Mtandao umekufa rasmi, kazi ni kusafisha matokeo yake.

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,312
24,171
Kwa wafuatiliaji wa kisiasa mtakumbuka jinsi mtandao ulioundwa na Kikwete na Lowasa ulivyotikisa siasa za Tanzania toka miaka ya 1990's.
Hatimaye mtandao huu ulifanikiwa kuingia madarakani mwaka 2005 na wakuu wa mtandao huo wakagawana vyeo kama ile waingereza wanaita "spoils of war" , yaani matunda ya kugawana madaraka yaliyotekwa.

Wakati zkikwete aliwasogeza ndugu jamaa na marafiki zake madarakani, Lowasa kwa gia kubwa aliingiza kina Ole wengi kwenye utawala wa mikoa na mashirika ya umma.

Lakini utawala wa tamaa tu na si kutumikia wananchi ulianza kuleta matokeo yasiyo tarajiwa.
Chama CCM kikakosa malengo baada ya vichwa kama Mangula kutimuliwa au kuondoka.
Mawaziri wakawa wengi na walikuwa wanabadilishwa kama circus.
Na kwa vile tamaa haikuishia kutawala tu kwa wana mtandao, tofauti kubwa, na zinazotokana na tamaa ziliibuka kati ya waasisi wa mtandao, yaani Kikwete na Lowassa.

Tofauti hizo na hatimaye ugomvi uliokuwa ukiendeshwa kama gemu la chess, uliishia kuwamaliza wote wawili katika kimsimamo wa kuuendeleza mtandao.

Watanzania lazima tumshukuru Mungu, kwamba ni tamaa ya madaraka na mali ndio imewamaliza wana mtandao.

Magufuli amefanya vema kwa kuanza kuibua madudu ya kutisha ya uongozi ambao ulikuwa hautawali bali unajinufaisha na utendaji wa serikali.

Ni vema utafiti wa kina ujafanywa na wataalam wa sayansi ya jamii , na katika kipindi kifupi, ili madhara mahsusi yatambuliwe, na hatua za kurekebisha zichukuliwe.

Kitu kinachoonekana dhahiri ni kuubinafsisha ukusanyaji wa kodi, na kodi hizo kuingia mifukoni mwa watu binafsi badala ya serikali ili kutumikia wananchi.
 
Mkapa ana kazi ya kuwaeleza watanzania ni nini kilitokea pale Dodoma mwaka 2005.
Yale yalikuwa mapinduzi, kikundi cha mtandao kushika madaraka kwa njia za hila.
Matokeo yake tumeyaona na si mazuri sana.
Mbaya zaidi CCM imelea siasa za vikundi, yaani mitandao ndani ya chama, Lowassa naye aliunda mtandao wake ndani ha chama.

Tunashukuru kuwa huu mtandao unafikia mwisho wake na wazee kina Mkapa, Mwinyi na wengine wanakazi ya kuondoa huu UBAGUZI WA KIMITANDAO.
Maana ndani ya ubaguzi wa kimtandao kuna SISI NA WAO!
 
Tungoje,, maana sina uhakika kama magufuli atawaacha wanamtandao kwenye serikali yake.

Kama atawaacha akina Makamba na Mwigulu nitajua nguvu ya kutengeneza mitandao ndani ya chama imekwisha.

Tungoje tuone..
 
Mtandao ni janga la kitaifa na kuwaacha madarakani katika nafasi yoyote ile ni kuendeleza ubaguzi kama mtoa posti mmoja hapo juu alivyoeleza.

Kule China , mtandao kama huu wetu wa the Gang of Four uliisha vibaya sana kwa kuwekwa kizuzini , kupelekwa mahakamani na hatimaye kufungwa jela.
Katika hilo Gang of Four alikuwemo mke wa Mao Tse Tung, kiongozi wa Chama cha kikomunsti cha China.
 
umenena vema sana. unaijua ccm. kuna vijana waliokaririshwa mfumo ndani ya ccm ulioasisiwa na wanamtandao,natamani wangepitia uzi huu ili waelewe haya uliyoyaeleza kwa ufasaha kabisa. manyumbu wakiujua ukweli huu watawekwa huru na kutoka katika unyumbu ambao umewavaa.
 
kwenye huu mtandao wengine hawakujua kuwa yule mswahili lengo lake lilikuwa kuwatumia awe rais.
inafahamika wazi kuwa alikuwa maskini asingeweza kupambana na wenye hela.
wenzake wakamuamini wakitegemea atakuja kuwabeba.
lakini ukweli ni kwamba wametufirisi sana hawa jamaa.!!!
kodi zetu walikuwa wanajaza kwenye k za wanawake tu.
 
Acha hasira mkuu, jadili kwa mapana!
 
Kwa jinsi JK alivyoingia madarakani kwa mipango mipango, CCM ina mengi ya kujifunza nmna ya kuondoa makundi ya kibaguzi ndani ya chama.

