Mtanzania, Alphonce Simbu ashika nafasi ya tatu Marathon IAAF LONDON

hivi tofauti kat ya marathon na Olympic ni ipi? maana naona vtu vngi vnafanana
 
Jamaa ametimua mbio yaani nimefurahi sana kuona mtanzania kajaribu namna hii....Simbu amemweza Kipketer wa Kenya ambaye amemaliza ktk nafasi ya nne...Tanzania is now in the medal table...infact most EA nations except Somalia, Burundi and Rwanda are on the medal table...congrats to the man Simbu!!! a true hero
CqZSHCWWAAAdGTO.jpg
At last nashuhudia tukishinda medali medani ya kimataifa zaidi.
Hongera sana kijana wetu.
 
hivi tofauti kat ya marathon na Olympic ni ipi? maana naona vtu vngi vnafanana

Marathon ni mbio za km 42 (nusu marathon km 21). Olimpiki ni michuano inayofanyika kila baada ya miaka 4, mwaka 2016 ilifanyika Rio de Janeiro, Brazil na inayofuata itakuwa mwaka 2020 Tokyo, Japan. Ndani ya michuano mingi ya riadha, iwe mbio za dunia, olimpiki ama mashindano mengine huwa kuna mbio za umbali tofauti tofauti ikiwamo marathon.
 
Duuhhh..., aisee hongera sana, huyu akirudi JPM amnunulie gari nzuri, apewe nyumba nzuri hata mbezi au kimara na aolewe mke mzuri kabisa kama hana, hii itasaidia kutengeneza morale boost kwa upcoming talents, hivi ndivyo Kenya wanavyo wa-motivate athletes wao. DO THIS PLEASE. Hizo pesa zitarudi kupitia utalii maana ameitangaza Tanzania dunia nzima
upo sawa mkuu. Huyu jamaa ndio ameiwakilisha nchi vyema anatakiwa apewe ufadhili WA nguvu awe na maisha ya ki professional. Utakuta mtu anakatika viuno au anaigiza upuuzi Ana utajiri mwingi wakati international athlete ambae Ni maarufu duniani Ana maisha ya kawaida
vodacom,airtel,tigo leteni ela zenu kwa huyu simbu
 
..umesahau pia kuwa hata kwa maendeleo ni Arusha Na Moshi ziko juu...Na pia elimu....shule bora ziko Arusha Na Kili....pia watu vichwa Na wenye mafanikio Na wasomi wengi wanatoka Arusha Na Kilimanjaro... Ndio maana hata JPM anaumia....kwa mafanikio ya mikoa hii....wanasahau kuwa watu wa huku ni wenye juhudi sana Na wenye kupenda maendeleo...
Kwa ubaguzi tu mmebarikiwa
 
Safi Simbu.Serikali imulike huu mchezo,hasa upande wa viongozi wake ndio wanauangusha sana mchezo huo bongo.
Hawa akina Simbu wamehangaika wenyewe kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hapo.
 
Simbu ni mtu wa kupigiwa mfano. Japo vyama vya michezo na serikali zinamwangusha katika support. Zimamoto zinatuppnza
 
Hongera kwake Simbu na Tz kwa jumla. Wakenya tumezoea kushindana na hawa wazungu. Itakuwa freshi wanaE.A tukitoana kijasho sisi kwa sisi! Lakini wakenya hamtatuweza bana, tz bado sana kwenye riadha! Itabidi mapenzi yenu na chipsi mayai myatupilie kando kwanza! Hehe!
 
Hongera kwake Simbu na Tz kwa jumla. Wakenya tumezoea kushindana na hawa wazungu. Itakuwa freshi wanaE.A tukitoana kijasho sisi kwa sisi! Lakini wakenya hamtatuweza bana, tz bado sana kwenye riadha! Itabidi mapenzi yenu na chipsi mayai myatupilie kando kwanza! Hehe!

Wakalenjin ndio wanaojua kukimbia, nyie watu wengine wasindikizaji tu.
 
Anaitwa Magdalena, sijui alimaliza wa ngapi, mwanzoni alikuwa kundi moja na wakenya.

Asante kwa jina hilo. Ngoja nikam-google.
Ila mbona hilo jina ni la kibongo wakati yeye alikuwa mzungu?
Anaitwa Magdalena Shauri, sijui alimaliza wa ngapi, mwanzoni alikuwa kundi moja na wakenya.

Okay. Ila mimi nilikuwa namzungumzia yule Uliyemtaja hapo juu. Nadhani ni yule Mreno aliyeanza kwa kuongoza.
 
Safi Simbu.Serikali imulike huu mchezo,hasa upande wa viongozi wake ndio wanauangusha sana mchezo huo bongo.
Hawa akina Simbu wamehangaika wenyewe kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hapo.
Mafanikio ya Simbu ninavyoona hayajaja tu from nowhere. Multichoice walim spot mwaka jana na kuanza kumdhamini chini ya uongozi huu mpya wa MD mTanzania wa multichoice.

Kama utaweza kumfuatilia jamaa tangu aingie udhamini na multichoice amefanya vizuri mashindano karibu yote anayoshiriki. Naona kikubwa kwa hata wakimbiaji wengine ni jinsi ya kuwawezesha ili waweze kujiandaa vema kwa mashindano na si kusubiria "zimamoto" na pia kuwr na udhamini unakuwa wa kipindi kirefu(sio kipindi cha mashindano tu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya ndugu yetu Alphonce Felix Simbu kututoa kimasomaso kwa kishika nafasi ya tatu katika michuano ya IAAF marathon huko London, nimekuwa na maswali mengi sana.
Kipi kafanya cha tofauti mpaka kufikia mafanikio haya, Je ni mwalimu wake? Ni nidhamu yake? Au kawekeza pesa ya kutosha katika training yake? Wapi anafanya mazoezi? n.k.
Kama unafahamu historia yake tupia hapa.
 
Back
Top Bottom