Mtandao wa Airtel hili halina tofauti na uhujumu uchumi

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
794
500
Napenda kuwapongeza kwa huduma mlizonazizito kupitia mtandao wenu. Lakini ni muda sasa takribani wiki 3 huku Serengeti tumekuwa tukiweka bundle lakini ni Kama zinapotea bure maana mtandao uko chini na huwezi mpigia simu mtu.

Sasa naomba either mtupe wateja wenu nini kinajiri au mrekebishe mtandao wenu ili msitupotezee pesa zetu na kuturudisha kwenye uchumi wa chini wakati tupo kwenye uchumi wa kati.

Maana hii naiona ni Kama ni kutuhujumu watumiaji wa mtandao wenu. Mathalani sasa nalazimika kutumia laini nyingine kufanya mawasiliano na kutumia gharama kubwa.
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
8,612
2,000
Huku Arusha ni kero sana huu mtandao.
Unaweka MB alafu ukiwasha data inawaka nusu dakika inazima, inaweka tena na kuzima 😀
Saa nyingine inasoma 4g na inaonyesha iko vizuri ila Ukiingia mtandaoni haieleweki utadhani ni 2g
Chaajabu MB zikiisha network inakaa poa. Alafu unaweza kuweka bando hata hujalitumia lakini unashangaa umejulishwa bando limeisha..... Ukiwapigia ndio hivo hawapokei!
Ngoja nijaribu kusajili halotel nione
 

Kibua

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
285
1,000
Cheap is expensive bandugu.! Hamieni voda japo ni gharama ila huo upupu haupo kabisa
 

masagati

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
469
500
Mimi nime nunua kifurushi cha muda wa maongezi cha mwezi tsh 10,000/= wamekata pesa ila dakika hawaja nipa ukipiga simu wanakujibu tunalishughulikia mpka sasa ni mwezi mmoja hawaja nipa huduma na pesa hawaja ludisha.
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,796
2,000
Kuna shida mahali na wameshindwa kuitatua Rufiji mtandao huu,hii ni week sasa watu simu hazipatikani.
Nimeamua kuifunga line natumia line ya voda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom