TANZIA Mtanzania afariki Ufaransa, msaada unahitajika ili ndugu wapate taarifa

UBALOZI SAFIRISHENI MAITI HADI DAR HIVI KWANINI HAMTAKI KUJIFUNZA KWA BALOZI NYINGINE?

MNAPITISHA BAKULI WAKATI MNA FUNGU LA KUFA NA KUZIKANA? INA MAANA WATANZANIA WAISHIA UFARANSA HAWANA UMOJA WA KUFA NA KUZIKANA?

SISI HUKU HATUWEZI KUCHANGA NI TOZO JUU YA TOZO. MAMA ANAUPIGA MWINGI KWERII KWERII!
 
Ok kama hakuwa na passport ya tanzania basi alibadili uraia na sisi tanzania haturuhusu uraia pacha so wazike mungu ni wetu sote
Hivi unaelewa watu wanaposema "alikuwa na ugonjwa wa akili"?

Hivi unafahamu mtu mwenye ugonjwa wa akili anaweza hata kutoka nje bila nguo?!

Sasa kama anaweza "kusahau" hata alipoweka nguo, hivi mtu kama huyo unatarajia atafahamu lolote kuhusu kuwa na passport?!

Unadai waende uhamiaji...

Mtu mwenye umri wa miaka 61, ambae ameenda huko miaka kadhaa, uliwahi kujiuliza ikiwa taarifa zake zinaweza kuwa in electronic database?

Mbaya zaidi, jina lake halipo unique, surname yake yenyewe ni Mohamed... ulishawahi kujiuliza ugumu wa kutafuta taarifa kupitia jina kama hilo?
 
Wewe Acha janja janja hata huitwe mohamed na akuna jina unique duniani mzee ana miaka 60 tufanye kaenda huko na miaka 30 so itakuwa KWA makadirio kaenda 90s so miaka 30 iliyopta idara inakosaje kumbukumbu za muda kama huo??
 
Poleni ndugu ,jamaa na marafiki.

Ubalozi wamejuaje kama ni Mtz? Wamejuaje jina lake? Kama thru Passport basi watafute taarifa alizojaza enzi anaapply pspt.

Mbowe ,Adamoo sio Magaidi.
 
Wengine n wazamiaj tu ingekuwa ana passport taarifa zake zote zingekuwa wazi
Kwa umri huo ni wale wazamiaji waliotumia passpoti zile za kufunguliwa faili la kuandikwa kwa mkono na jina kuandikwa kwa mwandiko mcharazo amazing ambao ni mtu mmoja tu alikuwa anaandika hizo pasi, ni pasi ambazo watu wengi waliweza kughushi na kujiita Watanzania kumbe ni Warundi/Wakongo/Wasauzi/Wakenya na hata hazina kumbukumbu.
 
Wewe Acha janja janja hata huitwe mohamed na akuna jina unique duniani mzee ana miaka 60 tufanye kaenda huko na miaka 30 so itakuwa KWA makadirio kaenda 90s so miaka 30 iliyopta idara inakosaje kumbukumbu za muda kama huo??
Seems like hujui watu walikuwa wanaenda vipi mbele miaka ya nyuma....

FYI, moja ya changamoto wanazopata balozi zetu za nje ni kutokuwa na idadi sahihi ya Watanzania waliopo huko!!!

Sasa tatizo linakuja inapotokea mtu amefariki au kutupwa jela!! Mamlaka za huko zinakuletea taarifa kwamba huyu ni mtu wenu lakini mkiangalia kwenye rekodi, hayupo kwa sababu aliingia kwa kujilipua, na kwahiyo ubalozi haumfahamu!!

Miaka hiyo hiyo, enzi wa-South waliokuwa Tanzania wanarudi kwao baada ya uhuru, kuna mwana mmoja kitaa, sijui alifanya fanya vipi, anajua mwenyewe!! Mshikaji akaondoka na wa-SA kama mtu wa South Afrika wakati ni Mbongo PURE kwa sababu, hata Bush, nyumba yao na ya kwetu zinatazamana!!

Kama ilivyo ada ya Wabongo, mwana kafika SA, akaanza kuuza powder. Moja ya trips zake akaenda Amsterdam akadakwa, na kula mvua!!

Now assume huyu angekutwa na umauti huko Uhalonzi au nchi yoyote... it's obvious, mamlaka za huko zingewasiliana na ubalozi wa South Africa!

Ubalozi wa South Africa ungehangaika kutafuta ndugu zake huko SA, na wasingewapata na labda katika tafuta tafuta hiyo wangegundua kwamba mwana ni Mbongo!!!

Hatimae taarifa zingefika ubalozi wa Tanzania ambao hakuna records zake, na kwahiyo wangelazimika kufanya kama walivyofanya hao wa Ufaransa!!

Na mfano mwingine, ni kama pale Wanyarwanda waliokuwa ukimbizini TZ walipopelekwa Canada!!

We unadhani hakuna Wabongo ambao walijichomeka mle?! Na kama wapo, unadhani ubalozi wa Tanzania nchini Canada watakuwa na taarifa zao wakati wameenda huko kama Wanyarwanda?
 
Back
Top Bottom