Mtandao gani wa Simu za mkononi unafikisha huduma ya internet hadi vijinini?

sawani

Member
Feb 7, 2010
9
7
Wadau natumaini mu wazima nyote. Tafadhali ninaomba msaada kupata taarifa. Ninataunda mitambo ya shughuli fulani zitakazofanyika maendeo ya vijijini. Nitahitaji kukusanya taarifa kutoka kwenye mitambo hiyo. Wazo la kwanza lilikuwa kutumia GPRS na kukusanya data kwenye server. Lakini nimepata taarifa kwa ndugu mmoja kuwa sio minara yote ya simu ina mifumo ya GPRS. Kwa maana hiyo nitalazimika kutumia GSM kukusanya data kwa kupitia SMS.

SMS ni gharama sana kulinganisha na GPRS. Hivyo ninafikiri kuifanya mitambo yangu kutumia njia zote mbili na kui-tune kufuatana na mazingira nitakayo iweka.

Kufuatana na hilo, kujua ni mtandao gani nitaweza kuutumia utakaoniwezesha kupunguza idadi ya mitambo itayohitaji kuwa tuned kwa matumizi ya SMS. Yaani ni mtandao upi umefunga minara yenye mifumo ya GPRS hadi katika maeneo ya mbali na mijini. Njia mojawapo rahisi ya kufahamu ni kuwa na uwezo wa kupata mawasiliano ya internet kwa kutumia mtandao huo hata ukiwa maeneo ya mbali na miji. Ni Airtel, Voda, Tigo...??

Natumaini nimejitahidi kujieleza. Lakini pia ninaweza kujibu swali kama maelezo haya hayatoshi kueleza ninachouliza?

Natanguliza shukrani
 
yote utapata gprs
Maeneo maarufu kidogo utapata Edge
Vitovu potential utapata 3G..
 
Back
Top Bottom