Mtanzania ukweli ni huu; Nchi haina malighafi za kutosha kuvutia viwanda,viwanda ni ndoto

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Nimekuwa nikijiuliza,hii Tanzania ya viwanda itatumia malighafi gani kuviendesha hivyo viwanda?

Kanda ya ziwa wakulima wameacha kulima pamba ambayo ingelisha viwanda vya nguo.

Kilimanjaro na mbeya na maeneo mengine yanaacha kwa kasi kulima kahawa ambayo ingetumika katika viwanda vya kahawa.

Alizeti pale singida haitoshi kuendesha kiwanda kwa miezi 12,non stop kwa masaa 24.

Zabibu za dodoma ni kama hazipo.

Korosho pia hazitoshi kuwa processed na kiwanda,mfululizo kwa miezi 12.

Matunda ya tanga hayafai au hayana viwango vya kumudu soko,na hata kama yana. viwango,hayatoshi kuendesha kiwanda kwa mwaka mzima.

Mpunga hauzalishwi kwa kiwango cha kutosha kufanya processing kwa mwaka mzima,pia hata mahindi,ndio maana kila siku serikali inazuia export.

Chuma cha liganga kimeimbwa miaka tele kumbe hakina viwango kama ilivyo kwa makaa ya mawe ambayo dangote aliyapiga chini

Reli ya Ku support viwanda iko wapi?

Viwanda vya samaki vinakufa,samaki hakuna ziwani,hata vile tulivyoambiwa eti vitajengwa kwenye ukanda mreefu wa pwani,havipo,

Mpaka sasa hakuna mkoa ulioainisha malighafi zilizopo na kufafanua zinaweza Ku support Tanzania ya viwanda kwa kiasi gani

Tumekwama na hatutatoka hapa!!!!
 
Wewe unadhani kwa kilimo hiki cha kubangaiza mvua tutatoka na ili tutoke ilibidi tuanze na mapinduzi ya kilimo ndio mapinduzi ya viwanda yafatwe sasa kilimo chetu chenyewe kinategemea mvua za msimu sasa zimekata siku hizi haziji kwamsimu uliozoeleka.
 
Malighafi zipo, akili ndo hakuna..... Kama utakuwa na policy makers wanaweka akili mfukoni, wanatumia resources rafu rafu tu.. viwanda utavisikia kwa wengine hata kama ukimwagiwa resources... mfano tu: tunasikia daraja la mto wami li karibu kuanguka, unajiuliza ni kwanini isingefanyika allocation nzuri ya resources badala ya kujenga yale madaraja matatu ya mwendokasi ambayo yanatutoa jasho asubuhi, ni kwaninihizo resources zisingetumika kujenga daraja la mto wami?.... AKILI HAKUNA
 
Kweli kabisa mkuu
 
Aiseee wafuasi wa chadema akili zao ni kama za mwentekiti wako. Huko ulaya walikojenga viwanda wana malighafi? Japani wanakotengeneza magari wana malighafi za chuma? Aiseew chama kikiongozwa na Mr Ziro wafuasi wake wanakuwa kama mataahira vile
 
Viwanda jambo zuri japokua lilitamkwa kisiasa kama ahadi nyingi zilizopita huko nyuma hivyo kutimia kwake kuna mashaka.

Tungeanza na mapinduzi ya kilimo yaende sambamba na uanzishaji ya viwanda vidogo vya kuongeza thamani

Ila haya yote yanahitaji mipango ya kisayansi na sio siasa. Nahisi serikali ingeomba wanasayansi wa uchumi waandae mkakati kazi kuelekea kwenye viwanda na wasiubane ktk miaka 5 ama 10 ya utawala wao, waache uandaliwe mkakati wa muda mfupi, wa kati na mrefu kwani nchi ya viwanda it is not an overnight success
 
Malighafi zipo, akili ndo hakuna..... Kama utakuwa na policy makers wanaweka akili mfukoni, wanatumia resources rafu rafu tu.. viwanda utavisikia kwa wengine hata kama ukimwagiwa resources... mfano tu: tunasikia daraja la mto wami li karibu kuanguka, unajiuliza ni kwanini isingefanyika allocation nzuri ya resources badala ya kujenga yale madaraja matatu ya mwendokasi ambayo yanatutoa jasho asubuhi, ni kwaninihizo resources zisingetumika kujenga daraja la mto wami?.... AKILI HAKUNA
kiwanja cha chato sidhani kama kina umuhimu kuliko daraja la wami. ndio ujiulize mara mbilimbili
 
Haya,wewe mkara andika na sisi tuone
Kila ulichoandika hapo kina solution lakini naona umeorodhesha matatizo na kuyatupa mitandaoni huku.
Badili mindset hiyo.

JAPAN hakuna hata zambarau zile ulizokuwa unaziponda lakini kuna viwanda hakuna mchezo. Mfano mdogo Mbunge Aliambiwa mkoa wako kuna Madini ya bati, fikirisha kichwa bati zipatikane akabaki anatoa macho tu.
Sababu zote ulizotoa hazizuii tanzania kuwa na viwanda ni ndogondogo sana
 
Bati kwa kiwango kipi? Kuzalisha bati mia madini yanaisha?
 
Ukimuuliza waziri wa viwanda anakuambia yeye anaona viwanda vinakuja vingi tu, hapo ndio huwa najiuliza, hawa viongozi wetu wanaelewa viwanda vinavyohitajika?
Au zile wanamaanisha viwanda vya kutengenezea makalai
 
Back
Top Bottom