whatsapp online
Member
- Jan 17, 2017
- 86
- 95
Mie ni mteja ninayetumia zaidi ya mtandao mmoja wa simu, na huwa kila tangazo la mtandao la wowote linapotoka kwenye vyombo vya habari huwa nalifanyia kazi kama nahisi lina tija kwangu. Siku za hivi karibuni nikakutana na tangazo la TIMIZA mkopo. Sina hamu nao maana nilikopa 15,000/= nikakawia kulipa. ikawa kila baada ya siku chache penalty. Kwa sababu ya uzoefu wa kukopa kwenye mitandao ukilinganisha na mpawa (sina ubia na mtandao wowote) utagundua voda wanasaidia na sio kuwaumiza wateja wenye shida kama wanavyofanya airtel. hata ukihitaji kuwasiliana na wahudumu wa airtel kwa ajili ya matatizo mengine sio rahisi kama ilivyo wa mitandao mingine. Na hata ukiahatisha kuongea nao hawana lugha nzuri kama wengine. Naongea yaliyonitokea mie na sio kusikia kwa mtu.