Mtanzania apata mabilioni, Auza mfumo wa kununua Gesi kadri unavyotumia

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Mtanzania Andron Mendes ameuza mfumo wa mita ya kulipia ya kulipia gesi ya kupikia kadri unavyotumia (PAYG) kwa Kampuni ya Circle gas ya Uingereza kwa Sh.57.6 bilioni ili isambazwe kwa nchi za Afrika.

"Hakuna sababu ya kushikilia Teknolojia ambayo inapunguza matumizi ya Mkaa kwa sababu tu umeigundua. Nimeamua kuiuza Teknolojia hiyo kwa watu wenye fedha ili waisambaze Afrika" alisema Mendes wakati wa hafla ya mauziano ya Teknolojia hiyo iliyofanyika jijini Nairibi nchini Kenya.

WhatsApp Image 2020-01-17 at 10.06.20.jpeg


=====

Mtanzania kwa majina Andron Mendes hatimaye ameuza mfumo wa mita ya kulipia gesi ya kupikia kadri unavyotumia kwa kampuni ya UK , Circle gas kwa shilingi bilioni 57.6 ili usambazwe kwa nchi nyingine za afrika.

Sababu ya yeye kuuza mfumo huo ni kupata changamoto ya mtaji mkubwa wa kuendesha mradi huo kuwafikia watu wengi. Alisema kulikua hakuna sababu ya kuishikilia teknolijia ambayo inapunguza matumizi ya mkaa sababu tu umeigundua ndio mana ameiuza kwa wenye fedha zao.

Mtanzania na kijana mwenzetu ameasa vijana kutokata tamaa na zaidi kujiamini ya kua wanaweza kuleta mabadiliko ya kimaisha kwa wao binafsi na kwa jamii pia.

Kijana huyo atakua mmiliki wa hisa kwa asilimia 15, na ataongeza wafanyakazi wapya na kuhamia kwenye kampuni mpya.

Safari yake aliianza mwaka 2012, na kuendelea kuikuza hio teknolojia hio kwa miaka saba. Teknolojia hio iitwayo KOPA GAS itashirikiana na kampuni hio ya uingereza pamoja na kampuni ya safari com ya Kenya ili kuungamisha nguvu na kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuleta upatikanaji wa gesi ya bei nafuu kwa mamilioni ya watu katika bara la afrika.

Mradi huo tangu 2016 ulivyoanza hadi sasa umeshaunganisha wakazi wa Dar es Salaam zaidi ya 1430, na watafikia watu laki mbili mwaka 2021 lakini kutokana na ufinyu wa mtaji, aliamua kuiza teknolojia hio.

Hongera kwa kijana mtanzania.

"Get rich or die trying"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kutakuwa na mabomba ya gesi. Mtz mwingine avumbue mtungi ambao unaweza kuangalia salio la gesi ili tuondokane na adha ya gesi kukatika gafla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kukatika gesi siyo shuguli ya kwako tena! Mita inayo mfumo wa mawasiliona amboa unataarifu kampuni gesi inaelekea kuisha,kampuni wanaleta mtungi iliojaa gesi. Unanua gesi kwa mfumo uleule wa umeme wa luku. Mfano unalipia gesi Tsh 5000. Mita inakata matumizi yako yakizidi gesi uliyolipia.
 
Mtanzania, anauzia UK mfumo wa kuja kutusambazia waafrika gesi, tena wanakabidhiana pesa Nairobi, mimi naona ni kama aibu kwa nchi yetu.
Inawezekana alipoupeleka kwenye wizara zetu wakamchanganya na zile mbwembwe zao za mara lete vibari vya tume ya sayansi, vya brela, n.k
Na labda wataalam walibaini kuzibiwa mirija, labda walitoa ofa kiduchu. Ngoja Sasa iuzwe nje halafu iletwe Tz ilikozaliwa
 
Kwahiyo kutakuwa na mabomba ya gesi. Mtz mwingine avumbue mtungi ambao unaweza kuangalia salio la gesi ili tuondokane na adha ya gesi kukatika gafla.

Sent using Jamii Forums mobile app
siyo mambomba ya gesi ndugu. Huyu alichogundua ni Mita, anakuletea Mtungi wa kilo 6, 15 au 30 nyumbani kwako ila huwezi kuutumia mpaka ulipie, unaweza kununua gesi ya 2000 katika mtungi huo ikiisha inakata hadi ununue tena, ni kama Luku.
 
Kwahiyo kutakuwa na mabomba ya gesi. Mtz mwingine avumbue mtungi ambao unaweza kuangalia salio la gesi ili tuondokane na adha ya gesi kukatika gafla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hii itatusaidia sana,maana ile mambo ya kurudi nyumbani njaa inakuuma,umeshakatakata viungo vyako tayari upandishe jikoni,ile unawasha unakuta hola,kwakweli hicho kifaa ni cha muhimu mkuu...
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom