Mtanzania la leo: Polisi "wawawinda" waandishi wa habari wengine

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limesema limepata taarifa zinazoonyesha kuwa, Jeshi la Polisi Mkoani Iringa, lina mpango maalum wa kuwashughulikia baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Jukwaa la Wahariri Tanzania, limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

“Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari, Mkoa wa Iringa, aliuawa akiwa kazini juzi wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

source: Mtanzania la leo


 
Hizi tuhuma sio za kupuuza inabidi waziri wa mambo ya ndani atoe tamko haraka sana.Ili waandishi wa habari wawe na amani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom