Mtanzania Ashambuliwa na Mwanamke wa Kichina, Yasemekana kwa Kosa la Kudhalilisha Wanawake

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Inasemekana Mtanzania huyo amehukumiwa kifungo cha siku saba, na kuamriwa kuondoka China mara moja kwa kosa la kudhalilisha wanawake.

Kulingana na ripoti: Mnamo Septemba 12, 2022, karibu na Mtaa wa Jiaoda, Wilaya ya Beilin, Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, mwanamume mgeni alishukiwa kudhalilisha wanawake mitaani, lakini hakutarajia kushambuliwa na mwanamke huyo papo hapo. Inaweza kuonekana kwenye video hiyo iliyoenea mtandaoni.



Blog za huko China ziliripoti tukio hilo majira ya saa 9 ambapo walimtaja mtu huyo kama “Mwanaume mmoja”, huenda ni kwasababu hawakuwa wamepata taarifa za uraia wake. Pia, iliripotiwa kwamba alichukuliwa na polisi kutoka eneo hilo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.

Hata hivyo, baadaye majira ya 10:09 Alasiri, akaunti moja ambayo ipo verified (kwa rangi ya Bluu) katika mtandao maarufu wa Weibo nchini humo ilichapisha taarifa ya Polisi wa Xi’an ikimtaja bwana huyo kama Mtanzania mwenye umri wa miaka 25 aitwaye Lucas. Verification icon ya rangi ya Bluu kwenye mtandao wa Weibo unatumiwa na Makampuni, Asasi za Kiraia pamoja na Taasisi za Serikali. Watu maarufu na Vyombo vya Habari wanatumia verification icons za rangi tofauti kama vile rangi ya Machungwa na Nyekundu.

Taarifa hiyo ya Polisi inasema:

Mnamo Septemba 12, 2022, kituo cha polisi cha Xingqing Road kilipokea taarifa ikisema kwamba " Raia wa kigeni alimdhalilisha mwanamke mbele ya umma", polisi waliwatumwa mara moja na kuanzisha uchunguzi .

Baada ya uchunguzi, mkosaji Lucas (mwanaume, umri wa miaka 25, uraia wa Tanzania) aliwadhalilisha wengine na alizuiwa hapo hapo. Kwa mujibu wa Kifungu cha 44 na aya ya 2 ya Kifungu cha 10 cha "Sheria ya Adhabu ya Utawala wa Usalama wa Umma ya Jamhuri ya Watu wa China", ofisi yetu ilimshikilia Lucas kwa siku saba na kuweka kikomo cha muda wa kuondoka nchini.

Police.jpg


PIA, SOMA:
Ubalozi wa Tanzania Nchini China Watoa Tamko kuhusu Kijana wa Kitanzania Kushambuliwa na Mwanamke wa Kichina
 
Wabongo wamezoea kudharirisha wanawake hata humu nenda posts za kike za kutafuta wachumba uone. Tofauti na huku matakoni, uko usoni huwa wanashikisha adabu kenge yeyote anayedharirisha jinsia ya mtu, maumbile au ulemavu. Nenda kwenye nyuzi za Haji Manala muone wabongo walivyo wapuuzi.
 
Back
Top Bottom