Mtanzania 'Gaidi' apandishwa Kizimbani Marekani (New York, Marekani) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania 'Gaidi' apandishwa Kizimbani Marekani (New York, Marekani)

Discussion in 'International Forum' started by LD, Nov 11, 2010.

 1. LD

  LD JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtanzania anayetuhumia kuhusika katika mashambulio ya mabomu dhidi ya balozi za Mareka mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya mwaka 1998, Ahmed Khalifan Ghailan,ametajwa juzi na mwendesha mashtaka wa mahakama ya Manhattan nchini Marekani kama muuaji wa halaiki.

  Ghalaini anatuhumiwa kuwa mwanachama wa kikundi cha Al-Qaeda katika eneo la afrika Mashariki kilichopanga na kufanya mashambulio hayo ya Julai 7 mwaka 1998.

  Ghalain ambaye alikuwa ameshikiliwa awali katika gereza la Guantanamo nchini Cuba, ndiye mshukiwa wa kwanza katika gereza hilo kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kiraia nchini Marekani.

  Jaji Lewis Kaplan anayesikiliza kesi hiyo amesema huenda kesi ya Ghailani ikaendelea hadi mwakani.

  Katika mchango wake wa mwisho katika kesi hiyo, mwendesha mashtaka wa mahakama Manhattan, Harry Cherttoff alisema, Ahmed Khalfan Ghailani ambaye alikuwa ameketi viti kadhaa upande wake kushoto, ni muuaji wa halaiki mwenye alama ya adamu ya mamia ya watu mikononi mwake.

  Ghalaini, Mtanzania anayetoka Zanzibar, ana umri wa miaka 36 na anahusishwa sana katika kupanga mlipuko ya mabomu katika balozi za Marekani katika mji wa Nairobi na Dar es Salaam mwaka 1998 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia mbili.

  Mshukiwa huyo alikana makosa hayo.
  Mahakama ya Manhattan ipo hatua chache kutoka katika jengo la mnara wa World Trade Centre (WTC) ambapo shambulio la kigaidi la september 11 mwaka 2001, lilitekelezwa na wanachama wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

  Wachunguzi wanalinganisha uhusiano uhuo kama hatua kubwa ya kutanzua mashambulizi ya kigaidi.

  Raisi Barack Obama wa Marekani alitoa amri ya kufungwa kwa mahakama ya kijeshi ya Guatanamo na washukiwa wanaoshikiliwa wafunguliwe mashtaka katika mahakama ya kiraia.

  Azimio hilo lililpingwa vikali na wachunguzi kadhaa wakidai kuwa uzito wa kesi hizo za ugaidi haufai kushughulikiwa katika mahakama za kiraia  Source: Nipashe Nov 10, 2010
  pg 15
   
Loading...