Mtanzania Jennifer Shigoli atajwa kuwa Mjasiriamali bora Afrika 2016

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jennifer-AEAward-750x375.jpg



Mtanzania Jennifer Shigoli ni miongoni mwa washindi 11 wa shindano la wajasiriamali wa Afrika baada ya kufanikiwa kutwaa ushindi katika kategori ya kwanza na kuondoka na dola za Marekani 150,000.

Akitangaza washindi hao walioko katika kategori ya elimu, mazingira na mengineo, Rais wa benki ya BMCE, Othman Benjelloun alisema tuzo hizo zimetolewa kwa wale waliofanya vyema katika kuleta hali bora ya ujasiriamali na kuwa na biashara endelevu.

Mtanzania huyo ametoa tuzo hizo katika kategori ya elimu kupitia taulo za usafi – “Reusable Sanitary Pads”

Tuzo hizo ambazo zinatolewa kwa ushirikiano kati ya BMCE Bank of Africa na African Entrepreneurship Award zimetengewa dola za Marekani milioni 1.

Washindi hao 11 ni miongoni mwa washiriki 37 waliofikia fainali ambao walikuwapo katika Boot Camp mjini Casablanca, Morocco kuanzia Novemba 30 hadi Decemba 3, 2016.

Washindi hao ni kama ifuatavyo:

Nafasi ya kwanza ya tuzo $150,000

-Mazingira: Mahmud Johnson – Liberia – “Oil Palm products”

-Elimu: Jennifer Shigoli – Tanzania – “Reusable Sanitary Pads”

Nafasi ya pili tuzo $100,000

-Mazingira: Ernie Aylward – Afrika Kusini “Electric mini-cabs”

-Elimu: AbideenAdelu – Nigeria – “Mobile application for students”

-Mengineyo: Joyce Kyalema – Uganda – “Pumpkin food”

Tuzo za wanaochipukia, $50,000

-Frederico Peres da Silva – msumbiji – “Connect blue-collar, informal workers to customers”

-Achiri Nji – Cameroon – “Live status updates on road conditions”

-Benti Gelalcha – Ethiopia – “Veterinary Ambulatory Clinical Services”

-Murtula Sanni – Nigeria – “Online platform for skilled workers”

-Omar Kadiri – Morocco – “Free phone credit”

Tuzo za African Entrepreneurship zilitangazwa Novemba 2014, mjini Marrakesh, na Mwenyekiti Othman Benjelloun katika mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali (Global Entrepreneurship Summit), ikiwa na lengo la kuboresha ujasiriamali na kuwashawishi wajasiriamali kuanzisha biashara, kuziendeleza kutengeneza fursa za ajira na kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika.
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    135.8 KB · Views: 68
Back
Top Bottom