Mtanzania wa ughaibuni aipatia Busisi madawati

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Madawati.jpg


Kwa ufupi
Akikabidhi madawati hayo shuleni hapo jana, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Busisi, Safia Ibrahimu aliwaomba wadau wengine wa maendeleo katika kata hiyo kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu kwa kuchangia madawati na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.

Sengerema. Shule ya Msingi Busisi imepokea msaada wa madawati 80 yenye thamani ya Sh5.6 milioni kutoka kwa mmoja wa wadau wa maendeleo, Bahati Sanga unaolenga kupunguza uhaba uliokuwapo.

Akikabidhi madawati hayo shuleni hapo jana, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Busisi, Safia Ibrahimu aliwaomba wadau wengine wa maendeleo katika kata hiyo kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya elimu kwa kuchangia madawati na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.

Bahati ambaye ni mzaliwa wa Busisi anayeishi nje ya nchi, kwa mujibu wa Ofisa mtendaji huyo, alifikia hatua hiyo baada ya kuguswa na taarifa za upungufu wa madawati katika shule zilizopo katika kata hiyo na kuamua kuanza kuzisaidia.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Zamzam Abdakhary alisema shule yake yenye wanafunzi 883 ina madawati 221 kati 250 yanayohitajika.

Alisema bado wanahitaji msaada zaidi ili waweze kumaliza kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu sasa.

Mwalimu wa taaluma shuleni hapo, Mfungo Kasulilo alisema upatikanaji wa madawati hayo ni chachu kwa ufaulu wa wanafunzi wao huku akitamba kuongeza kiwango cha ufaulu mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambao kati ya wanafunzi 53 waliofanya mtihani wa darasa la saba, 40 walichaguliwa kujiunga na shule za sekondari.

Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Sengerema, Osca Kapinga alisema wamepunguza upungufu wa madawati kutoka 32,000 mwishoni mwa Machi mwaka huu hadi kufikia 23,500.


Chanzo: Mtanzania wa ughaibuni aipatia Busisi madawati
 
Amefanya vizuri, amekumbuka wajibu wake kwa kuwa alisoma kwa kodi zetu;
 
Back
Top Bottom