Mtanzania apata mabilioni, Auza mfumo wa kununua Gesi kadri unavyotumia

Mtanzania kwa majina Andron Mendes hatimaye ameuza mfumo wa mita ya kulipia gesi ya kupikia kadri unavyotumia kwa kampuni ya UK , Circle gas kwa shilingi bilioni 57.6 ili usambazwe kwa nchi nyingine za afrika.

Sababu ya yeye kuuza mfumo huo ni kupata changamoto ya mtaji mkubwa wa kuendesha mradi huo kuwafikia watu wengi. Alisema kulikua hakuna sababu ya kuishikilia teknolijia ambayo inapunguza matumizi ya mkaa sababu tu umeigundua ndio mana ameiuza kwa wenye fedha zao.

Mtanzania na kijana mwenzetu ameasa vijana kutokata tamaa na zaidi kujiamini ya kua wanaweza kuleta mabadiliko ya kimaisha kwa wao binafsi na kwa jamii pia.

Kijana huyo atakua mmiliki wa hisa kwa asilimia 15, na ataongeza wafanyakazi wapya na kuhamia kwenye kampuni mpya.

Safari yake aliianza mwaka 2012, na kuendelea kuikuza hio teknolojia hio kwa miaka saba. Teknolojia hio iitwayo KOPA GAS itashirikiana na kampuni hio ya uingereza pamoja na kampuni ya safari com ya Kenya ili kuungamisha nguvu na kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuleta upatikanaji wa gesi ya bei nafuu kwa mamilioni ya watu katika bara la afrika.

Mradi huo tangu 2016 ulivyoanza hadi sasa umeshaunganisha wakazi wa Dar es Salaam zaidi ya 1430, na watafikia watu laki mbili mwaka 2021 lakini kutokana na ufinyu wa mtaji, aliamua kuiza teknolojia hio.

Hongera kwa kijana mtanzania.

"Get rich or die trying"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera humu mimi nilishatoa wazo kuhusu mafundi kujituma kugundua vitu. Nikatoa mfano kuwa Mtu ajitahidi kugundua mita za majiko ya kupikia ya gesi ili zifungwe kwenye mitungi mtu ajue gesi Kama imebakia kiasi gani awahi kununua ingine.

Kuna watu waliniponda ponda humu Sasa huyo kagundua bilionea tayari.

Hilo la gauge za majiko ya gesi zinahitajika watanzania mafundi ingieni gereji mtengeneze
 
Kukatika gesi siyo shuguli ya kwako tena! Mita inayo mfumo wa mawasiliona amboa unataarifu kampuni gesi inaelekea kuisha,kampuni wanaleta mtungi iliojaa gesi. Unanua gesi kwa mfumo uleule wa umeme wa luku. Mfano unalipia gesi Tsh 5000. Mita inakata matumizi yako yakizidi gesi uliyolipia.
Huyu utajiri mkubwa wa kutisha unamsubiri gesi za bomba zimeanza kusambazwa majumbani na viwandani huo mradi utamtoa haswa

Kaweza hiyo mwingine atengeneze ya maji Kama ya gedi imewezekana na ya maji inawezekana
 
Inawezekana alipoupeleka kwenye wizara zetu wakamchanganya na zile mbwembwe zao za mara lete vibari vya tume ya sayansi, vya brela, n.k
Na labda wataalam walibaini kuzibiwa mirija, labda walitoa ofa kiduchu. Ngoja Sasa iuzwe nje halafu iletwe Tz ilikozaliwa
Serikali hainunui mifumo yaani software sababu haiko kwenye hiyo biashara ilikuwa haki yake kuuza popote Duniani anapoona pana faida na inakubalika

Matajiri wa Tanzania Hakuna venture capitalist wanunua mawazo na wapenda kuingia ubia na wagunduzi

Nchi za wenzetu Wako kibao waweza wauzia wazo au ugunduzi wako au mkaingia ubia
 
Mtanzania, anauzia UK mfumo wa kuja kutusambazia waafrika gesi, tena wanakabidhiana pesa Nairobi, mimi naona ni kama aibu kwa nchi yetu.
Tz hamna kusapotiana utajitokeza tu at once utashangiliwa but no further actions ukijikuta mjuaji zaidi unapotezwa kabisa (ata kukatishwa uhai)
 
Back
Top Bottom