Mtanzania (Profesa Kennedy Gastorn) achaguliwa Katibu Mkuu Jumuiya ya Sheria ya Afrika na Asia

salaama

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
251
325
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)

gastorn.jpg

Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kennedy Gastorn amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika-‘Asian-African Legal Consultative Organisation-AALCO’.

Profesa Gastorn alichaguliwa kwa kauli moja wakati wa Mkutano wa 55 wa Jumuiya hiyo yenye jumla ya nchi wanachama 47 uliofanyika Mjini New Delhi, India tarehe 17 Mei, 2016.

Aidha, Profesa Gastorn ambaye alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Tanzania na kupitishwa na Umoja wa Afrika, anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Profesa Rahmat Mohamad wa Malaysia ambaye muda wake unamalizika rasmi ifikapo mwezi Agosti, 2016na Profesa Gastorn anatarajia kukabidhiwa madaraka hayo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2016.

Mkutano wa Jumuiya ya AALCO ulifanyika kuanzia tarehe 16 Mei na kumalizika tarehe 20 Mei, 2016.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 20 Mei, 2016.
 
Tanzania inang`aa kimataifa. Ni hatua nzuri sana kwenye mambo ya kidiplomasia na faida katika nchi yetu.
 
Hongera zake afanye kazi, alinde heshima ya Taifa. Ila haya majina yetu unaweza ukafikiri ni Mzungu.
 
Kuchaguliwa sio tatizo bali wawe mstari wa mbele kurekebisha kasoro za kisheria nchi kwetu hasa kwenye mikataba ya uwekezaji.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)

gastorn.jpg

Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kennedy Gastorn amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika-‘Asian-African Legal Consultative Organisation-AALCO’.

Profesa Gastorn alichaguliwa kwa kauli moja wakati wa Mkutano wa 55 wa Jumuiya hiyo yenye jumla ya nchi wanachama 47 uliofanyika Mjini New Delhi, India tarehe 17 Mei, 2016.

Aidha, Profesa Gastorn ambaye alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Tanzania na kupitishwa na Umoja wa Afrika, anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Profesa Rahmat Mohamad wa Malaysia ambaye muda wake unamalizika rasmi ifikapo mwezi Agosti, 2016na Profesa Gastorn anatarajia kukabidhiwa madaraka hayo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2016.

Mkutano wa Jumuiya ya AALCO ulifanyika kuanzia tarehe 16 Mei na kumalizika tarehe 20 Mei, 2016.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 20 Mei, 2016.

Wow!! Hongera sana, he is a good guy, modest and knowledgeable in legal matters (especially land law) and, on top of it, he was my Academic Advisor at UDSM.
 
Kama Tanzania hatujui kafanya nini, hakukuwa na haja ya kumposti humu,hawa ndio wasomi wanaojificha kwenye makabati,jamii haiguswi na usomi wake,labda jinsia ya pili wa pale law school
 
Back
Top Bottom