Mtandao wa tigo kimbilio la matapeli hasa madalali wa nyumba Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtandao wa tigo kimbilio la matapeli hasa madalali wa nyumba Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inanambo, Jun 26, 2011.

 1. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  NASHINDWA KUELEWA NCHI HII SHERIA ZINAKWENDAJE. MWAKA JANA TULIKIMBIZWA MCHAKAMCHAKA WA KUSAJILI LINE ZA SIMU LA SIVYO HAKUNA MAWASILIANO. NIA ILIKUWA KUZUIA MATUMIZI MABAYA YA SIMU IKIWEMO UHALIFU KAMA VILE MATUSI NA UTAPELI. MTEJA ALITAKIWA AWE NA KITAMBLISHO HALALI NA AENDE PEKE YAKE(KIMWiLI) AU PHYSICALLY KUJISAJILI. WENGI TULIFANYA HIVYO NA MITANDAO YA SIMU KAMA VODA, TIGO, ZAIN NA ZANTEL WAKAKAGUA KWELI UHALALI WA LINE ZA WATEJA. BILA KUJISAJILI WALIKUWA HAWAKUPI MAWASILIANO. LEO HII MTANDAO WA TIGO NI TOFAAUTI KABISA NA WITO HUO. UNACHUKUA LINE KWENYE VIBANDA VYAO BILA KUJISALI WALA KITAMBULISHO UNATIA KWENYE SIMU YAKO UNAPATA UNANUNUA VOCHA UNALONGA KAMA KAWAIDA. UKITAKA KUMTAPELI MTU UNAWASILANA NAYE, UKIMALIZA UNATUPA LINE YAKO UNAENDELEA NA UTAPELI MWEINGINE KWA LINE NYINGINE KWA STAILI HIYO YA KUTOSAJILWA NA HAKUNA ANAYEJALI. WEWE NUNUA LINE WEKA VOCHA WAFANYA BIASHARA HAWA WA TIGO WAPATE KIJINADI WANA IDADI KUBWA YA WATEJA AMBAO HATA MAJINA HAWAJUI. UKISHAIBIWA UKIENDA TIGO KUTAFUTA INFO ZA TAPELI WAKO WANAKUTOLEA NJE WAKIDAI UJE NA POLISI WANALINDA SIRI ZA WATEJA KAMA ZILIVYO ACCOUNT ZA BENKI! UKIENDA POLISI KUTOA HIYO TAARIFA HUCHUKUA MUDA NA HUWA HAILEWEKI KWA SABABU HAWANA USAJILI WA HAO WATEJA WAO. IFIKE MAHALI SASA TIGO WALIPE FIDIA WANAOLALAMIKA KUIBIWA NA WATEJA WALIOTUMIA MTANDAO WAO KWA SABABU WANAWALINDA. MAMLAKA YA MAWASILIANO PSE MJARIBU KUZUIA UHURU WA MTU KUMILIKI LINE ZAIDI YA MOJA YA MTANDAO MMOJA. NIKISEMA HAYA YOTE MIE NIMELIZWA NA WATEJA WA TIGO AMBAO NILIAMINI USAJILI UTANISAIDIA KUMBE SIKUJUA NAISHI NCHI YA ULIMWENGU WA TATU AMBAYO LEO TUNAKUBALIANA HIVI KESHO TUNARUKANA HATUNA MSAADA. WAKATI MWINGINE HAWA WASAJILI SIMU AU WAUZA LINE HATA KUANDIKA NA KUSOMA HAWAJUI VIZURI. KUKAGUA KITAMBULISHO HAWAWEZI HATA UKIJIITA NYANYA BIN KABEJI WAO HAWAJALI. WANAJAMII NISAIDIENI NIFANYE NINI IKIWA NIMEIBIWA KWA NJIA YA SIMU NIKITUMAINI KUMBUKUMBU ZA USAJILI WA MTEJA AMBAZO HAZIPO? NAWEZA KUWASHTAKI TIGO WAPI MIE JAMANI ILI WAWE SERIOUS NA HUDUMA YAO?
   
 2. d

  dropingcoco Senior Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo imekula kwako, kwa nini uibiwe kif a l a f a l a kwenye simu, sio kila mtu umwamini,siku nyingine uwe mjanja
   
 3. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  pole sana mkuu....nimecheka sana jina la nyanya bin kabeji...
   
 4. m

  mkaa Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah!kweli makubwa.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Du!!mzee unakandamiza sana.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Naona wewe ndo umechemka hapo, wewe ulitaka data za watu ziwe zinagawiwa kiholela kwa kila anayeomba? Fungua kesi, ukiwa na court order Tigo watakupa data.

  Umeibiwa kivipi? toa maelezo ueleweke.
   
 7. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  acha aibiwe kama ni mtandao mbaya hama, na uko utakapokwenda ukiibiwa hama nchi Tanzania zaidi ya uijuavyo..... g n9t,
   
Loading...