Mtanzania mmoja akamatwa kwa kusafirisha wahamiaji 16 wa Ethiopia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,236
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ametangaza kuwa polisi wamemkamata raia mmoja wa Tanzania akihusishwa na usafirishaji wa wahamiaji haramu 16 wa Ethiopia, na kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo ni Yohana Adam, mkazi wa Kasumulu katika wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Matei amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Jumapili jioni wakati aliposafirisha wahamiaji hao haramu kwenda Afrika Kusini kupitia nchi jirani ya Malawi. Waethiopia hao walisafirishwa kwenye gari lililoendeshwa na mshukiwa, na wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 11 na 18.

Aidha polisi pia wanawasaka washukiwa wengine sita ambao wanadaiwa kuendesha kundi la biashara ya binadamu katika mkoa huo.


Swahili.cri
 
Kumaliza haya serikali isiwabanie waethiopia iwaache wapite tu wanaenda south africa kujaribu maisha ,kwa nn tunabaguana ?? Kiac hicho

sent from HUAWEI
 
hawawaethiopia si wahamiaji harama muamiaji haram akamwatwi kizembezembe mbona hatuwasikii nchi nyingine wakiwa wanakamatwa kama hawa mimi naona sasa tuwaite ni wakimbizi tu wanaendatafuta hifadhi salama huko afrika kusini..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom