Mtandao wa Wanafunzi (TSNP)watoa Tamko zito waonya pilisi kutumia nguvu

Vella

Senior Member
Nov 16, 2016
167
158
TAARIFA YA AWALI YA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA JUU YA MAANDAMANO YA WANAFUNZI HUKO BARIADI SEKONDARI.

Na,
*Joseph Brighton Malekela*
Makamu mratibu Taifa
TSNP _ Kitengo cha Sekondari

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) unapenda kuutarifu umma kuwa, palifanyika maandano ya amani ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Bariadi siku ya jumatatu kupinga taarifa ya kitendo cha mwalimu wao mkuu ambae, kwa mujibu wa maelezo yao alikuwa mtendaji kazi mzuri sana (alikuta shule ina ziro 120 akazipunguza hadi chini ya 20), kuhamishwa na kurudishwa mkuu wa shule wa zamani ambae aliididimiza shule kitaaluma.

Taarifa hiyo ilimfikia mkuu huyo wa shule kwa barua maalum siku ya *jumapili* tarehe 5/3/2017 (sio siku ya kazi) ikimjulisha kuhamishwa kwake. Kesho yake Asubuhi ikabidi awaage wanafunzi na kuwaeleza kuhamishwa kwake, Jambo lililozua maandamano.

Aidha, Maandamano hayo yalipelekea wanafunzi kufunga barabara wakipaza sauti zao kuhusu haki wanayoitafuta.

Chakushangaza, wanafunzi hao waliishia kupigwa na kudhalilishwa na jeshi la polisi kikosi cha kudhibiti vurugu FFU. Ikumbukwe kuwa hawakufanya uhalifu WOWOTE na wala hawakuwa na UWEZO wa kuharibu chochote zaidi ya kudai Haki Yao.

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Kitengo cha Sekondari, *tunalaani vikali matumizi ya nguvu kubwa isiyo ba tija wala lazima, iliyolenga kuwaziba mdomo wapigania haki hao kwa kufyatua mabomu ya machozi na kuwanyanyasa wanafunzi hao kisha kuwakamata na kuwasweka lumande.

Jeshi la polisi Kitengo cha kudhibiti vurugu lilipaswa kutoa ulinzi ili wanapodai HAKI wasije kudhurika, badala yake wao wakawa maadui wa kuwadhuru Watu wasio na nia mbaya. Wapo wanafunzi waliojeruhiwa na wengine walizimia siku hiyo.

Hata hivyo, Mtandao kupitia mratibu wa TSNP mkoa wa Simiyu unaendelea kufanya tathmini ya mwisho kabla ya kutoa msimo wa Taasisi na tamko rasmi.

Aidha, tunatoa pole kwa wanafunzi hao waliokumbana na adha hiyo Pale walipokuwa wakidai HAKI ya kubakishiwa mkuu wa shule kwa maslahi yao na wadogo zao, mkuu ambae HATA MKUU WA WILAYA ALIKIRI KUWA, *AMEHAMISHWA KIMAKOSA NA UTARATIBU HAUKUFUATWA*.

Utaratibu utakapokamilika, TSNP tutatoa msimamo. Kwasasa yatosha kusema, KILICHOFANYIKA HAKIKUBALIKI NA KIMEKIUKA KATIBA INAYOTOA
*Haki na Uhuru wa kujieleza bila kuvunja sheria*


Imetolewa na:

Joseph Brighton Malekela
Mratibu msaidizi_Taifa
TSNP Kitengo cha Sekondari
Baruapepe: josephmalekela34@gmail.com
 
Inatupasa sote kupasa sauti zetu maana huwezi jua siku ya kuraruliwa binti au wavulana wetu?
 
poleni sana jamani. Tatizo kubwa la nchi yetu ni UJINGA
Wanaotoa amri ni wajinga na watekelezaji pia.
Halafu wote wana roho mbaya na hawajiamini.
Wana maono finyu na hawana weledi kabisa.
Kifupi ni HOPELESS na nafasi hizo walizopewa haziwafai.
 
Back
Top Bottom