Mtanzania anayeishi kwenye handaki jirani na Mlimani City

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,738
155,422
TAZAMA PICHA ZA MWANAUME ANAEISHI KWENYE HANDAKI MIAKA MINNE,LIPO KARIBU NA MLIMANI CITY



Makongoro Oging'
DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni kweli.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR5.JPG
Chacha Makenge (36) akiwa amepozi ndani ya chumba chake 'handaki'.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza samani zote.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR3.JPG
...Akitoka katika handaki lake.

"Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR6.JPG
...Akiwa nje ya handaki lake.

"Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR2.JPG
Chacha akifunika mlango wa handaki lake.

"Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.
"Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea, aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR8.JPG
...Akizidi kufunika handaki lake.

"Siku iliyofuata majirani walikuja tena kituoni wakaniwekea dhamana. Nilipofika kwangu nilikuta majivu tu, iliniuma sana, nililia lakini sikupata ufumbuzi. Kwa vile nilikuwa sina pa kwenda ilibidi niwe nalala palepale nilipochomewa nyumba nikisaidiwa chakula na majirani.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR1.JPG
...Akimalizia kufunika nyumba yake.

"Siku iliyofuata, saa nne usiku nilivamiwa na watu wanne, wakiwa na mapanga na marungu, nilipambana nao mpaka wakaondoka. Kesho yake nilikwenda kwa mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, Jumanne Malima kumweleza yaliyonipata, alisikitika, akaniandikia barua kwenda Polisi Stakishari.

AISHIKWENYEHANDAKIDAR7.JPG
Chacha katika pozi nje ya handaki lake.

"Nilipofika kituoni sikusikilizwa, badala yake walinikamata tena na kuniweka ndani wakidai kwamba nimefunguliwa kesi ya kumjeruhi mtu kwa panga. Hawakukubali niwekewe dhamana.
"Julai 31, 2009 nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ukonga na baadaye nilipelekwa Mahabusu ya Gereza la Keko, nikawa napelekwa mahakamani hadi Septemba mwaka huo ambako nilihukumiwa kwenda jela miezi 9.
"Nilitumikia maisha ya jela hadi Desemba 10, 2009 nikatolewa kwa msamaha wa Rais Jakaya Kikwete. Nilikwenda kuishi kwa ndugu zangu huku wakifuatilia sababu ya kufanyiwa vitendo hivyo bila mafanikio.
"Maisha ya kwa ndugu hayakunifurahisha kwani hata wao walikuwa na majukumu mengi, niliamua kuendelea na kazi zangu za sanaa pia utunzaji wa mazingira na bustani kwa watu wakawa wananilipa fedha.
"Ndipo nilipoamua kutafuta sehemu iliyotulia ili niweze kuishi, nikapata hapa, ni jirani na Mlimani City. Nilichimba handaki kubwa kama unavyoliona, kwa chini kuna kitanda ninacholalia.
"Kwa hakika hapa sipati shida, wala kelele. Kwanza ni tulivu sana, nimefikia hatua ya kuishi kama mnyama kutokana na mateso na bugudha nilizopata, wengi hawajui nilipo, nipo katika pori hili kwa miaka minne sasa,"alisema Makenge.


CHANZO GPL

 
Ana akili sana kaachana na kelelrle za kodi za nyumba. Heri yake. Sasa demu anaingiaje huko kwenye handaki
 
Huyu labda kama ni@bujibuji mwenyewe anaandaa bongo movie kijana mtanashati anaoga wapi anafua wapi achilia mengine. Halafu miaka minne
Kajipange tena mi hunidanganyi
 
Jamaa usiku anaangalia sinema mlimani city afu anarudi kulala taratibu kwenye handaki lake...!! Bonge la ubunifu.
 
mhm! maisha popote, ilimradi usivunje sheria aza nchi yako
ila inasikitisha sana jamani wana jf tumsaidiaje mtu huyu
kwa wale wenye moyo wa huruma naupendo semeni hapa?
asante nkamu Bujibuji kwa uzi huu tunaweza msaidia ati?
 
Last edited by a moderator:
Luk'n smart...miakaka minne ajajipanga tuu ...mvua jee? Unaishi na nani? Na hayo mazingira CIO ya makazi we we umepata wapi kibali chakuish hpo ? Hao wasimamizi wa hlo pori uliwatuliza vp? nnamaswali mengi lkn CIO polis ni kwa sababu stori yko 80% s kwel
 
Ana akili sana kaachana na kelelrle za kodi za nyumba. Heri yake. Sasa demu anaingiaje huko kwenye handaki

Haha yani we umefikiri demu tu mengine yoote hujaona! You better than that
 
Huyu ni mchavuzi wa mazingira! anajisaidia wapi wakati hilo libangaloo lake halioneshi kuwa na choo wala bafu!
 
Back
Top Bottom