GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Sijui ni lini huyu Mtangazaji ataacha hii tabia yake ya kipuuzi na ya kimakusudi ambayo sasa ameshaifanya kama vile kuwa ndiyo utaratibu wake wa kila siku anapokuwa Kazini hapo Studioni Efm.
Ni kwamba kila pale ambapo kunakuwa na taarifa ya ' kuiathiri ' Klabu ya Simba Sports Club au taarifa ' mbaya ' ya kuihusu Simba SC au ina ' uelekeo ' mbaya kwa Simba SC yeye katika kutafuta ' maoni ' ya ama Wadau wa mpira au wenye Mamlaka ya Kitaaluma ya kuhusu mchezo wa mpira wa miguu yeye huwapigia tu wale ambao ni Wana Yanga FC ' lia lia ' kabisa halafu anawahoji na hata akiwa anawahoji huanza kwanza kuwauliza ' Maswali ' shawishi ambayo automatically tu yatamfanya yule anayeongea nae aelekee kule ambapo anakutaka Yeye na hapa namaanisha Yanga FC ambako hakuna asiyejua kuwa Mtangazaji Maulid Kitenge ni Mwanachama wake wa ' Kutukuka '.
Wanataaluma wa hiyo ' Tasnia ' sasa tumechoshwa kabisa na hii tabia ya ' hovyo hovyo ' hasa ya Kiutangazaji ambayo anaifanya Maulid Kitenge kiasi kwamba sasa anaanza ' kutukera ' wasikilizaji wa Vipindi vyao vyote vya michezo vya Efm.
Tunamtaka abadilike upesi kama siyo haraka vinginevyo sasa nasi ' anaotuudhi ' tutaamua ' kufyatuka ' dhidi yake.
Mbona Watangazi wenzie wengi tu wakiwa wanatangaza huwa hawaonyeshi ' Mahaba ' yao upande fulani japo sisi Watu wa mpira ( michezo ) huwa tunawajua wapo wapi Kiushabiki? Nani anayeweza kujua Mtangazaji Said Kilumanga au Alex Luambano au Amri Masare wanashabikia Vilabu / Timu gani hapa Tanzania?
Mfikishieni taarifa hii kuwa tumemchoka na karibuni sasa sisi anaotuumiza uvumilivu dhidi yake utafikia ' Kikomo '.
Nawasilisha.