TANZIA Mtanzania Johnson Mdoe auawa kwa risasi Marekani. Polisi watangaza dau kwa yeyote mwenye taarifa

MSATULAMBALI

Senior Member
Apr 1, 2012
187
53
Polisi mjini Dallas wameomba msaada wa kumpata mtuhumiwa wa mauaji ya mhamiaji kutoka Tanzania, Johnson Mdoe Mchaina ambaye alikuwa anafanya kazi usiku kusaidia familia yake iliyopo Tanzania anapotoka.

Hivi ya CCTV inamuonyesha mtuhumiwa akimpiga risasi Johnson na kuchukua maisha yake. Tukio hilo lilitokea saa 8:45 usiku tarehe 9 July 2020 ambapo muuaji alimkuta Mdoe yuko peke yake.

Wafanyakazi wenzie wamemuongelea Mdoe kama mtu mzuri sana na alikuwa na mtoto wa kike nchini Tanzania na alijitahidi sana kumhudumia.

Mtuhumiwa ambae alikfika kufanya tukio la uhalifu alimuamuru Mdoe kwenda kwenye Rejesta, akiwa nyuma ya kaunta huku mhalifu huyo akiwa na wasiwasi na kutoishikilia vizuri silaha yake.

Mdoe alimfungulia trei na mhalifu kuchukua pesa lakini alishindwa kumfungulia ya pili, alitumia sekunde kadhaa na alionekana kuwa na hofu wakati silaha ikiwa inamzunguka na ghafla akapigwa risasi.

Mdoe alijaribu kumshika mtuhumiwa, aligeuka na kumpiga risasi, alisema Lopez ambae ni afisa wa polisi. Imetangazwa malipo ya dola 15,000 kwa taarifa itayopelekea upatikanaji wake na afisa wa polisi ana imani kuna mtu anajua jina lake au jina la utani.

 
Ameuliwa.

"Apigwa risasi" inatumika kwa ambae hakufa.

Afisa upelelezi kasema, baada ya kutii amri za awali za kumpa hela, marehemu alijaribu kumpora bastola jambazi. Ikapelekea kuuawa kwake. Labda hapo kuna somo la kujifunza.

7-11 nao nadhani wana kesi ya uzembe ya kujibu. Mtumishi alikuwa peke yake dukani. Hakupaswa.
 
1ca7b374-1e4b-4b62-b526-dec28ff9f8bc.jpg

8b29ff40-f0c9-4ab5-a9d1-d9e482907825.jpg

53307f83-07ec-4331-ab8b-697515ed801e.jpg

26fd6daf-62aa-4cc4-a4c8-2eacf1000271.jpg

3db648ff-0d3d-45e6-85a8-4291efe7ea67.jpg

2276ca86-bb59-4330-89db-d6af631f903d.jpg
 
Ameuliwa.

"Apigwa risasi" inatumika kwa ambae hakufa.

Afisa upelelezi kasema, baada ya kutii amri za awali za kumpa hela, marehemu alijaribu kumpora bastola jambazi. Ikapelekea kuuawa kwake. Labda hapo kuna somo la kujifunza.

7-11 nao nadhani wana kesi ya uzembe ya kujibu. Mtumishi alikuwa peke yake dukani. Hakupaswa.
Achana na google translator mkuu
 
pumzika unakostahili baharia

wakati mwingine maisha ndivyo yalivyo ni ajali kazini

get rich or die trying
 
Dalas, Texas.

Polisi katika jiji la Dallas, Texas nchini Marekani imeahidi kutoa takribani dollar za kimarekani 15,000 sawa na shilingi za kitanzania takribani 35mil kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu aliyemuua kijana wa kitanzania Johnstone Mchaina Mdoe.

Mdoe aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu aliyefunika sura yake mnamo Mwezi wa July.9.2020 kwenye duka alilokuwa akifanyia kazi.

Pole kwa ndugu na wote wanaoguswa na msiba msiba huu.

Angalia video footage hapa chini.


 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom