Mtanzania aliyetengeneza Chopa aalikwa South Africa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kijana wa Kitanzania Adam Kinyekile aliyefanya juhudi za kutengeneza ndege aina ya Helkopta na baadae kupigwa marufuku na TCAA amepata mualiko kutoka kiwanda kimoja cha kutengeneza Ndege hizo huko Afrika Kusini.

Chini ni taarifa ya marufuku ya TCAA
================

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

MAELEKEZO JUU YA MIRADI YA UBUNIFU WA KUTENGENEZA NDEGE

1. UTANGULIZI

1.1. Taarifa hii kwa umma imetolewa kwa mujibu wa madaraka ya kisheria aliyonayo Mkurugenzi Mkuu kupitia sheria ya Usafiri wa Anga nchini, sheria namba 80 (iliyofanyiwa maboresho mwaka 2006) pamoja na kanuni zake mbalimbali zilizopo zikiwa na lengo la kuhakikisha hususan usalama katika usafiri wa anga pamoja na kulinda maslahi ya wananchi na mali zao kwa ujumla kutokana na shughuli za usafiri wa anga.

1.2. Taarifa hii kwa umma imetolewa ili kuufahamisha umma kwa ujumla juu ya tahadhari za ki-usalama za kuzingatiwa pindi unapofanya shughuli za uendeshaji wa usafiri wa anga nchini Tanzania. Taarifa hii kwa umma imetolewa kufuatia Mamlaka kubaini kwamba hivi karibuni kumeibuka wimbi la watu binafsi pamoja na taasisi zinazodai kuwa na uwezo wa kutengeneza ndege(Helikopta) na wapo katika hatua ya kuzifanyia majaribio ya kuzirusha angani pasipo kuzingatia kanuni za usafiri wa anga na taratibu zake za ki- usalama zilizopo.

1.3. Taasisi ama mtu yeyote anayetarajia kutengeneza ndege au vifaa vyake anakumbushwa kuhakikisha anafanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za usafiri wa anga ikiwemo pamoja na kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kabla ya kuanza mradi wake.

1.4. Lengo ni kuhakikisha usalama kwa wananchi na mali zao, kuzingatia viwango vya ubunifu husika, aina na ubora wa malighafi zinazotumika kufanya ubunifu, vipuri vya ubunifu husika, jinsi ya uundwaji wa chombo husika unavyofanyika hasa kuangalia kama vifaa vinavyotumika kutengenezea ndege ni vile vinavyokubaliwa na kanuni za Mamlaka ya usafiri wa anga nchini pamoja na zile za kimataifa .

2. KUTAMBULIWA KWA NDEGE

2.1. Kanuni namba 5 ya usafiri wa anga (inayohusu ubora wa ndege) kanuni ya mwaka 2011 imeweka bayana kwamba:

2.1.1 Mamlaka italitambua ombi ama wazo la kutaka kutengeneza ndege, vifaa vya ndege endapo Mamlaka itajiridhisha kwamba,

(a) Kazi itakayofanywa ni ile inayoendana na miundo inayokubaliwa katika utengenezaji wa ndege;

(b) Uwepo wa utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na uwepo wa usimamizi wa mhandisi mwenye cheti cha kutengeneza aina ya ndege husika atakayehakikisha anasimamia hatua zote za ubunifu na ufundi wa ndege husika ; na

(c) Taratibu za maandalizi yake zinakubaliwa katika kutengeneza ndege husika.

3. UBUNIFU NA MATENGENEZO YA NDEGE

3.1 Kanuni za kimataifa kama zilivyoainishwa na ICAO kwenye Annex namba 8 (inayohusu ubora wa ndege) zimeanisha kwamba “Maelezo ya kubuni na kuunda ndege lazima yaweze kuthibitibisha bila ya shaka kwamba vipuri vyote vya helikopta husika vitafanya kazi kwa uhakika na kwa usalama katika mazingira mbalimbali iwapo angani. Na lazima iwe imetokana na tafiti za kina zilizofanywa na kuthibishwa kutoa majibu ya kuridhisha au iwe imethibitishwa kwa majaribio maalum au kwa kupitia tafiti maalum za watafiti waliobobea katika masuala ya anga au iwe imepitia hatua zote hizo kwa ujumla.

3.2 Tanzania kwa sasa haina wataalamu waliobobea katika kudhibiti shughuli za utengenezaji ndege, wala kuwa na taasisi ama viwanda vinavyotengeneza ndege wala viwanda vya vipuri vya ndege ili kuweza kuthibisha ubora na ufanisi wa vifaa hivyo.

Hata hivyo Mamlaka inaweza kuandaa utaratibu kwa kupitia washirika wake na Mamlaka zingine za usafiri wa anga duniani (mfano Mamlaka ya usalama wa Anga ya Ulaya (EASA) au Idara ya usalama wa Anga ya Marekani (FAA) ili kuweza kusaidia kuhakikisha kwamba kabla bidhaa husika haijaanza kutumiwa na umma, hatua zote za ubunifu, malighafi zake ziwe zimefanyiwa majaribio stahiki ili kuweza kuhakikisha kwamba bidhaa husika inaweza kuhimili mazingira magumu ya hewa iwapo angani bila kuleta athari. Hatua zote ikihusisha injini, mota na mabawa ya ndege husika nk yawe yamekidhi na kufaulu majaribio mbali mbali ya kuhimili mazingira magumu ya hewa angani.

4. HITIMISHO

4.1 Ili kuendelea kulinda usalama kwa umma, taasisi ama mtu binafsi anapaswa kuhakikisha anazingatia sheria za usafiri wa anga pamoja na kanuni zake. Kuanzia sasa si ruhusa kwa yeyote kujihusisha na ubunifu wa ndege, kutengeneza ndege ama vifaa vya ndege bila kuwasiliana na Mamlaka ili kuweza kupatiwa maelekezo na hatua stahiki zinazopaswa kupitia na kuzingatia ili hicho kinachondaliwa kiwe kimezingatia taratibu za kimataifa za utengenezaji ndege.

4.2 Mamlaka inaunga mkono ubunifu wa aina hii katika masuala ya usafiri wa Anga, ila inapaswa kufanywa kwa mujibu wa taratibu maalum ili kuhakikisha usalama. Sambamba na hili wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga wa Mamlaka watawatembelea wabunifu husika waliojitokeza ili kuweza kuwapatia ushauri na maelekezo zaidi.

4.3 Kwa kutolewa kwa taarifa hii, tunatoa wito kwa watu binafsi ama taasisi kusitisha shughuli zote za utengenezaji wa ndege na wanaombwa kuwasiliana na Mamlaka ya usafiri wa anga kwa maelekezo na miongozo zaidi kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na

Hamza S. Johari

MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA
 
Si tumeambiwa hajui kusoma wala kuandika?

Sasa kwenye kampuni inayotengeneza ndege atakuwa anawasilishaje idea zake.

THE KICK.
 
Wapi pameonyesha amealikwa South?
 
Katika hali asiyo itarajia FUNDI Adam kinyekile(34) ,Alitembelewa na Wazungu wawili waliotoka simiyu hifadhi ya mwimba kuchukua mabaki ya helikopta iliyo tunguliwa na Majangili,wazungu hao walimtafuta na kuonana nae kisha wakamwuliza maswali mengi sana kuhusu ubunifu wake wa kuunda helikopta hiyo pamoja na malighafi alizotumia

hel2.jpeg
hel2.jpeg

wazungu hao waliridhika na majibu ya Adamu KINYEKILE na kukubali kazi yake na kumpa mwaliko wa kwenda afrika ya kusini.

Hata hivyo baada ya kuweka picha walizopiga na wazungu hao kwenye ukurasa wake wa fB ndipo alipopokea simu kutoka kwa MENEJA WA TCCA MBEYA NA KUMJULISHA KUNA WAGENI wata mtembelea kutoka makao makuu ya TCCA DAR ES SALAAM.

Mbali na hapo awali baada ya taarifa hizi kuzagaa kwenye mitandao mamlaka ya usafiri wa ANGA Tanzania ilipiga marufu mtu yeyote kujihusisha na utengenezaji wa ndege bila kufuata utaratibu,gazeti la mwananchi la leo limeandika onyo hilo lilionekana kumlenga ADAMU KINYEKILE.

Wadadisi wa mambo wanahoji wakati mamlaka ikitoa onyo hilo ilikua haijawahi kumtembelea hata siku moja zaidi ya kiongozi wa mbio za mwenge aliweka jiwe la msingi kwenye eneo la ubunifu huo.

jaribu kujiuliza mkoani DODOMA kuna jama alijulikana kwa jina la BAHATI ALIWAHI KUTENGENEZA helikopta maeneo ya 77,kwa mimi mpaka leo sijui yupo wapi.

Na je hawa wabunifu wetu wa mtaani watazijuaje hizo taratibu za kutenengeneza ndege? au kwani kutengeneza ndege au helikopta ni kosa la jinai?

helik1.jpeg

Mpaka sasa ntashangaa kama WAZIRI HUSIKA HAJAFIKA ENEO HILO,LAKINI WATU KUTOKA S.A WAMEFIKA.
Ntashangaa wataalamu wetu kutoka vyuo vikuu vyote wanaofundisha utaalamu kutofika kwa kijana huyu.

NI AIBU KWA NCHI KUPUUZA WATU WENYE UWEZO HUU.

hel3.jpeg
 
Hii nchi bana!ndio mana tuliwekwa Bara la giza weusi ka mkaa aisee! hatuoni mbele!wacha weupe wafanye yao!

Shida ni pale watawala wetu wanapoabudu VYETI na sio uwezo (capability ) eti mpaka asimamiwe na mhandisi mwenye vyeti vya taaluma hiyo. Huyo mhandisi hajadiliki pamoja na vyeti vyake atamsimamiaje aliye diriki?
 
Katika hali asiyo itarajia FUNDI Adam kinyekile(34) ,Alitembelewa na Wazungu wawili waliotoka simiyu hifadhi ya mwimba kuchukua mabaki ya helikopta iliyo tunguliwa na Majangili,wazungu hao walimtafuta na kuonana nae kisha wakamwuliza maswali mengi sana kuhusu ubunifu wake wa kuunda helikopta hiyo pamoja na malighafi alizotumia

View attachment 373798 View attachment 373798

wazungu hao waliridhika na majibu ya Adamu KINYEKILE na kukubali kazi yake na kumpa mwaliko wa kwenda afrika ya kusini.

Hata hivyo baada ya kuweka picha walizopiga na wazungu hao kwenye ukurasa wake wa fB ndipo alipopokea simu kutoka kwa MENEJA WA TCCA MBEYA NA KUMJULISHA KUNA WAGENI wata mtembelea kutoka makao makuu ya TCCA DAR ES SALAAM.

Mbali na hapo awali baada ya taarifa hizi kuzagaa kwenye mitandao mamlaka ya usafiri wa ANGA Tanzania ilipiga marufu mtu yeyote kujihusisha na utengenezaji wa ndege bila kufuata utaratibu,gazeti la mwananchi la leo limeandika onyo hilo lilionekana kumlenga ADAMU KINYEKILE.

Wadadisi wa mambo wanahoji wakati mamlaka ikitoa onyo hilo ilikua haijawahi kumtembelea hata siku moja zaidi ya kiongozi wa mbio za mwenge aliweka jiwe la msingi kwenye eneo la ubunifu huo.

jaribu kujiuliza mkoani DODOMA kuna jama alijulikana kwa jina la BAHATI ALIWAHI KUTENGENEZA helikopta maeneo ya 77,kwa mimi mpaka leo sijui yupo wapi.

Na je hawa wabunifu wetu wa mtaani watazijuaje hizo taratibu za kutenengeneza ndege? au kwani kutengeneza ndege au helikopta ni kosa la jinai?

View attachment 373797

Mpaka sasa ntashangaa kama WAZIRI HUSIKA HAJAFIKA ENEO HILO,LAKINI WATU KUTOKA S.A WAMEFIKA.
Ntashangaa wataalamu wetu kutoka vyuo vikuu vyote wanaofundisha utaalamu kutofika kwa kijana huyu.

NI AIBU KWA NCHI KUPUUZA WATU WENYE UWEZO HUU.
Wangu hao wakuwapi
 
Si tumeambiwa hajui kusoma wala kuandika?

Sasa kwenye kampuni inayotengeneza ndege atakuwa anawasilishaje idea zake.

THE KICK.
Wa Mbeya anajua, yule g/mboto mzee wa gari la kifahari ndo hajui
 
Katika hali asiyo itarajia FUNDI Adam kinyekile(34) ,Alitembelewa na Wazungu wawili waliotoka simiyu hifadhi ya mwimba kuchukua mabaki ya helikopta iliyo tunguliwa na Majangili,wazungu hao walimtafuta na kuonana nae kisha wakamwuliza maswali mengi sana kuhusu ubunifu wake wa kuunda helikopta hiyo pamoja na malighafi alizotumia

View attachment 373798 View attachment 373798

wazungu hao waliridhika na majibu ya Adamu KINYEKILE na kukubali kazi yake na kumpa mwaliko wa kwenda afrika ya kusini.

