Mtandao wa Tigo ni kero hii sasa

Nuraty J

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,729
3,829
Juzi nimenunua vocha ya efu mbili ya tigo nikaweka huku nikiwa nimezima data, baada ya kuweka vocha nikajiunga kifurushi Cha saizi yako, nikarudishiwa meseji kuwa umefanikiwa kujiunga ,,
Basi baada Ya hapo nikawasha data kwakujua nishajiunga na meseji isharudi kama siku zote, nikawa naperuzi jf na mitandao mingine,
sasa baadae nataka kumpigia mtu gafla inaingia meseji sina salio, wakati nilijiunga nimepata MB na dakika kibao Kwa masaa 24 ,kupiga namba yao *102*00# kweli najibiwa sina Salio wala mb,
Nikachanganyikiwa, ikabidi niwapigie tigo customer care,
nawaambia jamani inakuwaje nimeweka vocha ya efu mbili na nikajiunga, na meseji mkanitumia kuwa nimefanikiwa kujiunga, saizi Nataka kumpigia mtu naambiwa sina Salio?
majibu yao eti ulivyoweka salio na kujiunga ulikuwa ujafanikiwa kujiunga, nikawauliza mbona meseji ilirudi kuwa nimefanikiwa kujiunga ,,wakanijibu muda mwingine meseji inaweza ikarudi lakini ukawa ujafanikiwa,,

Kwakwel hii mitandao mingine ni kero na yakipuuzi
 
Hamia voda huku mambo ni mswano, BONGE LA BANDO ni buku yako unajipatia GB 1 ya kifurushi cha data mbali na hilo voda wanatoa ofa ya dakika na mbs za bure za kutumia mpaka mwezi mzima. Voda kumenoga!
Screenshot_20191001-162718~2.jpeg
 
Hamia voda huku mambo ni mswano, BONGE LA BANDO ni buku yako unajipatia GB 1 ya kifurushi cha data mbali na hilo voda wanatoa ofa ya dakika na mbs za bure za kutumia mpaka mwezi mzima. Voda kumenoga! View attachment 1220729
hao voda mbs zao zinalika kama moto wa mabua, nilijiunga ya 2500 ,wala haina haja kusimulia, laini yao natumia Kwa M-pesa tu
 
Back
Top Bottom