Mtanzania adai kugundua dawa ya corona, ataka kuonana na Waziri wa Afya

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,281
EW4mnkAXsAA9BGe.jpeg


MKAZI wa Chanika jijini Dar es Salaam Seleman Mwamsumbwe (pichani kushoto) akiwa na dada yake(kulia) ameomba kukutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa lengo la kumueleza habari njema ya kwamba amegundua dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa COVID-19 unaotokana na virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani Chanika huku akiwa na furaha na tabasabu tele Mwamsumbwe amesema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua hawezi kuitaja hadharani kwa sasa hadi pale atakapoona na Waziri Ummy Mwalimu.
"Natambua changamoto kubwa Dunia inapitia kwa sasa na kusababisha mataifa mbalimbali kuhaha kutafuta tiba ya corona Dawa yangu ambayo tayari nimeifanyia utafiti wa kutosha nimjeridhisha ina uwezo wa kutibu ugonjwa huo bila tatizo lolote, naomba kukutana na Waziri wa Afya nizungumze naye na kisha nipate baraka ili kuokoa maisha ya watu ambayo yanaangamia kwa Corona,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu dawa hiyo Mwamsumbwe amesema kwamba dawa hiyo inauwezo wa kutibu mfumo mzima wa mapafu, kuondoka mafua makali pamoja kikohozi.
."Namuomba Waziri wa aje tuonane ninahakika dawa hii itasaidia kuponya ugonjwa huu wa Corona au kupunguza makali ya gonjwa."amesisitiza na kuongeza anao uhakika wa asilimia 100 wa dawa hiyo kutibu Corona.

Mkazi wa Chanika Dar, Seleman Mwamsumbwe ambae anadai kugundua dawa ya kutibu Corona akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake kuhusu dawa hiyo ambapo ameomba kukutana na Waziri wa Afya ili kuzungumza nae kwa kina.


Swali kama ana dawa kwanini kavaa maski kubwa hivyo ?
 
Kwa hiyo kwasababu mseto ipo huwa unaenda kulala walipo Mbu ili wagun'gate umeze mseto?
Silali na chandarua mimi!Ila Malaria ingekuwa haina tiba weee saa 1 niko ndani ya chandarua!
 
Back
Top Bottom