Mtanganyika ni nani?

Watanganyika ni Wananchi wanaopatikana upande wa pili wa Muungano! mbona haieleweki. Upande wa kwanza wa Muungano ni upi..
Maswali yote uliyouliza, majibu yake yako wazi kabisa. Muungano ni wa nchi mbili; Tanganyika na Zanzibar.

Hivyo kama Mpemba anafanya biashara/kazi Dar, bado atabakia tu kuwa Mzanzibari. Na kama kuna Mmasai anafanya shughuli zake Unguja, huyo ni Mtanganyika aliyebatizwa jina la Mtanzania.

Na kuhusu huyo Rais wa Zanzanzibar, nadhani wenye majibu sahihi ni hao waliomchagua. Ila ukija upande wa pili, wala siyo siri! Kwa sasa Watanganyika tunatawaliwa na Rais Mzanzibari.
 
Wakerewe, wajita, wakwaya, waruri na waikizu asili yao ni Haya. Ni mtawanyiko kama unavyoeleza. Ndiyo maana kuna mskilizano wa maneno na kihaya. Ni sawa na wasambaa na wapare.
 
Maswali yote uliyouliza, majibu yake yako wazi kabisa. Kama Mpemba anapatikana Dar, huyo ni Mzanzibari. Na kama kuna Mmasai anafanya shughuli zake Unguja, huyo ni Mtanganyika aliyebatizwa jina la Mtanzania...
Hayo majibu yako sio ya Katiba. Kama unasema Mpemba anayepatikana Bara ni Mzanzibar, basi fahamu pia kuwa Asili ya Kabila la Mama Samia ni kutoka Bara kwa hiyo yeye ni Mtanganyika.

Leta jingine
.
 
Kwa hiyo Tanganyika ya miaka mitatu ambayo tayari.kulikuwa na Wazanzibar ndani ya chama na Serikali.

Ujue watu wengi hawafahamu hata harakati za Uhuru kwamba Kuna Wazanzibar walishiriki na wengine Wanachama wa TANU.

Hata historia ya hii CCM nyuma ilianza mwaka 1927 na chama cha African Association ambacho kilikuwa na matawi Mjini Zanzibar, Dar na Dodoma.

..kulikuwepo na Wazungu, Wahindi, Waarabu, kwa uchache.

..kuna wakati mkuu wa majeshi alikuwa Mzungu.

..Tanganyika siku zote imebeba watu wenye asili toka maeneo mbalimbali.

..kwa msingi huo kuwepo kwa Wazanzibari sio hoja ya kufifisha madai ya kurudisha serikali ya Tanganyika.
 
Sawa kabisa hata Zanzibar kulikuwa na mchanganyiko kama huo mpaka Wachina walikuwepo. Kuna watu kutoka Comoro (Ngazija) Tabora, Kigoma, Wazaramo na hata wa kanda ya ziwa ambao waliunda African Association.

Muungano haukua wa bahati mbaya isipokuwa tulilazimika kuwa nchi mbili kutokana na mfumo wa Muingereza kuzitenganisha Bara na visiwani ilihali hata Mombasa, Malindi na Lamu zilikuwa sehemu yetu kablanya 1963.
 
Sawa kabisa hata Zanzibar kulikuwa na mchanganyiko kama huo mpaka Wachina walikuwepo. Kuna watu kutoka Comoro (Ngazija) Tabora, Kigoma, Wazaramo na hata wa kanda ya ziwa ambao waliunda African Association...
Muungano wetu ni mzuri.

Wananchi wanaupenda muungano.

Kinachowakwaza ni kuuwawa kwa serikali ya TANGANYIKA.

Pia udanganyifu uliotumika ktk kuufutilia mbali utambulisho wa MTANGANYIKA.

Udanganyifu mmojawapo ni madai kwamba Tanzania ilipata uhuru tar 9 Dec 1961.
 
..muungano wetu ni mzuri.

..wananchi wanaupenda muungano.

