Mtanzania bila ya haya yachakachua kauli ya Prof. Lipumba............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania bila ya haya yachakachua kauli ya Prof. Lipumba.............

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Katika khali inayothibitisha ya kuwa fani ya uandishi wa khabari imeingiliwa na kuvamiwa na mamluki wenye nia mbaya ya kushusha hadhi ya vyombo hivyo machoni pa jamii, gazeti la Mtanzania la leo limedai Prof. Lipumba amesema Dr. Slaa hafai kuwa Raisi kwa sababu ni mpenda makundi jambo ambalo siyo la kweli hata chembe.

  Katika gazeti la Habari Leo la leo limeweka bayana Prof. Lipumba akimnadi Dr. Slaa kwenye kichwa cha khabari kisemacho "Lipumba asema kama siyo yeye basi ni Dr. Slaa"

  Haiwezekani kabisa Prof. Lipumba atoe kauli mbili ambazo zinazotofautiana kiasi hicho........Upande mmoja anamsigina Dr. Slaa na wakati huohuo anamnadi kuwa kwa wale ambao hawapo tayari kumchagua yeye Prof. Lipumba basi kura zao wazielekeze kwa Dr. Slaa ambaye mafanikio yake Bungeni ni ushahidi tosheleza wa kuwa ana nia na uwezo wa kulisaidia taifa hili kuhakikisha "Maisha bora kwa kila Mtanzania."

  Gazeti la Mtanzania inashangaza hata watafiti wa "SYNOVATE" hawakulimulika kwa kufanya kazi kiushabiki na wala siyo kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.........Wamiliki wa gazeti hili waone haya na wajirekebishe kwa sababu ni ukweli usiopingika ya kuwa nchi hii bila CCM yawezekana kabisa.................
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Haya magazeti ya bongo lazima kuhoji taaluma ya wahariri wake!
   
 3. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani haya magazeti yanatakiwa yakae kando, haraka sana tubaki na gazeti ambalo linaeleweka ni la chama fulani basi.Hakuna maana ya kuwa na magazeti yasiyoheshimu wasomaji, yaliyojaa propaganda wakati yakijitwisha zigo la walipa kodi kuwa ya serikali. Damn!!
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mkuu,
  mbona unajitaabisha sana, mbona unaangaika sana na hayo magazeti, nimeona article zako zaidi ya mbili unalalamika kuhusu hili gazeti, kwa nini unapoteza fedha yako kununua hilo gazeti, mbona kuna ombaomba wengi wanahitaji hizo hela unazonunulia huo uchafu,
  Mkuu usiangaike sana , USHINDI WA SLAA HAUWEZI KUBADILISHWA NA HAYO MAGAZETI YASIYOUZIKA, NADHANI MKO WACHACHE SANA MNAONUNUA HAYO MAGAZETI
   
Loading...