Mtanzania akamatwa na unga China ananyongwa J'nne

Serikali ya Wasanii na wachina feki ndio waliosaini! Sheria ya china ipo palepale! Juhudi za kumnusuru zinahitajika!

Juhudi zifanyike kwenye mambo ya msingi sio kwa UPUMBAFU kama huu; ili mwisho wa siku tuanze tena kutumia muda wetu kumjadili alohusika na kumnusuru hayawani huyu; la hasha wacha sheria ifate mkondo wake"
 
No way out lazima tuheshimu sheria tunaishi kwa sheria kila mahali ni kujifunza na kujipanga pole kwa familia ubalozi uangalie kama kuna namna money inaweza nunua sheria sisi tunajisumbua hapa wenye mali watafanya namna tu

jamani kuna nchi unaweza kuongelea mambo ya pesa ndio inaongea,lakini sio uchina,yaani issue ikishakuwa ni madawa na wakajiridhisha kuwa ni kweli unayo imekula kwako hata iwe ni 0.006g

yaani sheria zao zipo wazi sana na huwa hawana kuchelewesha kesi ili mradi tu wanakidhibiti

huwezi nunua kesi wala dawa haziwezi pungua uzito zikiwa kituo cha polisi,kwani hata polisi wao wanaelewa fika kuwa sheria yao ni death pernaty

kama ni kweli kakamatwa tusubiri wiki ijayo kuletewa majivu kama tunayahitaji
 
YERICKO

Unajidanganya,umezoea Tanzania kuwa tutayaongea na yataisha,china hiyo haipo,nakueleza haipo na haiwezi tokea hata aende obama,

wanamsemo wao kuwa " NO WAY OUT"

soma hapa chini

China has executed a South African woman for drug smuggling, rejecting an appeal by President Jacob Zuma to spare her life, an official says.

Daaah inasikitisha sana mkuu, nimeishi Beijing kwa miaka mitatu, nimeona sheria zikizingatiwa pale china kuliko kitu chochote, daah lakini hii ya mtz imenihuzunisha mkuu! Sheria ifuate mkondo kama ni kunyongwa na anyongwe!
 
Hivi na mjomba (Mpoto) ilikuwaje nasikia Baba Liz alienda kumtetea????????
 
Hivi ile kesi ya yule mtoto wa liyumba na mwenzake waliishia wapi na unga kontena zima
 
China hawana mchezo na ufisadi. Wale jamaa zetu wanaojirahisi kutumiwa kubeba miunga waogope uchina na uarabuni. kule hakuna upuuzi kama Bongo ambapo wanapita Airport na kutoa chochote kitu na kupeta. RIP Zuberi.
 
Hivi ile kesi ya yule mtoto wa liyumba na mwenzake waliishia wapi na unga kontena zima

huyo dada wa SA alinyongwa kwa kubeba 3kg of methamphetamine,ina maana kama ni container kwa wachina hiyo kesi ingekuwa imekwisha na wahusika wangesha oza kitambo sana

na jiulize haki za binadamu mbona hawaonekani uchina? mbona hatuwasikii wakipiga kelele uchina wala kwenda uchina kuandamana?

wanaelewa kuwa wakienda uchina kwanza hawatarudi,mbili USA haitawasaidia na tatu watahukumiwa kwa sheria za uchina

utawaona wakija tanzania na nchi nyingine ambazo kwao wanaelewa kuwa hawatakamatwa wala kushitakiwa

HONGERA UCHINA

[FONT=Arial, Helmet, Freesans, sans-serif]
[/FONT]
 
Mh!Hii iwe fundisho kwa waliobaki wenye tabia kama hiyo. Watanzania tujishughulishe na biashara halali,tuachane na shughuli zozote haramu. Pole kwa ndugu,jamaa na wakubwa wake wa kazi.
 
Dah!?! Huyu Zuberi vipi tena? Kila siku wenzie wanapeleka Sauzi na Ulaya, yeye kajichanganya kwa wachina. ...RIP.
 
Taarifa za kuaminika nikuwa,
Mtanzania
akamatwa na unga China ananyongwa J'nne anaitwa Zuberi, Ni mkaazi wa Mzanzibar aliwahi kuishi Canada! Sijui atasaidiwa vipi maana yeye ni container tu Ma don wapo Bongo

Kina Ngereja na Nundu wananyongwa lini? Mbunge wa Nkasi alipendekeza hilo
 
Kina Ngereja na Nundu wananyongwa lini? Mbunge wa Nkasi alipendekeza hilo

Na hapo ndipo ilinganishwe ... madhara ya Unga kwa jamii na madhara ya kufuja mali ya umma kwa jamii kipi hasa cha hitaji adhabu ya kifo!!!
 
Miaka miwili nyuma kuna muingereza zuzu alibebeshwa cocaine kuingiza China na alikamatwa Airport naye alinyongwa bila kujali kama ana mtindio wa ubongo. Usichezee Peking
 
Kwa kubeba madawa hayo kanyonga wengi sana,
Sasa yeye serikali infanyie nini?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom