Mtanzania wa awamu ya kwanza hadi awamu ya tatu ya mzee Mkapa, alikuwa anaishi maisha yanayo aksi kipato chake

So far away

Member
Jan 7, 2017
58
121
Mtanzania wa awamu ya kwanza ya Mwalimu hadi awamu ya tatu ya mzee Mkapa alikuwa anaishi maisha fulani ambayo yalikuw yanaaksi kipato chake. Hakukuwa na maisha ya utajiri wa mwedo kasi kama wa awamu ya Nn
Kwenye awamu hizo tatu za mwanzo; Mwenye mali alikuwa yule alieachiwa urithi; au mtoto wa chifu ama mtu aliezitafuta mali kwa njia za halali. Si kwamba matajiri hawakuwepo la hasha walikuwepo ila walikuwa si wakutilia shaka. Ikimbukwe tu utajiri wa Lowasa waziri mkuu mstaafu ndo ulikuwa unatiliwa shaka tu!

  1. Kipindi hicho cha awamu ya kwanza; ya pili na ya tatu watanzania walikuwa na displine ya pesa. Ukiwa na sh. 10000 ulikuwa unaona kuwa unapesa nyingi sana na tena ilikuwa haionekani ovyo ovyo kwa kila mtu mfukoni kama note

    Katika awamu hizo tatu za mwanzo; vipato vya watanzania vilikuwa duni hata mishahara kwa watumishi wa uma ilikuwa ya chini sana ila maisha yalikuw yanasonga. Nakumbuka mwaka 2003 nikiwa naenda shuleni pale Njombe High School nilikuwa napewa na wazazi sh. elfu 15 kama pocket money kwa semester nzima. Ndio ilikuwa inatosha kwani pale vitumbua vilikuwa vinauzwa sh. 50 kimoja. Anadazi sh 50; bagia sh 25 mkate mzima sh 500. Maisha yalikuwa ya saizi yetu. Hata nauli.kutoka nyimbani Kyela hadi mbeya mjimi ilikuwa sh 1600. Mbeya hadi njombe ilikuwa sh 2000 kwahiyo total nilikuwa natoa sh 3600 nauli ukilinganisha na sasa ambapo ni zaidi ya 18000!

    Kipindi kile mfumko wa bei haukuwepo kama ilivokuwa katika awamu ya nne.

    Kipindi hicho cha awamu hizo tatu. wamiliki wa magali walikuwa wakuhesabu. Si kama ilivokuwa imefikia kwenye awamu ya nne ambapo hata mtoto wa juzi ulikuwa unashangaa anaendesha gali tena lake! Ilikuwa si ajabu kukuta nyumba moja ina magari zaidi ya mawili!

    Ndo kipindi hicho ambapo watumishi wa serikali walikuwa wanaheshimika mitaaani. Kwani wao ndo walikuwa na uhakika wa maisha au wa vipata kwa mwezi kupitia mishahara. Kada kam za uwalimu na manesi pia polisi na majeshi walikuwa waaheshimika. Kwanza ukiwa na rafiki shuleni ambae wazazi wake ama mmoja wa wazazi wake ni mtumishi serikalini ulikuwa unafaidi sana. Pia watoto hao wawayumishi walikuwa wanaonewa gere!

    Kipindi kile vipato vyetu vilikuwa vianakuwa pole pole. kutokana na hali zetu.

    Nakumbuka pia kwenye tamasha la wasanii wa kipindi kile akina : Juma Nature;Ferooze; Dudu Baya; Profeser J; Mwana FA akina AY ; Mr Nice nk. wakija pale ukumbi wa Dhando Mbeya viingilio vilikuwa vya kawaida sana tena saa sh. 1500 hadi 2500. Hata na Wao ( wasanii ) walikuw wakupiga shoo zao kwa sh. elfu 50. Na maisha yalikuwa yakisonga mbele. Na walikuwa wakitanua mjini kwa malipo hayo hayo ya shoo za elfu 50. Maisha yalikuwa standard kulingana na maisha ya mtanzania. Tulikuwa tunaishi maisha halisi ya kwetu!

    Ada za shule za private.

    kipinndi kile ada za shule za private zilikuwa reasonable. Zilikuwa za bei ya chini japo kuwa zilikuwa za ma Laki kadhaa. Hazikuwa za ma million kama sasa. Nakumbuka mdogo wangu alipofeli la saba alipelekwa Shule ya private ya kibaptist Kipoke iliiyo pake Kiwira. Ada yake ilikuwa sh. Laki mbili na 50 kwa mwaka. Shule kali kama. Meta ; Sangu, Swila; Lutengano ; Ndembela nk ada zao zilikiwa zikirange kwenye Laki 4 hadi Laki 5. Mambo yalikuwa safi japokuwa kwa kipindi hicho kupata hizo laki jwa wazazi ilikuwa ngumu. Na ndio maana kipindi kile kumpeleka mtoto shule ya private ilikuwa inshu kweli kweli. Hata wanaosoma huko walikuwa wa tofauti sana na walikuwa na busara na heshima kwanj walikuwa wakihurumia wazazi wao.

    Nakumbuka kipindi kile picha moja kwa camera man ilikuwa sh 250 ; daftari counter cuire 4 ilikuwa sh 2000 kushon suruawali ilikuwa sh 2500 du!

    Kodi za nyumba na viwanja.

    kipindi cha awamu ya 1;2 na 3 viwanja vilikuwa vinauzwa kwa bei ndogo sana hata kodi ya nyumba ilikuwa ndogo sana. Chumba kizuri chenye hadhi kabisa na kila kitu kipo ilikuwa sh 20000 kwa mwezi. Chumba cha kawaida kabisa ambacho hakina umeme wala sakafu ilikuwa ni sh 3000 kwa mwezi. Kwa hiyo kipindi kile vyumba vya sh 3000 hadi 10000 vilikuwepo. Tena kati ya 10000 hadi 20000 vilikuwepo vingi sana. Ndo kipindi kile tulikuwa tunamshangaa Mr. Nice aliyekuwa Maarufu sana kama Dimond wa sasa alikuwa akiishi nyumba ya sh 50000 kwa mwezi. Tulikuwa tunaona kuwa anaishi maisha ya anasa sana .

    Hakika ; tunaweza tukachukuwa muda mwingi sana kuelezea jinsi gani maisha yalikuwa kipindi hicho cha awamu 3 yaani kuanzia miaka ya 2004 kwenda chini.

    Awamu ya Tano; Awamu ya mdororo na Maisha ya Maigizo!

    Awamu ya tano yenye kauri mbiu ya "Ari Mpya; Nguvu Mpya; Kasi Mpya" Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" ilipoanza miaka ya 2005 hadi 2015 ndo watanzania tukahama mfumo wetu wa maisha na tukaishi maisha mengine kabisa ambayo yalikuwa si yetu. Wengi sana waliumia sana na wengine wachache sana kama akina Saidi Lugumi kuneemeka vya kutosha.

    Hapo tulianza kushuhudia nchi ikihama na kuyumba yumba kiuchumi huku ikifata matakwa ya mabepari.

    Tulianza kuona kila mtu akiwa fisadi! Kila mtu aliepata nafasi alihakikisha Amechuku Chake Mapema. Ilifika wakati mtu akipata kanafasi kidogo tu wengine wanasema eti jamaa Ameula!
    Maana yake atameki sana. Raisi aliyekuwepo alikuwa Laiser faire! Yeye mwenyewe alikuwa mtu wa ughaibuni kila week! Ndo tukaanza kuona mengi yakibadirika kwa kasi. Mfumo wa maisha ikibadirika kwa kasi.

    Upandishwaji na nyongeza za mishahara holela sambamba na umbandaji bei kwa bidhaa holela.

    Kwenye awamu ya tano yenye kauri mbiu ya Ari Mpya; Nguvu Mpya Kasi Mpya . Maisha Bora kwa kila Mtanzania tulishuhudia mishahara ikipanda na kuongezwa mara dufu huku nako ubandaji wa bidhaa masokoni ukienda sambamba na hali hiyo!
    Ile mishahara ya watumishi wa umma ya elfu 70 hadi laki kwa nwezi ilipanda hadi kufikia kati ya Laki 7 hadi ma milions of wages. Kila mwaka mishahara ilikuwa ikipanda na katikati ya mwaka nyongeza za mishahara zilikuwa bwerere!! Sasa hali hiyo ilisababisha mfumuko wa bei mitaani bei za bidhaa zikaanza kunadilika gafla. kil siku vitu vinapanda bei! Lile Andazi la sh. 50 sasa likawa linauzwa sh. 100 hadi 500!

    Kodi za nyumba na viwanja vilipanda juu.
    Wamiliki wa nyumba nao waliona wapandishe bei za vyumba kwa wapangaji. Vyumba vikawa juu sana mpaka kati ya sh. 40000 hadi 50000 chumba cha kawaida. Nyumba nzuri nzuri bei ikawa mpaka elfu 70 kwa single na double self ikawa 150000.

    Tena wamiliki wa nyumba wakajuanzishia na kautartibu kao k kudai kodi ya miezi sita sita. Kwa hiyo mpangaji inambidi alipie miezi sita kodi ndo aingie! Mambo yabadirika sana.

    Viwanja navyo vilianza kuwa bei maradufu.

    Ada za shule za private

    Ada za shule za private zilipanda kqa kasi. Zile ada za malaki za kawaida sasa zikawq za mamilioni. Mpaka sasa utasikia shule hata ya chekechea ada ni milioni 3 na uchee!!

    Kila kitu kilikuwa juu sana kwa bei.

    Je ni kweli watanzania walikuwa wakimdu gharama hizo? Au ndo ilikuwa level yetu ya maisha ? Lahasha si kweli.

    Hii kauri mbiu ya Maisha Bora Kwa Kila Mtabzania ilitekelezwa vibaya. Mh. Raisi wa awamu hiyo na washauri wake waliitekeza ndivyo si vyo. Wao waliamini wakimga mahela kila kona; wakiwaacha watu wapige dili watakavyo; wakiwaacha watu wafisidi nchi yao watakavyo n kupndisha bei kwa bidhaa ndo kuwapa Maisha bora watanzania. Na ndio maana kw hali hiyo uchumi wa tanzania ulidorora sana Mpaka ka nchi kama Burundi kanatuzidi uchumi. Kwa sasa hela yao iko juu kulio ya tanzania licha ya mzozo wa vita walionao kila mwaka.

    Kwa hali hiyo shiling ya Tanzania ilishuka sana dhamani. Ndo maana hadi leo noti ya sh. 10000 haina dhamani tena. ulishaicange imekwisha!. Leo hii si ajabu ukakuta mtoto wa darasa la.tatu anayo mfukoni mwake kapewa na wazazi kama pocket money. Hii ni kwamba vituu viki juu sana na hela imeshuka dhamani.
    Ndo kipindi cha awamu ya nne kuokana n esa kupigwa kila kina kwa walikuwa na nafasi qa kuzipiga; tulikuwa tunaona ongezeko la magari ya kila aina mjini. Ongezeko la.majumba ya kifahari ya vati la msauzi kila mhali; ongezeko l magirofa ya maana kila mahali; ongezeko ya mabaa na kumbi za starehe zikiota nchini kila sehemu kama uyoga.
    Ma shell ( Petrol station) nayo hayakuwa nyuma. Yaliotesha barabani kama uyoga. Mijini yaliota kama uyoga. Hii ni kutokana na pesa kuwepo na kuzagaa mtaani kama mchanga.
    Kipindi hucho watumishi walikuwa safi;wafanya biashara walikuwa safi na hata baadhi ya wananchi walikuwa safi pia!

    Swali la kujiuliza; Je nikweli chumi wa nchi hupimwa kwa kuwepo na maisha ya juu kwa vituu kuuzwa bei kubwa na kuwepo kwa pesa mitaani kama mchanga?

    Nahisi hapana. Uchumi hauko hivo? Nchi ya kenya ambayo inauchumi imara sana hapa Afrika mashariki hali haiko hivo. Leo hii pale kenya Note kubwa ni ya ksh 1000 tu. Pale kenya ksh 10 ksh 15;ksh 20; ksh 50 bado zinatumika tena sana. Utashangaa unakula sahanu ya wali nyama kwa mama ntilie kwa ksh 80.
    Maisha mazuri si mfumko wa bei!

    Haikuwa na haja ya kuongeza mishahara kila mwezi huku kukiwa na mfumko wa bei kwa bidhaa kila saa.

    Awamu ya Tano.

    Awamu ya tano ya ndugu Mh. Raisi John Joseph Pombe Magufuli inekuwa suluhisho la kila kitu. Hii awamu ya Hapa Kazi Tu inaturudisha watanzania kuishi maisha yetu halisia; maisha yetu wenyewe ambayo si ya maigizo. Kwamba fanya kazi ndo upate pesa. Hakun pesa za kona kona.

    Kama tunavyoona mkuu huyu ana miaka miwitu madarajani ila kashafanya makubwa sana. Karekebisha kila pahala.

    Sasa watanzania tulichepuka kwa miaka 10 tukiishi maisha ambayo si yetu sasa leo hii tunaona taabu kurudi nyuma. Tumesahau tulikotoka. Maisha yetu tumeshayasahau kuwa hayakuw ya level hii.

    Mambo kila pahala yamegoma. watu tunalia lia ovyo tukisema pesa imepotea! Pesa mtaanu haionekani!!

    Raha iliyoje kwa wapangaji kuaga mfumo kandamizi wa kulipia kodi ya nyumba miezi sita sita!

    Kwenye Awamu hii ya Tano sina haja yakusema mengi maana wote tunajionea.

    My take!

    1. Raisi wetu akaze uzi huu huu.

    2. Apunguze bei za bidhaa na kudhibiti mfumko wa bei.

    3. Mishahara kwa watumishi ibaki hii hii iliyopo isiongezwe. Endapo imeongezwa Mfumuko wa bei udhibitiwe.

    4. Adhibiti ada kubwa za ma millions of money kwa taasisi binafsi.

    5. Wakenya walojazana kwenye taasisi nyingi binafsi mathalani taasisi za elimu kutimuliwa kama alunvofanya mwalimu kwenye azimio la Arusha. Hii ni kutokana na vijana wengi wa kitanzania kukosa nafasi za kazi.
 
Back
Top Bottom