Mtanzania wa kwanza kuupanda Mlima Everest apewa zawadi ya Maziwa!

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Inashangaza na inasikitisha sana, Mtanzania wa kwanza kuupanda mlima Everest na kufika kileleni kurudi salama alipofika kwao Kilimanjaro wakamzawadia box la maziwa!

Hawa wa Kilimanjaro wakoje jamani?

Source: ITV
 
Chezea chaga wewe..wampe hela kabisaa..yewomii..maziwa yana nguvu mlaa
 
hivi nikwel huyo ndo wakwanza,
au ye ndo wakwanza kutangazwa

Ndio wa kwanza kuupanda hadi kileleni na kurudi salama. Ni achievement ya hali ya juu na anastahiki zaidi ya box la maziwa.
 
Inashangaza na inasikitisha sana, Mtanzania wa kwanza kuupanda mlima Everest na kufika kileleni kurudi salama alipofika kwao Kilimanjaro wakamzawadia box la maziwa!

Hawa wa Kilimanjaro wakoje jamani?

Source: ITV
Jamaa alifurahia maziwa,wewe kinachokuuma ni nini?
 
Dr. Mahathir Muhammad wa Malaysia aliposhika madaraka na kuanza kufanya mageuzi ya uchumi Malaysia na ili kuwapa moyo wa Malaysia wajione kuwa na wao wanaweza, alichukuwa vijana akawaambia kapandeni mlima everest, walipofika kileleni akautangazia umma kuwa Malaysia sasa iko "on top of the world" na inaweza kufanya chochote wanachofanya wengine, basi naam hiyo ndio ikawa chachu ya maendeleo Malaysia na ikawa hakuna kurudi nyuma kuanzia hapo.
 
Inashangaza na inasikitisha sana, Mtanzania wa kwanza kuupanda mlima Everest na kufika kileleni kurudi salama alipofika kwao Kilimanjaro wakamzawadia box la maziwa!

Hawa wa Kilimanjaro wakoje jamani?

Source: ITV

Kwani wakilimanjaro walimtuma ili akirudi wamzawadie au kwa utashi wake alienda huko. Na je aliposhuka alisema ni wa kilimanjaro au wa Tanzania? Embu tuambie Tanzania imemzawadia nini acha Majungu na chuki binafsi
 
Haya haya hayaaa tiririkaaaaaaa niliuliza jaman huyo mtanzania wa kwanza kujitangaza kupanda mt evarest amepata nini? Kumbe amepata box la maziwa? lol ngoja niurudie ule wimbo wangu wa mkoloni.
 
Kwani wakilimanjaro walimtuma ili akirudi wamzawadie au kwa utashi wake alienda huko. Na je aliposhuka alisema ni wa kilimanjaro au wa Tanzania? Embu tuambie Tanzania imemzawadia nini acha Majungu na chuki binafsi

Hapana si majungu wala chuki binafsi nawasikitikia sana wana Kilimanjaro kutokuona huyu mtoto wao aliejituma na kufika kilele cha dunia kwa nguvu zake. Ningefarijika sana angepatiwa mapokezi yanayostahili na kumuenzi, isitoshe, huyu kashukia kwao Kilimanjaro alistahiki zaidi ya box la maziwa..

Nna uhakika angeshukia kwetu tungemuenzi kwa mapokezi stahiki. Ngoja niongee na wazee wenzangu tumualike huku kwetu, aje tumuenzi.
 
Wamemsaidia kurudisha nguvu safi sana.Kunywa maziwa kwa afya yako.
 
Hapana si majungu wala chuki binafsi nawasikitikia sana wana Kilimanjaro kutokuona huyu mtoto wao aliejituma na kufika kilele cha dunia kwa nguvu zake. Ningefarijika sana angepatiwa mapokezi yanayostahili na kumuenzi, isitoshe, huyu kashukia kwao Kilimanjaro alistahiki zaidi ya box la maziwa..

Nna uhakika angeshukia kwetu tungemuenzi kwa mapokezi stahiki. Ngoja niongee na wazee wenzangu tumualike huku kwetu, aje tumuenzi.

Zomba wewe kama sio mwana CCM basi uko addicted na siasa zao maana kila kitu unafikiri sherehe na zawadi tu, Kilimanjaro hawako kama Mikoa mingine wakivuna mdundiko na sangura kila mtaa ili mradi wamepata sadolin moja ya mpunga kwahiyo inatakiwa iliwe iishe. Wale wako kimikakati zaidi na ndio maana kila ukitaja wenye maendeleo yasiyohusishwa na ufisaadi watano wachaga watakuwa watatu na mhindi mmoja na aliyebaki ndo mikoa mingine. Jifunze walichokifanya acha kulazimisha unayoyazoea ambayo bado yamekupa maisha duni mpaka sasa
 
Unaongea kama huwajui vile.

Yeye kupanda mlima huo imefaidisha nini anakotoka hadi awekwe juu? Kama imekuuma basi kampe zawadi wewe.

Kama siwajui nikiwajua itafanyaje, umeona zawadi gani wametoa kwa wengine waliotimiza hobby zao?
 
Huyu jamaa alitumwa na nani? Kama alienda huko Kwa gharama zake na kupanda mlima kwa raha zake basi hahitaji zawadi toka kwa mtu zaidi ya familia yake. Hivyo hayo maziwa bado ni zawadi kubwa kwake.
 
Back
Top Bottom