..kinachowakwaza ni kuuwawa kwa serikali ya TANGANYIKA.

..pia udanganyifu uliotumika ktk kuufutilia mbali utambulisho wa MTANGANYIKA.

..udanganyifu mmojawapo ni madai kwamba Tanzania ilipata uhuru tar 9 Dec 1961.
Hakuna kitu MTANGANYIKA wala MZANZIBAR isipokuwa kuna mzawa wa Bara na Zanzibar kama ilivyo mzawa wa NewYork na Chicago wote ni Wamerekani.

Hoja ya kuiua Tanganyika ni hekima kubwa sana kwa sababu Tanganyika ingekuwa na wabunge 600 Wa Bara na Bunge la JMT. Madiwani pia mara 2 na Mawaziri, Manaibu na kadhalika. Upuuzi mtupu.

Leo hii tunalia na matumizi makubwa ya Serikali. Siku tukiunda Tanganyika, tunaongeza hesabu ya viongozi kugharamia status tu ya Utanganyika ambao ni watu wale wale aidha waitwe Watanzania au Watanganyika.

Tunagombania mkate wa urithi badala ya kuongeza ufanisi katika Uzalishaji. Itazame Zanzibar kanchi kadogo hata Mkoa wa Bagamoyo mkubwa ina Wabunge wangapi? Viongozi wa Serikali kibao kila wizara. Tatizo la kutaka tu Identity ambayo inawanufaisha viongozi sio Wananchi.

Mimi Naamini katika Pan Africanism, hii kugawana ardhi kwa makabila sijui Uzawa ni ulimbukeni mtupu wakati watu ni wale wale mnaishi pamoja na mmejamihiana..
 
Kwa hiyo Tanganyika ya miaka mitatu ambayo tayari.kulikuwa na Wazanzibar ndani ya chama na Serikali.

Ujue watu wengi hawafahamu hata harakati za Uhuru kwamba Kuna Wazanzibar walishiriki na wengine Wanachama wa TANU.

Hata historia ya hii CCM nyuma ilianza mwaka 1927 na chama cha African Association ambacho kilikuwa na matawi Mjini Zanzibar, Dar na Dodoma.
Hapa unataka kusema nini? Mzanzibari gani alikuwa kiongozi wa kisiasa katika serikali ya Tanganyika? Kama ni utumishi tu, mbona wageni walikuwemo kuanzia katika Mahakama hadi jeshini? Hata katika TANU kulikuwa na raia wa Kenya, Malawi na Uganda na walishiriki vizuri tu katika shughuli za kudai uhuru wa Tanganyika. Wakina Nyerere walijiunga na AA wakiwa Makerere. Kwa sababu hiyo sioni hii linahusiana nini na uzanzibari na utanganyika wa sasa.

Amandla...
 
Samahani kuna pahala nimesema hawakuwepo?
 
Watanganyika ni Wananchi wanaopatikana upande wa pili wa Muungano! mbona haieleweki. Upande wa kwanza wa Muungano ni upi?

Je, Mmasai anayepatikana Zanzibar huyu sio Mtanganyika! Au Mpemba anayepatikana Dar huyo sio Mzanzibar?

Na kwa tafsiri hiyo, Huyu rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ni Mzanzibar au Mtanganyika!
Shida yako nini au hiloja yako ni nini, kwani ili uitwe taifa ni lazima ijulikane ulianza lini, kama nchi ni inakidhi vigezo vya kuwa nchi basi itaitwa inchi... shida hapa ni hili swala la muungano unaoneka kuupendelea upande mmoja..... mzanzibari akiwa tanganyika anakuwa na haki zote kama mtanzania lakini mtu kutoka bara(tanganyika) akienda Zanzibar kuna haki hawezi kupata hivi ndo vitu kizazi cha sasa kinataka kuvivunja... kuwe na usawa kama nchi moja ya Tanzania.. kama haya yataendelea sijui ni lini lakini kitu kimoja hakika ni kwamba utavunjika tu..
 
Kwa hiyo nchi hii imeanza mwaka gani? Maanake kama Tanzania ni fake basi hata Zanzibar ni fake!
Nisikilize..
Ikiwa kuna muungano lazima yawepo majina ya waliungana.

Muungano huu ni kati ya Tanganyika na Zanzibar .

Hadi sasa Zanzibar iko hai
Zanzibar ina rais wake, katiba yake na na wimbo wake.
JE kuna Tanganyika?
Kuna rais na katiba yake?
 
Hapa unataka kusema nini? Mzanzibari gani alikuwa kiongozi wa kisiasa katika serikali ya Tanganyika? Kama ni utumishi tu, mbona wageni walikuwemo kuanzia katika Mahakama hadi jeshini? Hata katika TANU kulikuwa na raia wa Kenya, Malawi na Uganda na walishiriki vizuri tu katika shughuli za kudai uhuru wa Tanganyika. Wakina Nyerere walijiunga na AA wakiwa Makerere. Kwa sababu hiyo sioni hii linahusiana nini na uzanzibari na utanganyika wa sasa.

Amandla...

..kama hoja ni ukubwa wa serikali au utitiri wa viongozi basi Znz ndio ilitakiwa ifutwe na sio Tanganyika.

..hoja yako ya kupinga ukubwa wa serikali huku Tanganyika ina mashiko.

..tunaweza kuamua kuunda serikali ya Tanganyika ambayo ni ndogo kulingana na
uwezo na mahitaji yetu.
 
Shida yako nini au hiloja yako ni nini, kwani ili uitwe taifa ni lazima ijulikane ulianza lini, kama nchi ni inakidhi vigezo vya kuwa nchi basi itaitwa inchi... shida hapa ni hili swala la muungano unaoneka kuupendelea upande mmoja..... mzanzibari akiwa tanganyika anakuwa na haki zote kama mtanzania lakini mtu kutoka bara(tanganyika) akienda Zanzibar kuna haki hawezi kupata hivi ndo vitu kizazi cha sasa kinataka kuvivunja... kuwe na usawa kama nchi moja ya Tanzania.. kama haya yataendelea sijui ni lini lakini kitu kimoja hakika ni kwamba utavunjika tu..
Umeenda Zanzibar au hadith tu za simulizi. Mbona wapo Wabara wengi wanaishi na wamewekeza Zanzibar. Wapo Wangazija, wahindi, Wachina, Wazungu wewe unabakia kulia tu. Hizi Siasa za kutafuta mchawi zinawapotosha sana, nenda kawekeze Zanzibar na utaishi kama Mzanzibar. Nina jamaa zangu wanaishi Zanzibar na sijasikia wakilalamika.
 
Nisikilize..
Ikiwa kuna muungano lazima yawepo majina ya waliungana.

Muungano huu ni kati ya Tanganyika na Zanzibar .

Hadi sasa Zanzibar iko hai
Zanzibar ina rais wake, katiba yake na na wimbo wake.
JE kuna Tanganyika?
Kuna rais na katiba yake?
Kwa hiyo unacholilia ni jina? Ok tunakuita Bara umepungua nini?viiongozi? Maana ukisema Serikali maana yake unataka viongozi ilihali Serikali ya JMT inafanya kazi zile zile.

Wenzenu huko Ulaya mpaka Wahindi wanaongoza nyie mnakalia Utanganyika. Afrika kazi kugombania urithi matokeo mnakosa wote. Toka familia zetu hadi nchi ni ugonvi wa mirathi ya ardhi.

Itazame Sudan, Ethiopia, Somalia, DRC ni ujinga tu wa kugombania mali ati hizi zangu! Wako wapi? Miaka nenda ni vita!

Jengeni UMOJA WENU kuikomboa Afrika Kiuchumi sio kugombania mali. Kutwa kupigania mali, hata Mkipewa Urithi mnauza kwa Wageni mnarudi katika umaskini. itazame Kariakoo!
 
Hakuna kitu MTANGANYIKA wala MZANZIBAR isipokuwa kuna mzawa wa Bara na Zanzibar kama ilivyo mzawa wa NewYork na Chicago wote ni Wamerekani.

Hoja ya kuiua Tanganyika ni hekima kubwa sana kwa sababu Tanganyika ingekuwa na wabunge 600 Wa Bara na Bunge la JMT. Madiwani pia mara 2 na Mawaziri, Manaibu na kadhalika. Upuuzi mtupu.

Leo hii tunalia na matumizi makubwa ya Serikali. Siku tukiunda Tanganyika, tunaongeza hesabu ya viongozi kugharamia status tu ya Utanganyika ambao ni watu wale wale aidha waitwe Watanzania au Watanganyika.

Tunagombania mkate wa urithi badala ya kuongeza ufanisi katika Uzalishaji. Itazame Zanzibar kanchi kadogo hata Mkoa wa Bagamoyo mkubwa ina Wabunge wangapi? Viongozi wa Serikali kibao kila wizara. Tatizo la kutaka tu Identity ambayo inawanufaisha viongozi sio Wananchi.

Mimi Naamini katika Pan Africanism, hii kugawana ardhi kwa makabila sijui Uzawa ni ulimbukeni mtupu wakati watu ni wale wale mnaishi pamoja na mmejamihiana..
Mimi naona kama unachanganya mambo. Hakuna nchi duniani ambayo ilikuwa na mipaka ya asili. Mipaka yote ni artificial na ilibuniwa na wajanja katika juhudi za kutawala watu wenye tofauti za kijamii. Mara nyingi hii ilifanyika kwa vita, ndoa au kuwarubuni watu waliowakuta. Wazungu walipoenda Marekani walikuta kuna makabila tofauti yanaishi huko. Kwa hila, mauaji ubabe na dhulma ndio wakabuni hiyo nchi inayojulikana kama USA. Pamoja na kulazimisha hivyo, palikuwa na jaribio la kujitenga. Na mpaka sasa bado linaweza kuongezeka kama Puerto Rico itaomba kuwa jimbo la Marekani. UK hivyo hivyo, ni upanga na dhulma dhidi ya wascot na wengine ndio hiyo mipaka iliundwa na mpaka leo ni tusi kubwa kumuita mscot muingereza. Spain hivyo hivyo ( wacatalonia mpaka kesho hawataki kuitwa waspanish).

Hapa kwetu kama ilivyokuwa katika sehemu kubwa ya Africa mipaka na mgawanyiko wa continent yetu katika sehemu za utawala tunaouita nchi ulifanyika Berlin ambako hatukualikwa na hatukuwa na uwakilishi. Mkutano huo ndio uliozaa German East Africa. Zoezi la kuweka mipaka kati ya himaya ya Ujerumani, Ureno na Uingereza lilikatishwa na vita kuu ya pili. Mtu unaweza kusema wajerumani ndio waliwalazimisha watu wote waliokuwa wanaishi katika himaya yake kuanza kujitambua kama wamoja, kama subjects wa Kaiser wa Ujerumani. Juhudi hizi zilipingwa sana na wakazi wa maeneo hayo.

Baada ya mjerumani kushindwa himaya yake iliyokuwa Afrika Mashiriki ikagawiwa kwa wabelgiji na waingereza. Muingereza akaipa jina la Tanganyika eneo lake. Na watu waliokuwa wakiishi humo wakajitambua kama watanganyika. Hili jina na identity hii iliendelea hata baada ya uhuru wake mpaka siku ilipoungana na Zanzibar. Kwa sasa hamna nchi inayoitwa Tanganyika. Lakini kutokuwepo kwa nchi inayoitwa Tanganyika katika ramani hakuwanyimi watu ambao asili yao ilikuwa ni katika eneo hilo kujitambua kama Tanganyika. Hao ndio watanganyika wa sasa. Wanaofanya hivyo bado wanaamini kuwa iko siku hilo eneo litatambuliwa tena kwa Tanganyika. Hamna mtu anayeweza kuwakataza kuwa na ndoto hiyo. Vilevile kuna wale ambao jina Tanganyika halina maana kwao, na wanajitambua zaidi kama watanzania. Hao nao hiyo ni haki yao.

Amandla...
 
Umeenda Zanzibar au hadith tu za simulizi. Mbona wapo Wabara wengi wanaishi na wamewekeza Zanzibar. Wapo Wangazija, wahindi, Wachina, Wazungu wewe unabakia kulia tu. Hizi Siasa za kutafuta mchawi zinawapotosha sana, nenda kawekeze Zanzibar na utaishi kama Mzanzibar. Nina jamaa zangu wanaishi Zanzibar na sijasikia wakilalamika.
Hivi vitu vinaenda mbali na kuwekeza ndugu kwani migodi ya barrick wale ni watanzania mbona hatuna shida nao... kwa sababu wao wanajulikana ni wawekezaji.. kwa hio ni kweli hata mtu wa bara anaweeza kuwekeza zanzibar. Lakini je tuangalie kwanini waliamua kuweka sijui kuna maswala ya muungano na yasiyo ya muungano yaani kukipatikana rasilimali tanganyika hio ni ya tanzania ila kukiwa na mali zanzibar hio ni ya kwao... bunge hupitisha bajeti ya tanzania na zanzibar ikiwemo wakati wanamifumo yao ya mapato je huu ni usawa nielewe mimi sina shida na muungano ila tunahitaji kuutafsiri upya iwe nikiwa zanzibar ni kama nipo ruvuma au singida ikiwezekana zanzibar ibaki kama mkoa wa Tanzania..
 
Samahani kuna pahala nimesema hawakuwepo?
Ndio maana nimekuuliza significance ya wazanzibari kuwepo katika serikali ya Tanganyika ni nini? Kama hata raia wa nchi nyingine walikuwepo, nini kilichokuwa cha pekee kwa wanzibari kuwepo? Ndio maana nilisema sielewi ulikusudia kusema nini kwenye hili.

Amandla...
 
Kwa hiyo unacholilia ni jina? Ok tunakuita Bara umepungua nini?viiongozi? Maana ukisema Serikali maana yake unataka viongozi ilihali Serikali ya JMT inafanya kazi zile zile.

Wenzenu huko Ulaya mpaka Wahindi wanaongoza nyie mnakalia Utanganyika. Afrika kazi kugombania urithi matokeo mnakosa wote. Toka familia zetu hadi nchi ni ugonvi wa mirathi ya ardhi.

Itazame Sudan, Ethiopia, Somalia, DRC ni ujinga tu wa kugombania mali ati hizi zangu! Wako wapi? Miaka nenda ni vita!

Jengeni UMOJA WENU kuikomboa Afrika Kiuchumi sio kugombania mali. Kutwa kupigania mali, hata Mkipewa Urithi mnauza kwa Wageni mnarudi katika umaskini. itazame Kariakoo!
Ndugu Zanzibar ni zaidi ya jina, ina Rais wake
Katiba yake, na serikali yake kabisa lakini tunambiwa hili taifa liliungana na taifa lingine, tukilitafuta lile taifa waliloungana ndo hatulioni sasa tunauliza lenyewe likowapi? Naomba na wewe unisaidie kunijibu Taifa lililoungana na Zanzibar kuunda Tanzania liko wapi mbona Zanzibar ipo..
 
Tunataka Tanganyika Ile baada ya uhuru wa bendera wa Muingereza.

Tunataka Tanganyika Ile kutoka Tanga(Pwani) mpaka Nyika( Bara).

Tunaitaka Tanganyika ambayo Nyerere alikuwa Waziri mkuu kabla hajawa Raisi wa Jamhuri.

Tunaitaka Tanganyika iliyowahi kuwa na kiti UN sio hii iliyofunikwa buibui la Utanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom