Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,631
- 4,225
Kwa mujibu wa Chinga Networks hapa Detroit tumepata ujumbe huu:
"Wanajumuiya,
Mmoja wetu amepata ajali mbaya ya gari na yuko kwenye coma
University Of Michigan Hospital.Habari zaidi tutaleta kadri tunapopata.
Sala zitasaidia m'da huu"
Kijana wa Kitanzania Bw. Ndalima Nzaro yuko mahututi kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan Ann Arbor, nje kidogo ya Jiji la Detroit nchini Marekani baada ya ajali iliyosababisha na kijana wa miaka 15 aliyeiba gari kugonga gari la Ndalima lililokuwa limesimama kwenye taa za kuongozea magari likisubiri rangi ya kijani.
Kijana huyo aliyegonga gari alikuwa anafukuzwa na Polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mji mdogo wa Westland kijana huyo aliyeiba gari na ambaye hakuna leseni ya kuendesha gari alikuwa anaendesha gari kwa kasi zaidi ya maili 100 kwa saa na aliyagonga magari ubavuni yaliyokuwa yamesimama hapo kwenye taa za kuongezea magari kwenye barabara ya Merriman.
"Wale madereva waliokuwa wanasubiri rangi ya kijani kuwaruhusu hawakuwa na jinsi yeyote ya kukwepa ajali hiyo" alisema Chifu Jim Ridener. Bw. Ndalima aliyekuwa anaendesha gari ndogo aina ya Honda Accord alitibiwa kwa dharura kwenye hospitali ya Garden City lakini kutokana na majeraha yake aliitiwa Helikopta ya Hospitali ambayo ilimchukua na kumkimbiza kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor.
Hospitali hiyo ni mojawapo ya hospitali zenye uzoefu mkubwa katika kuhudumia dharura za ajali katika eneo hili la Michigan.
Mtoto huyo wa miaka 15 alikuwa anaendesha gari aina ya Mercedes Benz S55MG ambalo ni la rafiki ya kiume wa mama yake. Kutokana na kijana huyo kuwa chini ya umri jina lake halitajwi kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo kijana huyo yuko mikononi mwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea na mashtaka dhidi yake yatategemea hali ya Ndalima inaendeleaje.
Habari ambazo tunazipata sasa hivi, hali ya mgonjwa siyo nzuri.
Tutawaletea habari zaidi kwa kadiri tunavyozipata.