Mtanzania akamatwa Indonesia akiwa na dawa za kulevya kilo 1 tumboni.

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Raia mmoja wa Tanzania aliyetambulika kwa jina la Abdul Rahman Asman anadaiwa kukamatwa Bali nchini Indonesia akiwa na dawa za kulevya alizokuwa amemeza tumboni.
narkoba-tanzania-01-960x639-600x399.jpg

Maofisa katika Uwanja wa Ndege wa Bali wameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa Mtanzania huyo alikamatwa Januari 30, 2019.

Wamesema alipopekuliwa alibainika alikuwa amemeza dawa hizo ambazo hata hivyo hazikufafanuliwa ni za aina gani. Lakini baadhi ya ripoti zilisema dawa alizokutwa nazo zinafahamika kwa jina la methamphetamine.

“Mtanzania huyo alikamatwa Bali akiwa na kilo kadhaa za dawa hizo,” chanzo cha habari kilisema.

Taarifa zaidi zimedai kuwa alipofanyiwa uchunguzi wa XRay na CT scan aligundulika kuwa na paketi kadhaa za plastiki na ndani yake kukiwa na unga.

Haikulezwa ni lini atapandishwa mahakamani na haikufahamika mara moja iwapo upande wa mashtaka utataka mtuhumiwa huyo ahukumiwe adhabu ya kifo.

Indonesia inatajwa kuwa ni moja ya mataifa duniani yenye sheria kali dhidi ya makosa yanayohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Kuna mlolongo wa watuhumiwa wanaosubiria adhabu ya kifo wakiwamo raia wa Uingereza, Marekani na wengine kutoka Afrika Magharibi ambao wamenyongwa ahadi kufa baada ya kutiwa hatiani.

-UDS
 
Raia mmoja wa Tanzania aliyetambulika kwa jina la Abdul Rahman Asman anadaiwa kukamatwa Bali nchini Indonesia akiwa na dawa za kulevya alizokuwa amemeza tumboni.View attachment 1020928

Maofisa katika Uwanja wa Ndege wa Bali wameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa Mtanzania huyo alikamatwa Januari 30, 2019.

Wamesema alipopekuliwa alibainika alikuwa amemeza dawa hizo ambazo hata hivyo hazikufafanuliwa ni za aina gani. Lakini baadhi ya ripoti zilisema dawa alizokutwa nazo zinafahamika kwa jina la methamphetamine.

“Mtanzania huyo alikamatwa Bali akiwa na kilo kadhaa za dawa hizo,” chanzo cha habari kilisema.

Taarifa zaidi zimedai kuwa alipofanyiwa uchunguzi wa XRay na CT scan aligundulika kuwa na paketi kadhaa za plastiki na ndani yake kukiwa na unga.

Haikulezwa ni lini atapandishwa mahakamani na haikufahamika mara moja iwapo upande wa mashtaka utataka mtuhumiwa huyo ahukumiwe adhabu ya kifo.

Indonesia inatajwa kuwa ni moja ya mataifa duniani yenye sheria kali dhidi ya makosa yanayohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Kuna mlolongo wa watuhumiwa wanaosubiria adhabu ya kifo wakiwamo raia wa Uingereza, Marekani na wengine kutoka Afrika Magharibi ambao wamenyongwa ahadi kufa baada ya kutiwa hatiani.

-UDS
Huyo ni kifo tu kwa firing squad,wenzetu hawapendi ujinga,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara chache humezwa kupitia mdomo, ila hua wanaziingiza kutumia sehemu ya siri (nyuma), japo kuna wachache hua wanazimeza. Ingia youtube kuna video za watu wengi waliowahi kufanya hio kazi wanaongea jinsi wanavyofanya, inatisha sana.
Basi tigo zao zinakuwa kubwa hata dushe la punda haliwezi kufit.
Hizi pesa zinawaachia watu vilema vya kujitakia!!
 
Back
Top Bottom