Mtanzania Bara anaruhusiwa kuingiza gari Zanzibar?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Ninapiga mahesabu ya kuagiza gari ya biashara lakini naona kodi za Tanzania Bara hazishikiki.
Kwa hiyo nimepata wazo niliingizie gari hilo kupitia Zanzibar and then lifanye biashara kule mpaka nitakapopata pesa ya kulikombolea na kulileta huku bara.
Je Mtanzania wa kutoka huku Bara anayo nafasi ya kufanya hivyo?
Naombeni kujuzwa...
 
Mtanzania bara ndio nani, mm kwa najua kuna Tanganyika, nandio maana mna sherehekea uhuru wa Tanganyika lakini baadhi yenu mnaukana Utanganyika na kujiita Tanzania bara acheni hizo hakuna Tanzania bara
 
Kuna Tanzania bara na Tanzania visiwani... Wewe wa wapi wewe?
 
Ninapiga mahesabu ya kuagiza gari ya biashara lakini naona kodi za Tanzania Bara hazishikiki.
Kwa hiyo nimepata wazo niliingizie gari hilo kupitia Zanzibar and then lifanye biashara kule mpaka nitakapopata pesa ya kulikombolea na kulileta huku bara.
Je Mtanzania wa kutoka huku Bara anayo nafasi ya kufanya hivyo?
Naombeni kujuzwa...
Cha Zanzibar ni cha mzanzibar lakini cha Tanganyika ni cha wote
 
Mtanzania bara ndio nani, mm kwa najua kuna Tanganyika, nandio maana mna sherehekea uhuru wa Tanganyika lakini baadhi yenu mnaukana Utanganyika na kujiita Tanzania bara acheni hizo hakuna Tanzania bara
Kombo why unasema ukweli ambao wengi hawataki kusikia? Hahahahhaa
 
Kuna njia ya barabara kupitia mipakani,njia ya viwanja vya ndege,njia ya reli na kwa njia ya majini kupitia bandari.ukiangalia Tanzania kodi kutokana na bidhaa toja nje zipo tatu TRA kwenye website yao wametaja ushuru wa forodha,ushuru wa bidhaa na kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT.hii ni kwa Tanzania nzima.hivo hata ukipitishia Zanzibar,Namanga kodi hizo zitakuwa sawa.Angalia ile calculator yao ya kodi za magari unapoingiza.
 
Nafikiri kauliza swali ambalo limeeleweka lakini sijui kwanini watu badala ya kujibu swali wameingia kwenye siasa, afu serikali ikifanya kila kitu siasa muanza kulalamika.

Mkuu unaweza kuingiza gari lako zanzibar na ukalitumia utakavyo kama kwa kazi au kwa matumizi binafsi tu..... na ushuru zanzibar huwa nafuu sana kuliko bara. Ila ukitaka kulipeleka bara kutoka zanzibar utalipia difference ilobakia, mfano ushuru ni milioni 5, zanzibar waweza lipa 3m, ukitaka kulipeka dar unalipa 2 zilizobaki
 
Back
Top Bottom