Hata hivyo baada ya kuweka picha walizopiga na wazungu hao kwenye ukurasa wake wa fB ndipo alipopokea simu kutoka kwa MENEJA WA TCCA MBEYA NA KUMJULISHA KUNA WAGENI wata mtembelea kutoka makao makuu ya TCCA DAR ES SALAAM.

Mbali na hapo awali baada ya taarifa hizi kuzagaa kwenye mitandao mamlaka ya usafiri wa ANGA Tanzania ilipiga marufu mtu yeyote kujihusisha na utengenezaji wa ndege bila kufuata utaratibu,gazeti la mwananchi la leo limeandika onyo hilo lilionekana kumlenga ADAMU KINYEKILE.

Wadadisi wa mambo wanahoji wakati mamlaka ikitoa onyo hilo ilikua haijawahi kumtembelea hata siku moja zaidi ya kiongozi wa mbio za mwenge aliweka jiwe la msingi kwenye eneo la ubunifu huo.

jaribu kujiuliza mkoani DODOMA kuna jama alijulikana kwa jina la BAHATI ALIWAHI KUTENGENEZA helikopta maeneo ya 77,kwa mimi mpaka leo sijui yupo wapi.

Na je hawa wabunifu wetu wa mtaani watazijuaje hizo taratibu za kutenengeneza ndege? au kwani kutengeneza ndege au helikopta ni kosa la jinai?

View attachment 373797

Mpaka sasa ntashangaa kama WAZIRI HUSIKA HAJAFIKA ENEO HILO,LAKINI WATU KUTOKA S.A WAMEFIKA.
Ntashangaa wataalamu wetu kutoka vyuo vikuu vyote wanaofundisha utaalamu kutofika kwa kijana huyu.

NI AIBU KWA NCHI KUPUUZA WATU WENYE UWEZO HUU.
Unamlenga Julius Sunday Mtatiro
 
Eti pawe na mhandisi aliyebobea katika kutengeneza helicopter amsimamie, Tanzania kuna mhandisi anaweza kuunda helcopter? Masharti mengi kiasi kwamba ukiwa na ndoto zako zinazimika mara moja. Ati badala ya serikali kuonesha ushirikiano na kumhamasisha wamekaa kwenye computer wanachapa barua kwenye word hata kuchapa vizuri hawawezi na kumpiga jamaa stop. Ngoja wanaojua thamani ya hawa watu wamchukue.
 
Hata China waliaanza na kutengeneza vitu feki na kuuza kwa bei ya chini, Tanzania ukiwa mbunifu kidogo tu shida watakuja na sheria na kanuni na protocols mpaka unaweza ishia jela. Sasa tutaendeleaje maana kukaa shuleni na kujiita engineer hatuoni wanagundua mashine zozote wala vitu vya maendeleo. Nyumbu toka kipindi cha Nyerere mpaka leo sijui kama ishawahi unda gari, Na huyo wa Mbagara na gari yake hadi karuhusiwa kwenda sabasaba ni maajabu ya Dunia.
 
Hawa waandishi wetu wanaojifanya waatalam na wanaopiga marufuku watu kuunda vyombo,
Wao hata kuunda jiko la mchina la madura ya taa hawawezi..... Wanabakiaaa kukariri tu
 
Tanzania inakuwaje na mhandisi wa ndege wakati haina mafundi wa kuzitengeneza?
Hapo kinachotakiwa, hawa hawa wanaotia makatazo, wanatakiwa kwenda kuiona ndege husika, kisha kuwatafuta wahandisi waelekezi kutoka kokote kwa gharama za serikali, ili kumuongezea skills fundi aweze kulekebisha kasoro zitakazotajwa na mhandisi mwelekezi, akifanikiwa kurusha.

Hiyo ndege baada ya ushauri wa mtaalamu aliyeletwa na serikali kwa kukuza kipaji cha mhusika, apelekwe kwenye viwanda vya kutengeneza sasa, ili kukomunika akirudi atakiwa ndiye injinia tanzania!!
 
Hiyo helicopter ni model mpya au?...halafu ni fantastic maana milango inafunguka kwenda juu badala ndege ndo iende juu.
 
Back
Top Bottom