Uchaguzi 2020 Mtanzania hasa mwanatunduma, kataa huu ubaguzi, ikataeni CCM kwa kishindo

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Sitaki kuwafundisha kufanya maamuzi lakini mnatakiwa mtoe adhabu kali kwa wanaowatisha kua msipowachagua watawanyima Maendeleo. Wakataeni hawa na waonyeshe ni kua mmechukizwa na kauli hizi.

Mnalipa kodi na kodi zinatakiwa ziwahudumie, mpeni ujumbe mzito anayesema hawezi kuwaletea maendeleo tarehe 28.10.2020 kwanza yeye asirudi ili tuone kama hayo maneno yatajirudia. Mgombea wa Urais wa CCM amekosea sana tunatafsiri kua hizi lugha ni za kibaguzi sana.Hatupaswi hata kumpa kura yeye ni bora apite asiyejua na lugha za kibaguzi.

=====

Akiwa Tunduma, Rais Magufuli amewaomba wananachi wamchague Silinde kuwa mbunge ili awatiririshie maji. Amewaambia kwa vipindi viwili wamekuwa wakichagua upinzani na hii ndio mara mwisho kuwaomba.

Alisema, "Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli."

Akiwa
 
Tumeccm,policcm,msajilcc wanachekelea na kumuunga mkono,ndio mana mashambulizi yote wameyaelekezea kwa Lisu,yaani makosa yote ya CCM wanayahamishia kwa Lisu,
Hatufai kabisa mbaguzi na mtishaji watu huyo
 
Mimi nipo tunduma yani silinde anatia huruma katika mikutano yake na watu wa Jana walifuata wasanii hasa diamond ndomana alipoimba diamond watu waliondoka kwa wingi kama bom limepigwa mkutanon ndomana mzee akapanic akaanza kufokea wananchi lakini kwa tunduma ni rahisi ngamia kupenya katka tundu LA sindano kuliko silinde kushinda ubunge labda bao LA mkono ndo litamsaidia
 
Wewe Endelea kuwadanganya wenzio waendelee kuishi Kama kuku wakati wewe Jimbo lako liko chini ya Mbunge wa CCM.

"Bila connection siwezi kuleta maendeleo" JPM
 
Sitaki kuwafundisha kufanya maamuzi lakini mnatakiwa mtoe adhabu kali kwa wanaowatisha kua msipowachagua watawanyima Maendeleo. Wakataeni hawa na waonyeshe ni kua mmechukizwa na kauli hizi.

Mnalipa kodi na kodi zinatakiwa ziwahudumie, mpeni ujumbe mzito anayesema hawezi kuwaletea maendeleo tarehe 28.10.2020 kwanza yeye asirudi ili tuone kama hayo maneno yatajirudia. Mgombea wa Urais wa CCM amekosea sana tunatafsiri kua hizi lugha ni za kibaguzi sana.Hatupaswi hata kumpa kura yeye ni bora apite asiyejua na lugha za kibaguzi.

Magufuli hafai kuwa kiongozi kwani hajui nilipanga kutopiga kura lakini kwa kauli za huyu mzee najiunga kwa Lissu kwa kulihali
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom