Mtandao wa maendeleo ya wanawake kuwanusuru vijana na dawa za kulevya

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
Mtandao wa maendeleo ya wanawake nchini kupitia vikundi vya ujasiliamali(INUKA)umezindua mpango wa kuwapatia elimu vijana,wahudumu wa bar (bar medy)jinsi ya kujikinga na matumizi ya madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa INUKA,David Msuya mpango huo una lenga kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya vijana na jamii kwa ujumla na kwamba ni mwendelezo wa mtandao huo kuhakikisha kuwa unawawezesha vijana kujikinga na matumizi ya madawa ya kulevya.

Aidha mpango huo unaunga mkono sera ya serikali ya kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana ili kupunguza katizo la maisha linalosababishwa na utumiaji wa madawa hayo.

Mpango huu pamoja na kuzinduliwa kwa kishindo katika wilaya ya Same mkoa wa kilimanjaro,pia utaelekezwa kwenye miji mbalimbali hapa nchini na wameiomba jamii iunge mkono ili kunusuru maisha ya vijana ambao taifa bado linawahitaji.
 
Back
Top Bottom