Huduma mbovu za Mtandao wa TTCL: Malalamiko ya wananchi

Godfather of Harlem

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,494
3,786
Sio siri ngoja niende kwenya mada moja kwa moja.

Huu mtandao una matatizo mengi sana kama yafuatayo:

1. Huduma ya T PESA
Aisee huu mtandao kama utatuma hela siku ya Ijumaa usiku ghafla litokee tatizo wallah utakuja kuhudumiwa siku ya Jumatatu.

Hili tatuzo limenipata juzi hapa Ijumaa tarehe 7 yaani nilitamani kulia wallah.

2. Vifurushi
Hawa majamaa ukitaka uende nao sawa kwenye masuala ya MBs nakushauri tafuta kitambulisho cha chuo.

Aisee yaani GB 5 kwa Tsh 5000 mwezi mzima.

3. Vocha
Asikwambie mtu, TTCL hawana vocha aisee. Jana nimeenda pale Makao Makuu niliulizia vocha ya 500 hakuna wanasema zipo za 1,000.

Aisee ukienda kuulizia madukani yaani muuzaji anaweza akashangaa maana hiyo vocha ya TTCL ndiyo kwanza anaisikia kwako.

Kilichonipata jana
Nilijiapiza nikaonane na Afisa Masoko pale Makao Makuu pale Posta ili nimshauri kitu kimoja tu. Yaani nikafika mapokezi nikaonane na bwana Kindamba lakini nikazuiliwa.

Yule mama wa mapokezi aliongea sana mpaka wakati naondoka nimeinamishwa kichwa chini kwa masikitiko.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom