TANZIA Mtangazaji Maarufu wa RTD Abissay Stephen amefariki dunia asubuhi hii

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,441
113,449
Wanabodi,

Nimepokea taarifa kuwa Mtangazaji Maarufu wa RTD, (sasa TBC), ABISAY STEVEN, amefariki dunia asubuhi hii.

Mpashaji habari wangu amesema msiba huo umetokea katika hospitali ya Muhimbili alikolazwa kufuatia kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa zaidi zitafuatia.

Kwa wale wa zamani huyu mtangazaji alikuwa maarufu sana enzi zike za kina David Wakati, Tido Mhando, Seif Salim Mkamba, Edda Sanga, Debora Mwenda etc. Aliwahi kuwa Mkuu wa Idhaa ya Biashara chini yake wakiweno Charles Hilary na Julius Nyaisanga.

Mpaka Mauti yalipomkuta alikuwa bado ni muajiriwa wa TBC.

Poleni wafiwa.

Mungu aiweke Roho ya Abysai Steven Uronu, Mahala Pema Peponi, apumzike kwa Amani. Amen!

UPDATE: 1
TBC wametoa update kwenye taarifa yao ya habari ya saa 2 usiku.

Marehemu atazikwa kijijini kwao Hai mkoani Kilimanjaro siku ya Jumanne.

Heshima za Mwisho ni Jumatatu saa 4 asubuhi nyumbani kwake Temeke Mikoroshoni na baadae kusaliwa Kanisa la KKKT Temeke Vetenari.

Abysai Steven alizaliwa mwaka 1951 huko Moshi. Aliajiriwa na RTD mwaka 1970 kama Mtangazaji Msaidizi Daraja la III. Alipanda ngazi mpaka mauti yalipomkuta akiwa ni Mtangazaji Mwandamizi Mkuu Daraja la I.

Marehemu ameacha mjane, watoto 3 na mjukuu 1.

Rip Abysai Stephen.

UPDATE: 2
Msiba umehamishiwa kwenye nyumba yake nyingine iliyoko Banana Kitunda.

Ili kupunguza mahangaiko, mwili wa marehemu utatoka hospitali ya Muhimbili saa 5 asubuhi moja kwa moja kanisa la KKKT Vetenari kwa misa na heshima za mwisho.

Baada ya hapo, safari ya kuelekea Hai, Moshi Kilimanjaro kwa mazishi, itaanza.

Rip Abysai Stephen

UPDATE: 3
Heshima za mwisho kwa Abysai Stephen zimemalizika hapa kanisa la KKKT Vetenary Temeke ambazo zimehudhuriwa na record ya umati wa watu kwa mtangazaji wa RTD.

Umati huo umejumuisha viongozi wa vyama na serikali, wafanyakazi wa TBC, waandishi na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari na kukolezwa na idadi kubwa ya watangazaji wakongwe wa iliyokuwa RTD.

Msafara kuelekea Hai Kilimanjaro umeanza.

RIP A.S
Paskali
Rejea
Mwandishi ni Mtangazaji wa zamani wa External Service ya RTD.
Mabandiko mengine ya mwandishi kuhusu Watangazaji wa iliyokuwa RTD
 
Duh! Poleni sana familia ya Abisaay, poleni TBC. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Kuna wakati nilisafiri kikazi Songea, huyu bwana alinisaidia sana wakati huo akiwa mwakilishi wa RTD Kanda ya Kusini. Alikuwa na mwenzake fundi mitambo akiitwa Silvanus Haule.
 
Back
Top Bottom