Mtandao wa 'Sema na Rais' kule Zanzibar mbona kuna jambo halikuingizwa?

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Habari za wakati huu watu wa jamvi hili.

Mimi ni miongoni mwa waliofurahishwa sana na juhudi za Dr. Mwinyi kule zanzibar kwa kuweza vyema kuwaunganisha wazanzibari kwa kuunda umoja wa Kitaifa chini ya Almarhum Maalim Seif Sharif Hamad (Allah Amrehemu).

Jambo jengine zuri zaidi Dr. Mwinyi aliloanzisha hivi karibuni ni huu mtandao wa "Sema na Rais" kwamba sasa wananchi wanaweza peleka malalamiko yao mbali mbali na moja kwa moja kwa rais kupita Taasisi mbali mbali mgawanyo wake.

Lakini jambo ambalo linanipa mashaka sana kuhusu uwazi wake katika zile category zote sijaona mtu anaweza peleka malalamiko yahusuyo Tume ya Uchaguzi ambapo eneo hili kwa uzoefu wangu watu huwa na malalamiko mengi sana.

Naomba kuwasilisha.
 
"Sema na Rais" inahusu changamoto za wanachi kwenye maisha yao ya kilasiku.

Mambo ya tume ya uchaguzi nenda mahakamani au kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar.
 
Hilo la tume huru ya uchaguzi sahau kabisa.mwinyi ameingia madarakani kwa kupitia tume hiyo hiyo.hawezi kuibadiri@ 5 tena
 
Katika sehemu ambayo inawaumiza wanasiasa wapendao madaraka ni issue ya tume ya uchaguzi, labda kiongozi mwenye hofu ya Mungu kwelikweli ndiye anaweza kucheza nayo, vinginevyo hakuna kitu.
 
Mimi sitoweza kamwe kumsifu Mwinyi mpaka atakapoweka tume huru, hicho ndicho kipimo chake kikuu mengine yote ni porojo tu
 
Back
Top Bottom