Uchaguzi 2020 Mtanzania amka! Hii ni sehemu ndogo ya elimu kwa Mpiga Kura

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Huduma muhimu kama elimu, maji, umeme, miundombinu majengo ya umma kama zahanati, hospitali, barabara ni haki zako za msingi wala si hisani ya kiongozi. Una haki kudai, kuhoji kadiri ya pato la taifa na mahusiano michango mataifa rafiki na jumuiya za kimataifa.

Kiongozi asiwatishe kwa ahadi maji, umeme, barabara, elimu nk.

Tuwapime viongozi wetu kwa sera rafiki, mazingira bora ajira, sera mahuasiano nje, uwekezaji wa ndani na nje, utawala bora, utu, haki na ustawi wa jamii.

Tambua kila Mtanzania alie hai ni mlipa kodi kwa viwango tofauti kadiri ya mapato na matumizi yake.

Unapopanda daladala ama boda na kulipa nauli tayari umelipa sehemu ya kodi kuwezesha serikali kutimiza wajibu wake.

Ukinywa kinywaji chochote cha dukani soda, juisi, pombe kali hata ya 500 (wanapima robo) tayari umelipa kodi pia.

Tumpongeze John Pombe Magufuli kwa maamuzi kujenga Bwawa la Nyerere ile ni sera na maamuzi bora, yatapunguza garama /bill umeme.
 
Nawashauri CDM na wengine watoe elimu hii kwa wapiga kura.Huduma muhimu si hisani ya watawala bali ni wajibu kadiri ya pato la taifa.
 
Asante sana kwa hili na hasa Mgombea wa CCM anapotosha sana kwa kuwaaminisha watu kwamba wasipompa kura hawatapata maendeleo.
 
Back
Top Bottom