- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele.
Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.
Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.
Huu Muungano ni wa kishenzi sana.
Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria.
Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar.
Huu Muungano ni wa kishenzi sana.
- Tunachokijua
- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa Aprili 26, 1964 ikiwa ni Muungano wa Mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964 huko Zanzibar.
Sababu ya Muungano
Picha: Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile undugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususan baina ya vyama vya TANU na ASP.
Pamoja na kuwepo muungano lakini Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwenye kila jambo bali kwa baadhi ya mambo tu, hivyo kuwepo kwa mambo yahusuyo Muungano na ambayo hayahusu Muungano hivyo kila upande huyashughulikia bila kuhusisha Muungano.
Je, Mtu wa Tanzania bara anaruhusiwa kuendesha gari Zanzibar kwa kutumia leseni yake aliyopewa na TRA?
JamiiForums Imezungumza na Kamanda wa Polisi Ramadhani Ng'azi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, ambaye amekiri kuwa:
"Ni kweli mtu hawezi kutumia leseni yake aliyopewa na mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) kwasababu Mamlaka ya utoaji wa leseni sio jambo la kimuungano hivyo Mamlaka za utoaji wa Leseni kati ya Tanzania bara na Zanzibar zipo tofauti.
Tanzania bara Mamlaka inayotoa leseni ni TRA, baada ya kupata uthibitisho kutoka jeshi la Polisi kuwa mtu huyo amesomea udereva na amepitia mitihani ya polisi au utahini wa polisi na kupewa hati maalum ya kufaulu na kwamba mtu huyo anatakiwa kupatiwa daraja fulani la leseni.
Baada ya TRA kupokea taarifa ya uthibitisho kutoka Polisi hutoa leseni kulingana na maelekezo ya jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani.
Lakini Zanzibar wao wana mamlaka yao ya utoaji leseni ambayo ni tofauti na huku Bara na ndio maana wameweka utaratibu mtu akitoka huku kwenda kule ataomba kibali maalum kwa kuwa mamlaka ya utoaji leseni siyo jambo la kimuungano.
Hivyo mtu akienda Zanzibar ataomba kibali maalum na vivyo ivyo mtu akitoka Zanzibar kuja bara ataomba kibali maalum ili aweze kuendesha gari".
Pia, JamiiForums imezungumza na Abubakar Nassor Ali Mkuu wa Divisheni ya Upasishaji Madereva, Mamlaka ya usafiri na usalama barabarani Zanzibar, ambaye amesema kuwa:
"Kimsingi tunapozungumzia suala la usafirishaji, Tanzania tuna sheria 2 tofauti, zikiwa na lengo moja la udhibiti wa usalama barabarani. Huko bara mna sheria ile namba 30, ya mwaka 1973 (Road Traffic Act) lakini Zanzibar tuna sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ivyo ni sheria 2 tofauti ila lengo ni moja la shughuli za usafirishaji.Na hii kutokana na jambo hili kutokuwa la kimuunano.
Kwa maana Zanzibar tuna sheria yetu, sheria hiyo ndio inashughulika na mambo mbalimbali ya leseni, na inamtaka dereva yeyote awe na leseni.
Sheria yetu inatuambia mtu yoyote ambaye atatoka nje ya nchi, inamtaka mwenye leseni ya udereva mbali na ile iliyotolewa na Msimamizi Mkuu wa usafiri barabarani( Mkurugenzi wa mamlaka na usalama Barabarani) kwenda kufanya jaribio au kuangalia afya au kufanya mtihani ili kupima uwezo wake wa uendeshaji chombo cha moto akiwa ndani ya nchi.
Kwa maana hiyo mtu yoyote ambaye atakuwa na leseni ya nje ya nchi( nje ya nchi hapa ni pamoja na Tanzania bara) anatakiwa kukata permit, kwa hiyo kwetu mtu yoyote ambaye atakuwa anatokea bara maana yake anatokea nje ya nchi, na anatakiwa kukata Permit (kibali maalum) ambapo kwa sasa gharama yake ni 15,000 ambayo hudumu kwa miezi 3.
Na kwa yule ambaye atakuwa anataka kuendelea kukaa Zanzibar kwa muda mrefu zaidi au kuweka makazi ya kudumu basi ana uwezo wa kubadilisha leseni yake, yaani atakata leseni ya huku Zanzibar,( hatubatilishi leseni ila atabaki nayo ya bara na atapewa nyingine ya huku baada ya kufuata taratibu za kuchukua leseni huku)
Mtu atakayekiuka sheria hii na kuendesha bila leseni atakuwa ametenda kosa, Kosa la mtu kuendesha bila leseni hapa ni kwa wageni wote ( nchi nyingine pamoja na wa bara) adhabu yake ni faini ya dola zisizopungua 50 ambapo kwa sasa ni sawa 116,500".
JamiiForums baada ya kusoma mambo yahusuyo muungano na kujiridhisha kuwa suala la usafirshaji si la kimuungano na kuzungumza na mamlaka za usafirishaji pande zote 2 za muungano ambao wamekiri mtu anayetoka upande 1 kwenda mwingine anatakiwa kukata kibali maalum ivyo imejiridhisha kuwa ni kweli Mtu wa Tanzania bara haruhusiwi kuendesha gari Zanzibar mpaka akate kibali maalum(permit)