Mtangazaji wa BBC Fred Mtoi afariki dunia

Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,173
708
fred.jpg
Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania
 
Inasikitisha sana.
Amefariki lini? Nini chanzo cha kifo chake?
Kijana mdogo bado na alikuwa katika harakati za kukamilisha ndoto zake.
RIP Fred. Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu awape nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu. Pole kwa wana-BBC na waandishi wa habari kwa ujumla. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.
 
R.I.P Fred Mtoi, nitakukumbuka daima kwa mahojiano tofauti tuliyoyafanya katika vipindi vyako!
 
RIP Bro Fred...yaani jana tumekuja kukuona Hospitali hatukujua kuwa tulikuwa tunakuaga.Pumzika kwa amani bro..Poleni familia tupo pamoja.Amen
Mdau wa North
 
Mr Freddy Mtoi wa katikati, rest in eternal peace!
 

Attachments

  • Mtoi.jpeg
    Mtoi.jpeg
    80.8 KB · Views: 490
Humu JF tunae Mohammed Mtoi, so uwe unafafanua Jina zima kwenye Heading
 
Back
Top Bottom