Mtangazaji maarufu iringa apigwa changa la macho bar ,aibiwa simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtangazaji maarufu iringa apigwa changa la macho bar ,aibiwa simu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 24, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mtandao huu jana ulikuwa na habari ya kada wa UV CCM ambaye ni mgeni mjini Iringa kuibiwa simu yake katika mazingira ya kutatanisha bar moja maarufu ambako alikwenda kutafuta mwanamke kwa ajili ya kuondoa uchovu wa kambi ya vijana inayoendelea kijiji cha Ihemi kwa vijana wa Tanzania nzima kuwepo huko,habari ambayo imesomwa pia katika kituo cha Radio Ebony Fm kupiti akipindi cha Morning Talk Show ambapo waendeshaji wa kipindi hicho waliweza kutumia taaluma yao kutoa elimu kwa umma kuhusina na utapeli huo unaofanywa kundi la wanawake watapeli mjini Iringa .

  Lakini hali hiyo ya utapeli imeonyesha kugeuka msumari wa moto kwa mmoja kati ya waendeshaji wa kipindi hicho ambaye amelipwa ujira wake wa kutoa elimu kwa umma kuhusina na wanawake hao matapeli wa simu baada ya kumgeuzia kibao mwenyewe kwa kumpora simu yake ya mkononi katika mazingira tata tofauti na yale aliyokuwa akiyatolea elimu kwa wanaume wenye tabia ya kwenda kuafuta wanawake bar.

  Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne usiku katika bar moja maarufu huku mmiliki wa mtandao huu ambaye alikuwa amekaa meza moja na mwanaharakati huyo wa elimu kwa umma kupitia kituo cha radio Ebony Fm huku wakijipumzisha kwa kupata supu ya kuku ghafla wakati wakijaribu kuondoka katika eneo hilo la bar maarufu sana nje ya ile ya kada wa CCM alipotapeliwa simu yake,ndipo alipobaini kuwa simu yake ya mkononi imepotea katika mazingira tata huku hali iliyomchanganya mwanahabari huyo na kujikuta akiwa shahidi mzuri wa ule usemi usemao usitukane mambaa kabla ya kuvuka mto.

  Mtandao huu unaamini kabisa simu ya mwanahabari huyo imepotea huku ikiwa na siri mbali mbali ila pamoja na kutoa pole kwa mhusika bado inazidi kuonyesha uhakika wa yale ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya utapeli wa simu ambao umeibuka ndani ya mji wa Iringa kwa wahudumu wa bar na wasio wahudumu wa bar zaidi ni wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wanapo kwenda katika maeno ya starehe na ikiwezekana vitu vya thamani kubwa basi kuwakabidhi kwa maandishi wahudumu wenyewe ili waweze kulinda japo kwa bar zenye wahudumu matapeli zinazidi kujikosesha wateja
   
 2. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijui ni kweli, au inanibidi niamini tu ya kuwa kweli jambo hili limetukia.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,734
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  CCM wameanza kuandaa wahuni wao wa kuiba kura na kufanya fujo wakati wa uchaguzi mkuu? Vyama vingine mnafanya nini? Ndiyo mnapigwa chenga za kisigino hivyo.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  sijaelewa mtoa mada na mchangiaji hapo juu mnaongelea nini!
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,986
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Nani huyo tena huyo Kilimasera? Au Jerry Muro?
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 9,299
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu ni kijana wa wapi?
   
 7. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii habari haijaeleweka kabisa, eeee bwana irudie kuisoma alafu ilete upya
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna vituka kibao vinakuja katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...