Nasema hivyo kwa vile vikundi hivi motivation yao ni personal material gain, tofauti na aspiration za kisiasa za wanachama.
Wachambuzi ndani ya chama wakae chini na watupe majibu walikosea wapi, na wajue kuwa tatizo si JK kuupata urais, lakini tatizo ni kwa nini CCM iliruhusu mtandao wenye malengo hasiyo ya kichama kuteka nchi.
 
Mkapa ana kazi ya kuwaeleza watanzania ni nini kilitokea pale Dodoma mwaka 2005.
Yale yalikuwa mapinduzi, kikundi cha mtandao kushika madaraka kwa njia za hila.
Matokeo yake tumeyaona na si mazuri sana.
Mbaya zaidi CCM imelea siasa za vikundi, yaani mitandao ndani ya chama, Lowassa naye aliunda mtandao wake ndani ha chama. Tunashukuru kuwa huu mtandao unafikia mwisho wake na wazee kina Mkapa, Mwinyi na wengine wanakazi ya kuondoa huu UBAGUZI WA KIMITANDAO.
Maana ndani ya ubaguzi wa kimtandao kuna SISI NA WAO!
Mkuu bado unanishangaza! Ni nini kimetokea mpaka umeongoka kama yule Paulo wa kwenye biblia! Wewe ulikuwa unautetea sanab utawala wa Kikwete!
Back to the topic: Alichotakiwa kufanya Mkapa ule mwaka 2005 ni kama alivyofanya Kikwete 2015. Angetumia njia za kijasusi kuwazima kundi la mtandao! Mimi ni mmoja wa wengi wanaoshangaa ilikuwaje Kikwete aingie madarakani kwa kutumia fedha kama ilivyotokea ule mwaka!
 
Naamini Magufuli atairudisha ccm mahala pake, mitandao imeshakatwa, tumuombee maana changamoto zipo
 
Kwa jinsi JK alivyoingia madarakani kwa mipango mipango, CCM ina mengi ya kujifunza nmna ya kuondoa makundi ya kibaguzi ndani ya chama.

Nasema hivyo kwa vile vikundi hivi motivation yao ni personal material gain, tofauti na aspiration za kisiasa za wanachama.
Wachambuzi ndani ya chama wakae chini na watupe majibu walikosea wapi, na wajue kuwa tatizo si JK kuupata urais, lakini tatizo ni kwa nini CCM iliruhusu mtandao wenye malengo hasiyo ya kichama kuteka nchi.
Umenena kweli.
Mtandao wa JK and company kuiteka CCM ile ilikuwa mapinduzi bila kumwaga damu.
Ilikuwaje CCM kutekwa kirahisi namna vile?
 
Mkuu bado unanishangaza! Ni nini kimetokea mpaka umeongoka kama yule Paulo wa kwenye biblia! Wewe ulikuwa unautetea sanab utawala wa Kikwete!
Back to the topic: Alichotakiwa kufanya Mkapa ule mwaka 2005 ni kama alivyofanya Kikwete 2015. Angetumia njia za kijasusi kuwazima kundi la mtandao! Mimi ni mmoja wa wengi wanaoshangaa ilikuwaje Kikwete aingie madarakani kwa kutumia fedha kama ilivyotokea ule mwaka!
Mkuu lazima tuelewe kitu kimoja.
Siasa si mtulinga kama ambavyo vijana wengi wangependa iwe hivyo.
Siasa ni chess ambalo inabidi utoe kete iliwe ili baadaye uendelee na mchezo.

Na bado katika vyama vyote vya kisiasa, sioni mbadala wa CCM. CCM huwezi kuiweka mfukoni kwa muda wote.
Ndio maana Lowassa ameshindwa kuiweka mfukoni licha ya pesa yake ndefu.

Hata mwenyekiti wake JK ameshindwa kulazimishia Membe kuupata urais kwa sababu CCM. ina kautaratibu wa kioganaizesheni ambao unaridhisha matakwa ya wananchi .

Katika mada hii mshangao wa wengi ni jinsi fedha ghilba na kaubaguzi ka kimtandao ilivyoweza kufanikiwa kuiteka CCM mwaka 2005.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, haya makosa tunaiomba CCM isiyarudie tena mama inataka kuwa chama cha wananchi.
La sivyo kuna watu tayari hadi sasa ambao wataamua kujenga mtandao wa kuiteka tena CCM mwaka 2020.
Na tunajua sote fedha itakayotumika itatoka wapi-kwa mafisadi.
 
Acha hasira mkuu, jadili kwa mapana!

Kama amesema ukweli ni hasira? watu wanawapa madaraka wanawake kisa kalala naye jana au ni hawala wa Mwanae.
ukiona mrembo mpitishe jirani basi kesho yake Mkuu wa wilaya, alafu sisi tunadanganya gander!!! mbona wenye sura ngumu hawakupewa???
 
Mkuu hayo ndo matokeo mabaya ambayo mtia mada amegusia.
Watu wanatafuta uongozi kukidhi tamaa zao!

Mtu anayeutaka uongozi ili akidhi tamaa zake au anufaike kibinafsi, huyo si mwana CCM wa ukweli, ni kama mamluki.
Na hapo ndo utata,bua kama una kiongozi au la!
 
Mkuu lazima tuelewe kitu kimoja.
Siasa si mtulinga kama ambavyo vijana wengi wangependa iwe hivyo.
Siasa ni chess ambalo inabidi utoe kete iliwe ili baadaye uendelee na mchezo.

Na bado katika vyama vyote vya kisiasa, sioni mbadala wa CCM. CCM huwezi kuiweka mfukoni kwa muda wote.
Ndio maana Lowassa ameshindwa kuiweka mfukoni licha ya pesa yake ndefu.

Hata mwenyekiti wake JK ameshindwa kulazimishia Membe kuupata urais kwa sababu CCM. ina kautaratibu wa kioganaizesheni ambao unaridhisha matakwa ya wananchi .

Katika mada hii mshangao wa wengi ni jinsi fedha ghilba na kaubaguzi ka kimtandao ilivyoweza kufanikiwa kuiteka CCM mwaka 2005.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, haya makosa tunaiomba CCM isiyarudie tena mama inataka kuwa chama cha wananchi.
La sivyo kuna watu tayari hadi sasa ambao wataamua kujenga mtandao wa kuiteka tena CCM mwaka 2020.
Na tunajua sote fedha itakayotumika itatoka wapi-kwa mafisadi.

Lakini kwa uelewa wangu na kwa watu mliopata elimu kwa shida kama wewe sioni kama kuna tija ya kuisifia ccm.
na kauli ya kusema hakuna mbadala wa ccm ni kama vile mlisha wahi kuwapa wapinzani alafu hawakufanya vizuri.
Mimi naona kuwa imefika muda wa ccm kupumuzika kwa maana baada ya miaka 54 bado tumekuwa omba omba. Cha kukusaidia katika Uchaguzi wa mwaka huu Mkwere amefanya hila nyinyi ikiwa ni pamoja na kunyang'anya matokeo ili kuirudisha ccm madarakani huku akitegemea kulindwa wizi wake lakini naona inatokea tofauti kidogo.
 
Mkuu hayo ndo matokeo mabaya ambayo mtia mada amegusia.
Watu wanatafuta uongozi kukidhi tamaa zao!

Mtu anayeutaka uongozi ili akidhi tamaa zake au anufaike kibinafsi, huyo si mwana CCM wa ukweli, ni kama mamluki.
Na hapo ndo utata,bua kama una kiongozi au la!

Tuwajuaje watu hao? ikiwa tu baba wa taifa alituhubiria kuwa Mkapa ni mtu safi sana lakini baada ya muda mfupi akajilimbikizia mali????
Cha kujiuliza zaidi hata mali za umma akazifanya zake, kweli jamani? naye bila aibu akatuletea Kikwete na kumsifia.
Hivi kuna mtu alijua kuwa Mkwere anaweza kuwa mbaya kiasi hiki?
ukitaka ccm ife inabidi ukae pembeni kama Magufuli itakufa yenyewe maana majizi yote yataichukia itakosa pesa za kampeni.
 
Tujijadili mada kama hizi , munkari haufai hata kidogo.
Tusisahau kuwa Magufuli ni zao a CCM.
 
Lakini kwa uelewa wangu na kwa watu mliopata elimu kwa shida kama wewe sioni kama kuna tija ya kuisifia ccm.
na kauli ya kusema hakuna mbadala wa ccm ni kama vile mlisha wahi kuwapa wapinzani alafu hawakufanya vizuri.
Mimi naona kuwa imefika muda wa ccm kupumuzika kwa maana baada ya miaka 54 bado tumekuwa omba omba. Cha kukusaidia katika Uchaguzi wa mwaka huu Mkwere amefanya hila nyinyi ikiwa ni pamoja na kunyang'anya matokeo ili kuirudisha ccm madarakani huku akitegemea kulindwa wizi wake lakini naona inatokea tofauti kidogo.
Kuendesha nchi siyo pata potea.
Kama chama kinaweza kununuliwa na mtu mmoja tena overnight, hakina hata chembe ya uadilifu unotakiwa kuitwa chama.
Kwa classification ya chama cha siasa , hicho si chama bali mradi wa watu.
 
Kwa jinsi JK alivyoingia madarakani kwa mipango mipango, CCM ina mengi ya kujifunza nmna ya kuondoa makundi ya kibaguzi ndani ya chama.

Nasema hivyo kwa vile vikundi hivi motivation yao ni personal material gain, tofauti na aspiration za kisiasa za wanachama.
Wachambuzi ndani ya chama wakae chini na watupe majibu walikosea wapi, na wajue kuwa tatizo si JK kuupata urais, lakini tatizo ni kwa nini CCM iliruhusu mtandao wenye malengo hasiyo ya kichama kuteka nchi.

Well said Lole Gwakisa
Wengine tunasubiria kwa hamu kuifahamu hii syndicate....natumai ipo siku kuna an individual kutoka within(kwangu mimi JK ndiye perfect) aje atuandikie kitabu ili tupate an insight toka early 1990's throughout 2015.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom