi endelevu, kwa kukibadilisha chama kutoka utendaji kwa uzoefu, kwenda utendaji wa kitaalamu unaozingatia nyakati tulizonazo.


  "Yaliyotokea Dodoma ni katika juhudi za chama kujinasua na mtego wa kuporomoka kwenye siasa za Tanzania na kimataifa...sasa ni wakati wa kuondokana na utendaji mazoea na kwenda kisayansi...kilichotokea ni kuondoa watu dhaifu na si kuondoa mfumo dhaifu, uliojengeka kwa kipindi kirefu ambao ulisababisha watu wenye uroho. Walioamua kuweka mustakabali wa taifa rehani kwa maslahi yao binafsi kuigeuza nchi kuwa jamvi la mafisadi.


  "Ni mfumo huu dhaifu uliopelekea uimarishaji wa watu badala ya kuimarisha mifumo ya utawala, siasa, demokrasia na haki za binadamu, utawala wa sheria na ushiriki wa wananchi katika kujiletea maendeleo," alisema Bw. Makonda kwa kirefu, akiongeza kuwa haitoshi kuwaondoa akina Andrew Chenge, Edward Lowassa na Rostam Aziz.


  Alisema kuwa kwa muda mrefu chama hicho kimejikita katika kuangalia matokeo kama njia ya kujihalalisha machoni pa watu na kuwatambia wapinzani, badala ya kuangalia mfumo unaokiwezesha kupata matokeo, hivyo kimeshtuka baada ya 'kuvuliwa nguo sehemu nyeti na wapinzani', kwa kushindwa katika maeneo aliyodai yalikuwa muhimu na ngome ya CCM, kwenye uchaguzi uliopita.


  Kijana huyo ambaye alionekana kutoa maelekezo kwa sekretarieti mpya ya CCM, alisema kuwa kinatakiwa kujifanyia marekebisho ya kimfumo ndani ya chama, kuufanya utafiti wa mwelekeo wa kisiasa kuwa ndiyo kipaumbele cha ofisi ya katibu wa uenezi na itikadi, kutumia mifumo ya kisasa ya mawasiliano kutoa taarifa kwa haraka, bila kuwa na milolongo ya kusubiri vikao halali.


  Akiwageukia wenzake wa UVCCM, ambao katika mkutano wa kwanza aliwapatia siku saba wajiuzulu akiwatuhumu kwenda kinyume na katiba na kanuni za CCM, alisema sasa yuko katika mchakato wa kuandaa UVCCM nyingine, ambayo amesema itaitwa UVCCM-Maadili, ambao uko mbioni kumalizika na kuwasilishwa mezani kwa katibu mkuu mpya.


  Alisema kuwa anatumia haki ya ibara ya 15 katika katiba ya CCM kuunda UVCCM-Maadili, akiwataka vijana wengine wanachama wa CCM, wanaotaka kuitumikia nchi kwa uadilifu, kujitokeza na kumuunga mkono katika mchakato huo, akisema UVCCM iliyopo imeshindwa majukumu, badala yake viongozi wake wamekuwa vibaraka na mawakala wa mafisadi.


  Pia alitoa madai mazito kwa mmoja wa makada wa chama hicho, wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Bw. Rostam Aziz, akitaka aondolewe katika chama, pamoja na viongozi wa UVCCM, Mwenyekiti Beno Malisa, James Millya, Hussen Bashe na Martine Shighela, ambao alidai ni vibaraka wake, akisema mwenendo wao umeharibu chama na ustawi wa taifa kwa ujumla.


  "CCM imetoa siku tisini kwa wale wenye tuhuma za ufisadi, walojihusisha na DOWANS, KAGODA, na mambo mengine yaliyoaibisha nchi na kushusha haiba ya chama mbele ya wapiga kura. Huu ni muda mrefu mno kwa watu kama hawa. Wanaweza kutumia muda huo kufanya mambo ya ajabu kabisa. Hivyo wao wenyewe wachukue hatua hizo mapema."


  Bw. Makonda aliongeza kuwa iwapo Bw. Lowassa aliwahi kujiuzulu katika kashfa ya Richmond, mapema wakati bunge likiendelea na mjadala, basi anatakiwa kufanya vivyo hivyo katika hatua hii, pamoja na watuhumiwa wengine wote.


  Msekwa ataja kinachotuumiza


  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tazania Bara, Bw. Pius Msekwa amsema kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanakiumiza chama hicho ndani kwa ndani ni mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.


  Msekwa aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kutambulisha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa iliyochaguliwa hivi karibuni mjini Dodoma baada ya chama hicho ujivua gamba' na kujiuzuku kwa ile ya awali.


  Msekwa alisema kuwa hivi sasa ndani ya chama hicho yapo makundi ya vinara wanaowania urais ambayo yamewagawa wanachama wa chama hicho na hali hiyo imekuwa ikiathiri umoja na mshikamano ndani ya chama kwa kiwango kikubwa.


  Alisema kuwa umoja na mshikamano ndani ya chama ni nguvu kubwa inayowahakikishia ushindi katika mashindano na vyama vingine, hivyo tatizo hilo la vinara kuwagawa wanachama ni kubwa na linaathiri chama kwa kiwango kikubwa, hivyo chama hakina budi kulitafutia ufumbuzi wa haraka.


  Akifafanua zaidi, alisema kuwa kiini kikubwa cha tatizo hilo ni utaratibu wa kupata wagombea wa CCM ambao unatumika hivi sasa kulingana na kanuni za uchaguzi wa kuingia katika vyombo vya dola zilizopo.


  Kufuatia hali hiyo, Bw. Msekwa alisema kuwa NEC imefanya mageuzi kwa kuelekeza utafutwe utaratibu bora zaidi wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambao utalenga kuzuia matumizi makubwa ya fedha kwa nia ya kununua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na vya uteuzi wa mwisho katika mchakato huo.


  Naye Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw, Wilson Mukama alisema kuwa yaliyofanywa na chama hicho ni maamuzi ya kimapinduzi na wala hayapunguzi heshima ya chama hicho, hivyo wana-CCM hawapaswi
  kukaa kama kuku katika tenga, watembee kifua mbele kwani chama chao kimeimarishwa.

  Mukama alisema kuwa mageuzi yaliyofanyika ndani ya chama si ya kujipodoa bali ya kukijenga upya ili kiweze kuleta ari mpya kwa wanachama wake na kuahidi kuwa kazi ya sekretarieti hiyo mpya wajiandae kuona matokeo mazuri.


  Imeandaliwa na Tumaini Makene, Dar; na Pendo Mtibuche, Dodoma
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Mukama: CCM haijipodoi

  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma;
  Tarehe: 15th April 2011


  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema chama hicho si jiwe, ni chama makini, na mageuzi ilichofanya si ya kujipodoa.

  Ametamba kuwa, CCM ni chama imara ndiyo maana kimeweza kufanya mabadiliko ya uongozi bila nchi kutikisika.


  Mukama amesema, CCM ni chama kinachokua kifikra, kimuundo, na kimazingira, na kwamba mabadiliko yaliyofanywa ndani ya chama hicho si nguvu ya soda.


  "Hii sio nguvu ya soda, katu, katu, katu" na akasema hata vyama vya upinzani vinajua CCM ni namba moja.


  Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuitambulisha sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyothibitishwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.


  "CCM sio jiwe, CCM ni chama kinachokua… nani kama CCM, na mnakaa chini kama mpo kwenye tenga, tembeeni kifua mbele, tumeshinda" amesema Mukama katika viwanja vya Nyerere Square.


  Amewaeleza wananchi wengi wao wakiwa viongozi, wapenzi na wafuasi wa CCM kwamba, maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM ilikuwa ni kutekeleza azma ya kujivua gamba.


  "Mageuzi haya yatafika mbali, na mtaona matokeo yake" amesema Mukama na kutamba kuwa yeye na sekretarieti ya chama hicho ni askari wa miamvuli, na anajivunia kuwa na damu changa katika sekretarieti ya CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na Katibu wa NEC wa siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Januari Makamba.


  "Sisi ni askari wa mwamvuli na tupo tayari kulibeba jukumu tulilokabidhiwa" amesema Mukama na kusisitiza kwamba, viongozi vijana CCM ni askari wa mwamvuli na wana dhamira ya kweli.


  "Mvuto mpya, watu wanaotaka kwenda na fasheni hawawezi kuwa wazee kama sisi, ni vijana, ni akina mama" amesema.


  Amesema, hoja zilizojadiliwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, zimezaa matunda stahiki.


  "Thamani ya fedha iliyotumika pale ilizaa gawio, ulikuwa na tija" amesema Mukama na kubainisha kwamba, maamuzi ya NEC CCM yalikuwa mazito, muhimu na hayajawahi kufanyika.


  Ametoa mfano wa uamuzi wa kuwapata wajumbe wa NEC kutoka wilayani badala ya mkoani kuwa ni wa kihistoria na wa kimapinduzi na si kweli kwamba thamani ya chombo hicho cha uongozi itapungua.


  "Sasa wajumbe wa NEC itabidi watazame chini…uongozi wa chama chetu umeunganisha wilaya na taifa" amesema katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa CCM mkoani Dodoma na makada wa chama hicho akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, George Mkuchika, na Waziri wa Maji, Mark Mwandosya
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Vigogo wanaoichafua CCM kulimwa barua

  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma;
  Tarehe: 15th April 2011

  HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kuwaandikia barua viongozi wanaotakiwa kujiuzulu kuwafahamisha kwamba, kama hawatafanya hivyo kikao kijacho cha NEC kitawafuta uongozi.

  Watuhumiwa hao wa rushwa na ufisadi wakiwemo wajumbe wa NEC taifa, wamepewa muda wapime uzito wa tuhuma zinazowakabili, wajiuzulu.


  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, amesema NEC imeamua kubadili muonekano wa viongozi wake hivyo watuhumiwa wa rushwa, wabinafsi, waliojilimbikizia mali, na wanaojitafutia umaarufu watawajibishwa ipasavyo.


  "Tulisema tuwape muda, wao wenyewe, watafakari, wajipime, wajiuzulu… lakini wasipofanya hivyo, chama kitatoa maamuzi ya kuwawajibisha chenyewe" amesema Msekwa mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa sekretarieti akiwemo Katibu Mkuu, Wilson Mukama.


  Kwa mujibu wa Msekwa, ufisadi umeathiri taswira ya CCM, na kwamba chama hicho kilifanya kosa la kuwakubali wafanyabiashara wasio waaminifu katika vikao vya CCM.


  "Bado wananchi wengi wanaionyooshea kidole CCM kuwa inakumbatia wala rushwa" amesema Msekwa na kubainisha kwamba rushwa imekuwa ni mzigo mkubwa sana katika chama hicho.


  "CCM imepoteza sifa yake ya awali ya kuwa ni chama kinachojali maslahi ya wanyonge na sasa inabebeshwa mzigo wa kuwa ni chama cha matajiri"amesema Msekwa.


  Amesema, CCM imejivua gamba, kimekuwa chama kipya, na kwamba jogoo amewika hivyo waamke. Msekwa amesema, maamuzi ya NEC CCM ilikuwa ni utekelezaji wa kufanya mageuzi ndani ya chama hicho kwa kujivua gamba mithili ya nyoka.


  Kwa mujibu wa Msekwa, NEC ilifanya maamuzi katika maeneo manne ikiwa ni pamoja kna kufanya mageuzi ya kuiwezesha CCM kupambana na ukoloni mamboleo unaoathiri siasa za nchi yetu.


  Amesema, CCM imefana mageuzi ya kubadilisha muonekano hasi wa chama hicho kwa wananchi, kujipanga upya ili kujiimarisha kishinde uchaguzi, na mageuzi ya kukiwezesha kupambana na maovu ukiwemo ufisadi na rushwa.


  Kwa mujibu wa Msekwa, CCM imeamua kusahihisha makosa ya nyuma kwa kubadili masuala mengi ikiwa ni pamoja na kutoteua wagombea wasiokubalika, na pia kitafanya mageuzi ili kuongeza wigo wa kuwa karibu na makundi ya watu.


  CCM pia imeamua kubadili utaratibu wa kumpata mgombea wake wa urais ili kuzuia matumizi makubwa ya fedha zinazonunua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na vya uteuzi wa mwisho katika mchakato huo.


  "Makundi ya vinara wanaowania urais yamewagawa wanachama wetu na kuathiri umoja na mshikamano ndani ya chama kwa kiwango kikubwa sana" amesema Msekwa.


  "Tatizo hili ni kubwa na lina athari kubwa kwa chama chetu" amesema Msekwa na kubainisha kwamba, CCM pia imesitisha utaratibu wa kutoa kadi za uanachama za papo hapo.


  "Tumefanya mageuzi ya kubadilisha utaratibu wa kuingiza wanachama wapya kwa kufanya uamuzi kwamba, chama katika ngazi ya matawi kitenge siku moja maalumu katika mwezi ambapo wanachama wapya watapokea kadi zao kwa sherehe rasmi" amesema.


  Kwa mujibu wa Msekwa, CCM pia imebadili salamu yake, mtu akisema ' Kidumu Chama Cha Mapinduzi' unaitikia ' Idumu CCM mpya'. CCM pia imebadili utaratibu wa utoaji kadi za uanachama wakati wa kura za maoni.


  "Tumefanya mageuzi ya kuweka muda wa mwisho wa utoaji wa kadi za wanachama kwa ajili ya upigaji kura za maoni uwe tarehe 31 Desemba ya mwaka unaotangulia mwaka wa uchaguzi mkuu husika" amesema Msekwa na kuongeza kuwa, CCM pia imebadili utaratibu wa uchaguzi wa chama na jumuiya zake


  "Kuanzia sasa tutakuwa tunafanya uchaguzi wa chama na jumuiya zake katika mwaka mmoja" amesema na kubainisha kwamba, uamuzi huo utaiwezesha CCM kupata muda wa kutosha wa kufanya kazi za chama ndani ya chama na kwa umma.


  Amesema, CCM pia imebadili utaratibu wa uteuzi wa wagombea wa CCM wa ubunge na udiwani, na kuanzia sasa watachujwa ili kupata wagombea wasiozidi watatu ambao watapigiwa kura za maoni.


  Msekwa amesema, CCM pia itaangalia uwezekano wa kuanzisha viwango vya ada vinavyotofautiana kulingana na kipato cha wanachama, kampuni za chama hicho ambazo hazifanyi kazi vizuri zitafutwa, na pia chama kitaangalia uwezekano wa kuuza baadhi ya mali zake ili kiwekeze kwenye miradi yenye tija.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Makonda sasa ataka UVCCM ivunjweThursday, 14 April 2011
  Geofrey Nyangóro


  MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kupitia Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Makonda, ameelezea azma yake ya kupendekeza kwa chama hicho, wazo la kutaka kuvunjwa kwa jumuiya hiyo na kuundwa upya.

  Makonda ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema azma hiyo inatokana na kitendo cha mafisadi kujiingiza katika jumuiya hiyo na kutumia vibaraka wao kutekeleza malengo yao ya kukihujumu chama.


  Machi 28 mwaka huu, Makonda alishauri mabaraza ya jumuiya hiyo katika ngazi ya taifa na mikoa na sekretarieti zake, yajiuzulu ndani ya kipindi cha siku saba.

  Hata hivyo ushauri huo ulipuuzwa.Katika mazungumzo yake ya jana, Makonda alisema baada ya kuona ushauri huo umepuuzwa, sasa anaandaa pendekezo la kutaka jumuiya hiyo, ivunjwe na kuundwa mpya.


  Kwa mujibu wa kada huyo wa CCM, pendekezo hilo ataliwakilisha kwa sekretarieti mpya ya CCM.Alisema pamoja na mambo mengine, atapendekeza jumuiya hiyo mpya iitwe UV-CCM Maadili, kulingana na malengo na matakwa yake kwa vijana na chama.


  "Kwenye katiba yetu ya chama, ibara ya 15 inatoa mamlaka kwa chama kuondoa, kupunguza jumuiya zake au kuongeza. Mimi nimeweka nia na nataka vijana wa CCM kote nchini kuunga mkono mchakato huu. Nitawasilisha mapendekezo ya kuanzishwa kwa jumuiya mpya ya vijana, ambayo itatimiza majukumu yote yaliyosababisha kuanzishwa kwa umoja huo,"alisema Makonda.


  Alisema jambo lingine linalomsukuma kufikia uamuzi huo ni uongozi uliopo kwenye jumuiya hiyo, kushindwa kuwajibika."Baadhi ya viongozi wanadiriki kujipambanua kuwa marafiki wa mafisadi walioligharimu taifa na kusababisha athari zitakazodumu kwa miaka mingi," alisema.


  "Namna pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuanzisha jumuiya hiyo mpya itakayojishughulisha na masuala ya vijana ili waweze kujiona kuwa sehemu ya CCM na wenye jukumu la kukijenga chama na kulitumikia taifa kwa uadilifu," alisisitiza.


  Katika hatua nyingine, mwanachama huyo wa CCM alimpongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuridhia mabadiliko ya sekratarieti kuu ya chama.Alisema tukio kama hilo halijawahi kutokea tangu enzi za Tanu na CCM.


  Alisema hata hivyo kilichofanyika ni kuwaondoa watu dhaifu.Alisema kinachotakiwa kufanyika hivi sasa ni mabadiliko ya mfumo utakaozingatia utendaji wa kazi wa kitaalamu na kutaka chama hicho kuachana na mfumo wa kizamani wa kufanya kazi kwa mazoea.


  "Sekratarieti iliyopita ilifanya kazi kwa mazoea iliteua watu kwa kutumia urafiki badala ya kuzingatia uwezo wa utendaji, ilifanya vitu kwa kusukumwa na uhitaji wa nje kuliko mikakati ya ndani na hilo ndilo lilisababisha tuhangaike kukirekebisha chama sasa,"alisema.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Comments
  +2 #5 Zindukani 2011-04-15 12:49 Kwa kuwa SIYO SIRI kwamba kwa sasa ili upate UBUNGE wa CCM NI LAZIMA KUWAPA RUSHWA (TAKRIMA) WANANCHI, maana yake ni kwamba MAWAZIRI WOTE WALIOTOKANA NA MFUMO HUU SIYO SAFI. Kwa hiyo mambo yamehama kutoka CCM yamehamia SERIKALINI. Yaani kwa busara ya kawaida tu huwezi ukatenganisha utendaji wa CCM na wa serikali iliyopo. RUSHWA kama ipo CCM ipo na SERIKALINI pia. UFI-SADI kama upo CCM SERIKALINI ndiyo umejaa kwani ndiko kwenye fedha ya wananchi – NA NDIYO MAANA KUNA MSURURU WA MIGOGORO KAMA: EPA, MEREMETA, RICHMOND, DOWANS,.
  POLISI, MAGEREZA, MAHAKAMA, NK. MALALAMIKO YA RUSHWA YAMEKUWA MENGI MPAKA YAMEZOELEKA KAMA NI MAMBO YA KAWAIDA TU! CCM WAMEKUWA WAKISEMA KWAMBA MALALAMIKO NI UCHOCHEZI WA WAPINZANI.
  MALIPO NA MANUNUZI HEWA KATIKA HALMASHAURI KARIBU ZOTE NI MAMBO YA KAWAIDA.
  HEBU JARIBU KWENDA KUTAFUTA TIBA KTK HOSPITALI YOYOTE K.M. YA RUFAA NDIYO UTAJUA NINACHOONGELEA (SIJUI KAMA WENZETU WABUNGE WANAYAPITIA HAYA)
  KATIKA JAMII YOYOTE, UKIONA RUSHWA IMEFIKA MPAKA KWENYE HUDUMA ZA AFYA (KWA MADAKTARI NA WAUGUZI) UKIONA NAO WAMEVUNJA VIAPO VYAO NA KUWEKA THAMANI YA FEDHA KATIKA UHAI WA MWANADAMU, UJUE HUKO KWENGINE NDIYO KUMEOZA KABISAAAA! YAANI KIMAADILI UJUE NCHI IMEANGUKA MPAKA CHINI KABISA. HAKUNA KUANGUKA ZAIDI YA HAPO. KILICHOBAKIA NI KUANZA KUINUKA TU.
  Kwa hiyo, CCM, kama kuna NIA YA KWELI YA KUJISAFISHA ILI KURUDISHA IMANI YA WANANCHI, KUJISAFISHA SERIKALINI PIA NI JAMBO LISILOEPUKIKA.
  KAMA CCM HAITAFANYA HILI ZOEZI SERIKALINI NA KWENYE TAASISI ZAKE BASI IMANI YA WANANCHI SAFARI HII NDIYO ITAKWISHA KABISA KWANI HILI ZOEZI LITAONEKANA NI MBINU ZILE ZILE ZA KULAGHAI ZILIZOTUFIKISHA KUJIVUA MAGAMBA.
  PAMOJA NA HAYO, JE CCM SASA IKO TAYARI KUKIRI HADHARANI KWAMBA AKINA SITTA, MWAKYEMBE, SELELI, NA WOTE WALIOTANGAZA SIKU ZOTE KUSIMAMA KWENYE HAKI WALIKUWA SAHIHI? JE WATATANGAZA RASMI KUWAOMBA RADHI NA KUWARUDISHA KUNDINI NA KUSEMA WAZIWAZI KWAMBA HAWA NDIO VIONGOZI WA MFANO WANAOWAPENDELEA ?
  Quote

  -3 #4 gava 2011-04-15 11:31 mimi naomba tusisahau kwamba rais ana majukumu pia ya kitaifa mbali na kuwa ni mwenyekiti wa chama tawala,hivyo tusubiri taratibu tuone mwisho wa maamuzi yake kama itakuwa ni ile dhamira aliyoweka hadharani au ni kile mnachofikiri ambacho kama anacho kakiweka moyoni.hata watoto wa chekechea wakihitimu wanapongezwa na kufanyiwa sherehe kwa hatua hiyo,huwezi kusema nataka umalize degree au phd ndo upongezwe. na mtu akimaliza mtihani anajipongeza kwa hilo bila kujali matokeo yatakuwaje. hongera kwa hatua hiyo Mh.RAIS
  Quote

  +1 #3 Gamba Beshubeo 2011-04-15 10:20 Uongozi wa UVCCM unahitaji kuundwa upya. Yaliyotokea Arusha hayakuwa mazuri. Kijana akawalaani mafisadi. Baadaye kijana huyo akafanyiwa mizengwe na jamaa wa mafisadi. Hivi CCM itajivua vipi gamba kama wanaokemea mafisadi wanaandamwa na CCM hiyo hiyo?
  Quote

  +3 #2 aieli nkya 2011-04-15 08:18 Makonda J.K hana lolote kujivua gamba kwa CCM sio kwa sumu imeondoka mwilini. Bado CCM kwa wananchi ni JANGA KUBWA
  Quote

  +4 #1 MBILIGI 2011-04-15 06:59 UVCCM na UWT-CCM zimetekwa na Mafisadi pamoja na Mwenyekiti wake JK ni ndumilakuwili.Jk,Msekwa,Chili gati,Wasira,meg hji na Makamba Jr pamoja na hizo Jumuia lazima ziondoke kabisaaaaaaa
  Quote  Refresh comments list
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  CCM itaweza tu kujivua gamba iwapo itafanya haya… Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:29

  [​IMG]GUMZO lililotawala katika kila pembe ya nchi yetu hivi sasa ni hatua ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mabadiliko ya uongozi katika sekretarieti na kuwatosa baadhi ya wajumbe mashuhuri wa vikao vya juu vya chama hicho katika ngazi ya taifa. Chama hicho kimesema kuwa kimechukua hatua hiyo ili kujisafisha na kuzaliwa upya, baada ya kuandamwa na tuhuma za ufisadi na mitafaruku isiyokwisha katika ngazi zote za chama hicho kwa muda mrefu.

  Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba ameondolewa katika nafasi hiyo pamoja na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti, huku wajumbe mashuhuri katika Kamati Kuu, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz wakipoteza nafasi zao kwa madai ya kuzongwa na tuhuma za ufisadi. Kwa muda mrefu sasa, baadhi ya wananchi ndani na nje ya chama hicho wamekuwa na dhana kwamba viongozi hao ni miongoni mwa wanachama wa CCM ambao wamekichafua chama hicho kutokana na tuhuma za ufisadi.

  Kwa kufanya hivyo, chama hicho kinasema kuwa kimejivua gamba la zamani na sasa kimejivika gamba jipya. Kwa maneno mengine, chama hicho kinawaambia wanachama wake na Watanzania waliokuwa wamekichoka kwamba gamba la zamani walikuwa akina Lowassa katika Kamati Kuu na akina Makamba katika Sekretarieti ambao sasa wametoswa. Kwamba kwa kufanya hivyo, sasa mshikamano ndani ya chama utakuwapo na chama hicho kitakuwa na dira na mwelekeo na hatimaye kitakuwa na mvuto kwa wananchi.

  Pamoja na kukipongeza chama hicho angalao kwa kubaini kuwa kimepoteza haiba miongoni mwa Watanzania, hatukubaliani nacho hata kidogo kwa dhana yake kwamba gamba la zamani walilojivua ni akina Makamba, Lowassa, Rostam, Chenge na wenzao waliotolewa katika Sekretarieti na Kamati Kuu ya Chama hicho. Tunasema hivyo kwa sababu matatizo yanayokisibu chama hicho ni lukuki na kitakuwa hakitendi haki kwa wanachama hao kusema kuwa ni hao pekee waliosababisha matatizo yote katika chama hicho.

  Lazima tuwe wakweli kwa kusema kuwa hekaheka ambazo chama hicho kinakabiliana nazo hivi sasa, kwa kiasi kikubwa zimesababishwa na vuguvugu zilizoamshwa na vyama vya upinzani kuliko wakati mwingine wowote katika maisha ya CCM. Chama hicho kilijisahau na kubakia na mfumo wa utendaji wa kizamani ambao uliwaweka kando wanachama wa ngazi za chini na kuwapa wanachama wachache wenye fedha, sauti na mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wengi. Ndio maana kelele zilizotawala kwa muda mrefu ndani ya chama hicho tawala zilihusu chama hicho kutekwa na wenye fedha.

  Hatusemi kwamba dhana ya kubadilisha viongozi ni potofu. Tunachosema hapa ni kwamba, baada ya kufanya hivyo, CCM pia ibadilishe mfumo mzima wa uendeshaji na ifuate mfumo wa chama cha siasa ili iweze kujivua gamba la chama Dola kwa lengo la kufanya mageuzi ya ndani kwa ndani yatakachokisaidia kuhimili vuguvugu la mfumo wa vyama vingi.

  Ndio maana wanazuoni wengi wanakiona chama hicho kuwa cha siasa kwa maana tu ya kusajiliwa, lakini uendeshaji wake umekuwa ukifanywa na Dola tangu enzi za TANU hadi Uchaguzi Mkuu uliopita. Mtafaruku katika chama hicho unatokana na ukweli kwamba chama hicho kimegundua kwamba katika hali ya sasa, Dola haiwezi kukilinda tena na kinapaswa kishindane katika uwanja sawa na vyama pinzani.

  Lakini pia chama hicho lazima kikubali kwamba, hata kama kimejivua sehemu ndogo ya gamba kwa kuwatosa akina Lowassa na Makamba, wananchi wanasubiri chama hicho kijivue gamba nene la kashfa nyingi ambazo mpaka leo hazijatolewa majibu, zikiwamo EPA, Meremeta, Kagoda, Rada, Deep Green, BoT, Richmond, Dowans, Kiwira na mikataba ya kifisadi ya madini na mingine mingi.

  Watanzania wanahitaji kujua waliohusika katika kashfa hizo ili washtakiwe na kurudisha fedha zao. Hawataki ngonjera na mashahiri yasiyo na mizani wala vina.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Laurent Gbagbo awe somo kwa viongozi Afrika Send to a friend Tuesday, 12 April 2011 20:12

  [​IMG]HATIMAYE Rais aliyekuwa aking'ang'ania madaraka nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo alikamatwa juzi na majeshi maalumu ya Ufaransa yakisaidiana na majeshi ya UN ya kulinda amani na yale yanayomtii mpinzani wake, Alassane Ouattara baada ya kujificha katika handaki nyumbani kwake wiki moja iliyopita. Kukamatwa kwa kiongozi huyo kunahitimisha mgogoro mkubwa uliozuka kati ya mahasimu hao wawili baada ya Rais Gbagbo kukataa kukabidhi madaraka kutokana na kushindwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini humo, Novemba 28, mwaka jana.

  Takribani miezi mitano tangu ashindwe katika uchaguzi uliopita, Rais Gbagbo alikuwa mtu aliyetengwa sio tu na wananchi wake, bali pia na jumuiya za kimataifa. Pamoja na kushawishiwa kuachia madaraka na AU kutuma marais watano, akiwamo Rais Jakaya Kikwete kumsihi akabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, Rais Gbagbo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi na hivyo ni rais halali.

  Lakini UN ambayo iliandaa uchaguzi huo, ilikubaliana na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwa Alassane Ouattara ndiye aliyeshinda uchaguzi huo licha ya Baraza la Ushauri lililoteuliwa na Gbagbo na ambalo lilisheheni marafiki zake kubatilisha matokeo hayo na kumtangaza Gbagbo kuwa mshindi kwa madai kuwa wasimamizi wa kura za mshindani wake walichakachua matokeo. Lengo la baraza hilo lilikuwa ni kumbakiza Rais Gbagbo madarakani kwa misingi ya uswahiba.

  Baraza la Usalama la UN na jumuiya za Ecowas na AU ziliamua Rais Gbagbo atolewe madarakani kwa nguvu na huo hasa ndio ulikuwa mwanzo wa mikikimikiki ya kumwondoa madarakani ambayo juhudi zake zilizaa matunda juzi wakati rais huyo alipokamatwa, baada ya kusababisha maafa makubwa ya vifo vya maelfu ya watu pamoja na umwagaji damu wa kutisha kwa sababu ya uchu wake wa kubaki madarakani kwa gharama yoyote.

  Itakumbukwa kuwa muasisi wa Ivory Coast, Rais Felix Houphouet-Boigny alipofariki akiwa madarakani mwaka 1993 bila kuwapo utaratibu wa kidemokrasia wa kurithishana madaraka, nchi hiyo iliyosifika sana barani Afrika kwa amani na utulivu wa aina yake iliingia katika mtafaruku mkubwa wa kisiasa. Ndipo Laurent Gbagbo alipopata upenyo na kuchaguliwa kuwa rais mwaka 2002 ingawa uchaguzi huo uliomuweka madarakani ulilalamikiwa kuwa uligubikwa na wizi wa kura.

  Mgogoro huo uliendelea hadi mwaka 2003 wakati nchi hiyo ilipogawanyika katika vipande viwili, kusini na kaskazini, hatimaye kuanza vita ya wenyewe kwa wenyewe. Gbagbo alitakiwa kuitisha uchaguzi mwaka 2005 lakini hakufanya hivyo, na aliendelea kuahirisha uchaguzi huo hadi Novemba mwaka jana wakati UN ilipoingilia kati na kuandaa uchaguzi huo ambao Alassane Ouattara aliibuka mshindi na Rais Gbagbo akakataa kumkabidhi madaraka.

  Tumelazimika kuorodhesha mlolongo wa matukio nchini Ivory Coast ili kuonyesha ni jinsi gani Rais Gbagbo alivyohusika kuitawala nchi yake kidikteta. Lakini pia tumefanya hivyo ili viongozi katika bara letu hili la Afrika wapate fundisho ili waache vitendo vya kufifisha demokrasia na utawala bora katika nchi zao, kwa maana ya kuingia madarakani kwa kuiba kura na kuweka mifumo haramu ya kisheria na kikatiba ili iwalinde waweze kubaki madarakani milele.

  Mkasa uliompata Gbagbo unapaswa uwe somo kwa viongozi wa Afrika ambao wameingia madarakani kwa gilba na wizi wa kura ili watambue kuwa wanakaribia kiyama, kwa maana kuwa jumuiya ya kimataifa haitafumba macho huku wakiendelea kuvunja haki za binadamu na kuminya haki za raia na kuwatawala pasipo ridhaa yao kwa kuweka mifumo ya kishetani inayolindwa na sheria na katiba za nchi zao.

  Mkasa uliompata Gbagbo ni mzuri. Watawala wa Afrika wamepata somo kuwa wakitawala kwa giliba na dhuluma wananchi watasema hapana. Na mifumo ya kimataifa itaingilia kati na kuwatia mbaroni kama wahalifu.Watakamatwa hata kama watachimba mahandaki yaendayo kuzimu na kuzimu.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,893
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Comments
  0 #10 2011-04-14 19:36 Gadafi ni muuaji tagu enzi na enzi,nani asiyejua kama ni gadafi aliyetoa majeshi kusaidiana na Nduli Idd amin dada wa Uganda na wakaua ndugu zetu wengi sana hususani wa kule Kagera?Mwnyezi mungu anasema kuwa hatachukua roho yako mpaka ulitenda utendewe,kama ni ya kheri mpaka utendewe ya kheri na kama ya shari mpaka utendewe ya shari,si kwa Gadafi tu ni kwa kila mtu .Jiandae.
  Quote

  0 #9 2011-04-14 15:49 Watoa maoni tuache kuongea kwa jazba na kukurupuka, bali tujue kuchambua, kutafakari na kutofautisha mambao. Gbagbo hawezi hata kidogo kuwa mfano kwa viongozi wengine wanaopenda kubakia madarakani kwani tatizo la Gbagbo ni tofauti. Kimsingi kilichomfanya Gbagbo abaki madarakani wala sio wingi au uchache wa kura za wananchi. KUNA ZAIDI YA HAYO. Tuulize sis tuliwahi kuishi Ivory Coast na Burkinafasso, kwani mgogoro wao kiini chake ni Ivory Coast na Burkina. Sisemi nani ni halali na nani ana haki, LAKINI siku za mbele zitatwambia kinachoendelea huko Ivory Coast. Kwa ufupi ni hayo.
  Quote

  0 #8 2011-04-14 15:37 NI AIBU KWA KIONGOZI KUNG'ANG'ANIA MADARAKA WAKATI WANANCHI HAWAKUTAKI KWA SABABU UNASABABISHA WANANCHI WAKO WAFE BILA SABABU JE UONGOZI NI BORA KULIKO UHAI? VIONGOZI HAMJUI KUWA DUNIANI TUPO SAFARINI?
  Quote

  0 #7 2011-04-13 21:51 Mbio za sakafuni..........................................
  Quote

  0 #6 2011-04-13 13:12 Hivi wewe Isra unataka kutuambia Waliompinga raisi wa Tunisia, Misri, Yemeneni n.k nao ni Vibaraka wa Marekani? Yaaaaaaaaaaani kila kitu mnapenda kumsingizia Marekani hata Ivory cost mtasema ni maagent wa magharibi.

  Yaani Isra unamjua Ghadaffi kuliko wananchi wake? unaangalia TV gani na kusoma magazeti gani wewe? Alipotuma jesshi na ndege zake na kuua watanzania wakati wa vita vya Idd Amin ulikuwa hujazaliwa nini?

  Ya ghadafi waachie Walibya wenyewe watanzania kimbelembele cha maandano ya kidini ni utumwa wa mawazo. Haya basi andamaneni kuhusu kukamatwa kwa Lautent Ghabo huko Ivory cost.
  Quote

  +1 #5 2011-04-13 10:47 Gbagbo awe mfano kwa marais wanaog`ag`ania madara ,awajibiswe ipasavyo.
  Quote

  0 #4 2011-04-13 09:28 Bado Mwai!!
  Quote

  0 #3 2011-04-13 09:11 Isra # 2 ... dada yangu isra je, unamjua Gadaffi au unamsikia?? kwa kifupi haeleweki yaani Leo ni hivi na kesho ni vile....! Wanaotaka uhuru wao sii waasi bali ni wademokrasia.
  Quote

  -1 #2 2011-04-13 08:58 Jamani Ggabo hafai lakin Muamar Ghadafi ni Rais mwema ninawachangaa waasi ni vibaka wa marekeani
  Quote

  0 #1 2011-04-13 04:09 Inawezekana baadhi ya viongozi wetu Africa wakajifunza kutoka kwa yaliyompata Gbagbo. Ubaya ni kwamba, viongozi wetu wanapenda madaraka mno. Angalia Zimbabwe na nchi nyingine za Africa. Raisi mmoja akiboronga, unaona kikosi cha maraisi kutoka nchi za kiafrica zinaenda kumpa PUSH ili aendelee kutawala. Libya ni mfano mzuri, Maraisi walienda kuongea na Ghadafi, lakini hawakumsaidia lolote. Wakaishia kunywa kahawa ya jangwani.
  Quote  Refresh comments list
   
Loading...