Mtangazaji wa Clouds alalamikia kutishiwa na Haji Manara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
P R I S C A - K I S H A M B A !
- Mwandishi / Mtangazaji wa clouds fm ametishiwa kudhalilishwa na msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

"KOSA LANGU NINI? Leo nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa klabu ya Simba SC na waandishi wa habari za michezo mkutano ambao uliongozwa na Haji Manara"

"Baada ya mkutano kumalizikiza Haji aliporuhusu maswali kwa waandishi waliokuwepo miongoni mwao waliouliza maswali ni mwandishi wa habari ABDUL DUNIA"

"Alimuuliza Haji 'Rekodi za michezo (3) ya mwisho kati ya Simba na Yanga ya ligi kuu inaonesha Yanga ilikuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba, huoni kwamba kwa rekodi hii ubora wenu uko kwa timu zingine na sio kwa YANGA ?"

"Haji Manara aliwaka sana na kumshushia maneno mwandishi yule na kumtuhumu kuwa yeye ni shabiki wa Yanga na ametumwa na Yanga, akamwambia siku zingine akienda kwenye PRESS awe na maswali ya kueleweka na sio maswali UCHWARA"

"Baada ya Haji kuwaka nikanyoosha mkono kumuuliza Haji kuwa, ni vyema kwa kuwa umetoa nafasi kwa watu kukuuliza maswali ujibu kwa kuwa swali hilo lilikuwa na lengo zuri tu"

"Kama kawaida Haji Manara alitumia mkutano huo uliokuwa live kwenye television na blogs mbalimbali kuniambia maneno ya VITISHO akiahidi KUNIDHALILISHA kwani anadai ana SMS zangu nyingi ambazo sio nzuri alisema..."

"Kaa kimya wewe, tena wewe ndio nilikuwa NAKUTAFUTA kwa muda mrefu, NITAKUDHALILISHA, hapa nina SMS zako huna adabu unanivunjia heshima kwenye press zangu kama nani?! Alisema Manara dhidi yangu"

"Mkutano ulipoisha Manara alipita na kunifuata nilipokuwa nimesimama akarudia tena akiahidi KUNIDHALILISHA siku moja huku akininyooshea kidole usoni"

"Nilijisikia vibaya kama binadamu, wakati huo alikuwa anatoka nje akiwa ameambatana na watu kadhaa, nilitoka nje ya ukumbi kumfuata na kumuita, nikamwambia 'Haji naomba usimame, nikamwambia kwa nini kila kunapokuwa na hadhara ya watu huwa unatishia KUNIDHALILISHA ?! Ni wapi nilikukosea?

"Nikamwambia naomba tumia fursa hii kuwaonesha waandishi hizo SMS zangu unazosema ni mbaya"

"Haji alinisogelea na kutaka KUNIKUNJA mbele ya UMMA wa Waandishi wa habari, waandishi kadhaa waliokuwepo wakawahi kumshika nami akanishika kaka anaitwa JACKSON kutoka NCARD kitengo cha mauzo aliyekuwa sehemu ya mkutano ule pamoja na MUSSA MWKISU na wengine waliokuwepo"

"Hii sio mara ya kwanza Haji kutumia jukwaa la watu KUNIDHALILISHA, ameshafanya hivyo kwenye group moja la WHATSAPP la Taifa stars kwa kuniita majina yasiyofaa"

"Nitafikisha ombi hili kwenye ofisi ya muajiri wangu kuandika barua kwenda uongozi wa SIMBA SC. Haji amenitishia mara kadhaa nikiwa kwenye majukumu yangu, ametishia KUNIDHALILISHA hata kupitia mitandao ya kijamii"

"Manara asitumie umaarufu wake, asitumie kivuli cha klabu yake ya Simba kutaka kuwadhalilisha watoto wa kike"

🔍 Prisca Kishamba
 
Yuko mmoja wa clouds juzi akawa anamuuliza kusah
Mo j; Nnasikia demu wako aunt ezekiel anadanga
Ningekuwa kusah huyu jamaaa angekuwa anatembelea wheelchair kwa sasa

Hawa waandishi wa bongo wana upumbavu mwingi
Hawako proffesional hata kidogo
Just imagine mtu anakuuliza swali kama hilo alafu anategemea umjibu vizuri eti kisa ni mwandishi wa habari hii si kweli na haifai hata kidogo

Waandishi mbadilike
 
Kakudhalilisha vipi ama kakuambia kuwa una sura mbaya na ngumu. Haukuona cha kufanya mpaka umekimbilia kuandika habari za soka! Vumilia huko ni pagumu sana kupigwa nje nje acha matusi. Muulize marehemu James Nnende alivyopigwa ndoga na Mogela. Ukiandika Siasa ujue pia utauliwa tu. Kila kazi ni ngumu hata ukienda kulima panya na nyani watakula mazao yako. Tuachie Lunyasi yetu. Ndio una sura mbaya hali ubishi..na waandishi nyie mna njaa sana uenda uliomba hela kwa Haji.
 
Manara leo kachemka bigly
Ni suala kubwa.
Ni kosa NJE ya soka.
Ni harrasment
Ni retaliation
Ni threat

Wa kuchukua hatua si Prisca pekee.
Ni Simba
Ni Clouds Media Group.
Ni TASWA
Ni TFF

Jamii itachukulia poa, ila kakosea sana

Ila acha atukanwe Tu njaa Zao na kujikomba kwa Simba, nakaonaga kako kimbelembele kuripoti habari za Simba... Wacha watukanwe Tu hakuna namna ***** Zao.
 
Maswali ya technical unamuuliza haji??

Haji kazi yake ni PR angemuuliza maswali ya kishabiki zaidi...

Hii phase ya kina Haji na Jerry Muro kufanya press conference badala ya makocha na wachezaji itaisha soon...
Tena jamaa linasema eti we ndio nilikuwa nakutafuta kuonesha ni kinyongo tu wala tatizo sio swali. This is Public Assault. Ila haya tuwaachie mamlaka na wao wenyewe. Tusiwaingilie, Watapatana hapa muonekane wabaya. Hamjifunzagi tu ? Hili sio la kwanza. Kuna mahali tulishakubali kukosea, tuendelee kukosea. Aliwahi kuwaita Taka².
 
P R I S C A - K I S H A M B A !
- Mwandishi / Mtangazaji wa clouds fm ametishiwa kudhalilishwa na msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara.

"KOSA LANGU NINI ? Leo nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa klabu ya Simba SC na waandishi wa habari za michezo mkutano ambao uliongozwa na Haji Manara"

"Baada ya mkutano kumalizikiza Haji aliporuhusu maswali kwa waandishi waliokuwepo miongoni mwao waliouliza maswali ni mwandishi wa habari ABDUL DUNIA"

"Alimuuliza Haji 'Rekodi za michezo (3) ya mwisho kati ya Simba na Yanga ya ligi kuu inaonesha Yanga ilikuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mazuri dhidi ya Simba, huoni kwamba kwa rekodi hii ubora wenu uko kwa timu zingine na sio kwa YANGA ?"

"Haji Manara aliwaka sana na kumshushia maneno mwandishi yule na kumtuhumu kuwa yeye ni shabiki wa Yanga na ametumwa na Yanga,, akamwambia siku zingine akienda kwenye PRESS awe na maswali ya kueleweka na sio maswali UCHWALA"

"Baada ya Haji kuwaka nikanyoosha mkono kumuuliza Haji kuwa, ni vyema kwa kuwa umetoa nafasi kwa watu kukuuliza maswali ujibu kwa kuwa swali hilo lilikuwa na lengo zuri tu"

"Kama kawaida Haji Manara alitumia mkutano huo uliokuwa live kwenye television na blogs mbalimbali kuniambia maneno ya VITISHO akiahidi KUNIDHALILISHA kwani anadai ana SMS zangu nyingi ambazo sio nzuri alisema..."

"Kaa kimya wewe, tena wewe ndio nilikuwa NAKUTAFUTA kwa muda mrefu, NITAKUDHALILISHA, hapa nina SMS zako huna adabu unanivunjia heshima kwenye press zangu kama nani ?! Alisema Manara dhidi yangu"

"Mkutano ulipoisha Manara alipita na kunifuata nilipokuwa nimesimama akarudia tena akiahidi KUNIDHALILISHA siku moja huku akininyooshea kidole usoni"

"Nilijisikia vibaya kama binadamu, wakati huo alikuwa anatoka nje akiwa ameambatana na watu kadhaa, nilitoka nje ya ukumbi kumfuata na kumuita, nikamwambia 'Haji naomba usimame,, nikamwambia kwa nini kila kunapokuwa na hadhara ya watu huwa unatishia KUNIDHALILISHA ?! Niwapi nilikukosea ?

"Nikamwambia naomba tumia fursa hii kuwaonesha waandishi hizo SMS zangu unazosema ni mbaya"

"Haji alinisogelea na kutaka KUNIKUNJA mbele ya UMMA wa Waandishi wa habari, waandishi kadhaa waliokuwepo wakawahi kumshika nami akanishika kaka anaitwa JACKSON kutoka NCARD kitengo cha mauzo aliyekuwa sehemu ya mkutano ule pamoja na MUSSA MWKISU na wengine waliokuwepo"

"Hii sio mara ya kwanza Haji kutumia jukwaa la watu KUNIDHALILISHA, ameshafanya hivyo kwenye group moja la WHATSAPP la Taifastars kwa kuniita majina yasiyofaa"

"Nitafikisha ombi hili kwenye ofisi ya muajiri wangu kuandika barua kwenda uongozi wa SIMBA SC. Haji amenitishia mara kadhaa nikiwa kwenye majukumu yangu, ametishia KUNIDHALILISHA hata kupitia mitandao ya kijamii"

"Manara asitumie umaarufu wake, asitumie kivuli cha klabu yake ya Simba kutaka kuwadhalilisha watoto wa kike"

🔍 Prisca Kishamba
View attachment 1836151
Donald Trump wa Bongo. Kiburi huja kabla ya kuanguka.
 
Kakudhalilisha vipi ama kakuambia kuwa una sura mbaya na ngumu. Haukuona cha kufanya mpaka umekimbilia kuandika habari za soka! Vumilia huko ni pagumu sana kupigwa nje nje acha matusi. Muulize marehemu James Nnende alivyopigwa ndoga na Mogela. Ukiandika Siasa ujue pia utauliwa tu. Kila.kazi ni ngumu hata ukienda kulima panya na nyani watakula mazao yako. Tuachie Lunyasi yetu. Ndio una sura mbaya hali ubishi..na waandishi nyie mna njaa sana uenda uliomba hela kwa Haji.
Dah
 
Back
Top Bottom