Mtanzania Single Mtambalike, Ashinda Tuzo ya Filamu Bora Ya Kiswahili, Afrika!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,317
Ma Star wa Bongo Movies wa Kitanzania, Watanzania, Single Mtambalike, "Richie Rich", na Elizabeth Michael, Lulu, wameshinda tuzo ya filamu bora ya katika tuzo za filamu bora za Afrika huko Nigeria usiku huu.

Richie ameshinda kupitia filamu yake ya Kitendawili aliyocheza na Mona Lisa na kutengenezwa na kampuni ya Proin, ameshinda katika kipengele cha ‘Best Indigenous Language Movie/TV Series/ Swahili.’

Lulu ameshinda kupitia filamu yake ya Mapenzi ambayo nayo imetengenezwa na Kampuni ya Proin.

Kwenye tuzo hizo, waigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Richie’ Mtambalike na Yvonne ‘Monalisa’ Cherry wanawania Tuzo.

Lulu alitajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha Best Movie – East Africa kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu pamoja na Monalisa kupitia Daddy’s Wedding.

JF pia ipo ukumbini hapo ikiwakilishwa na mwana jf Le Mutuz, hope soon ataripoti.

Mwanamuziki wa Tanzania, Ali Kiba atatumbuiza katika tuzo hizo.

Tuzo hizo kubwa za filamu Afrika, zitaoneshwa live kupitia channel ya Africa Magic na Maisha Magic East kwenye DSTV.

My Take.
Sisi wengine huwa hatuangalii bongo movies kwa sababu ya mambo ya hovyo hovyo na ujinga ujinga mwingi, lakini kitendo cha movi za kibongo kuanza kushinda tuzo za kimataifa, labda kutaturudishia attention yetu kurudi kutazama Bongo Movies, tangu alipofariki Kanumba, kwa wengine wetu, alikufa na Bongo Movie, landa sasa Kanumba kapata mrithi, hivyo kupandisha tena chati ya bongo movies!.

Hongera Richie Rich!. na Lulu japo amenikera kuja kupokea tuzo na nyonyo nje, lakini pia Hongera zake.

Pasco

Star wa Bongo Movie wa Kitanzania, Single Mtanzania, Single Mtambalike, "Richie Rich", meshinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili katika tuzo za filamu za aAfrika huku Nigeria usiku huu.

Source:AMCA TV Live from Lagos, Nigeria.

Pasco

hongera yake.

ht ivyo ametoka mbali sn, nakumbuka enz za bishanga, aisha na waridi ktk 'mambo hayo' kupitia itv.
 
Attachments

  • 1457205383297.jpg
    1457205383297.jpg
    14.9 KB · Views: 91
Star wa Bongo Movie wa Kitanzania, Single Mtanzania, Single Mtambalike, "Richie Rich", meshinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili katika tuzo za filamu za aAfrika huku Nigeria usiku huu.

Richie ameshinda kupitia filamu yake ya Kitendawili aliyocheza na Mona Lisa na kutengenezwa na kampuni ya Proin, ameshinda katika kipengele cha ‘Best Indigenous Language Movie/TV Series/ Swahili.’

Kwenye tuzo hizo, waigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Richie’ Mtambalike na Yvonne ‘Monalisa’ Cherry wanawania Tuzo.

Lulu alitajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha Best Movie – East Africa kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu pamoja na Monalisa kupitia Daddy’s Wedding.

JF pia ipo ukumbini hapo ikiwakilishwa na mwana jf Le Mutuz, hope soon ataripoti.

Tuzo hizo kubwa za filamu Afrika, zitaoneshwa live kupitia channel ya Africa Magic na Maisha Magic East kwenye DSTV.

Pasco

Sifa nyingine bhana ni sawa na kusema Mjapani ameshinda mashindano ya Sumo Duniani na nchi yote ya Ujapani isimame na kushangilia!!!
 
Back
Top Bottom