Mtanda; Kamati ya mitihani na Bodi inayoandaa mitihani ivunjwe

habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
456
Akichangia hivi sasa bungeni, mbunge wa jimbo la mchinga SAID MTANDA amesema kabla ya bajeti ya wizara ya elimu kupita, kwanza Bodi inayoshughulika na kuandaa mitihani ivunjwe na pia kamati ya mitihani inayopanga madaraja ya ufaulu ivunjwe, kwani ndio chanzo hasa cha matokeo mabaya na kiwango kibaya cha ubora wa wanafunzi hapa nchini.
Ameongea kwa uchungu kwamba wizara ya elimu inapaswa kufumuliwa OVERWHOLE ili iwe na tija kwa elimu ya tanzania
 
Huu ndio ubunge wenye kujali maslahi ya nchi na si chama. Mtanda anampa changamoto Kawambwa.
 
Huyu naye ni wale wale, He is firing around the bush! Kwanini usimwambie Kawambwa na Mulugo WAJIUZURU kwasababu wao kama watendaji wakuu wa WIZARA ndiyo waliobariki hiyo system mpya ya GRADING!

Ukitaka kumua nyani usimwangalie USONI, anawarukiwa watu ambao hawapo BUNGENI wakati wahusika wakuu ni hao wabunge wenzake kawambwa na Mulugo!

I hate hypocisy of CCM Mps
 
Wawajibishwe kwani wamekosea nini? Waalimu hawakulipwa vizuri kwa hiyo hawakufundisha vizuri, vifaa vya kufundishia hakuna, walimu wa kutosha hakuna, vyuo vinavyoandaa waalimu vimechoka, kat ya wahadhiri 3,700 waliopo nchini wenye PhD ni kama 670 tu. Unategemea nini? Kosa la NECTA ni lipi hasa???
 
Ameongea kwa uchungu kwamba wizara ya elimu inapaswa kufumuliwa OVERWHOLE ili iwe na tija kwa elimu ya tanzania

Mkuu na mimi nimemkubali japo ni gamba lakini amesema ukweli. Wizara lazima ifumuliwe kuanzia na Waziri mwanyewe na Mzee wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kisha vimeo vingine vyote vifuate. Kawambwa ameshindwa kuongoza na hana maamuzi hata kwa wale wanaoharibu hawezi kufanya chochote. Sasa huyu Kawa Mbwa ni sawa na Mbwa asiye na meno hafai hata kuwa kiongozi wa nyumba kumi
 
Hajitambui,
Baada ya kuanza kufuatilia watoto waanfundishwa nini huko madarasani anakomaa na wasaishaji.

Mjanja mjanja tu huyu jamaa je yeye kafanya nini katika jimbo lake kuinua elimu. Wenzanke masasi wanachuku wanafunzi wa mafunzo kila mwaka kuziba pengo wakati yeye ata bajeti katika wilaya yake hakuna!

Tuache unafiki!
 
Back
Top Bottom