Mtanange wa Klabu Bingwa Afrika: Al Ahly 5 vs Simba SC 0

Hawa jamaa tuko tofauti nao labisa. Ni mbingu na ardhi.
Haiwezekani first eleven ikafungwa na bandari ya kenya alafu tuote kuifunga al ahly. Hata walija hapa kwetu watatupiga bakora hii hii.
Tukubali tu kiwa simba tunacheza sana mpira magazetini. Kina mkude tunawaremba sana. Hiki kikosi ni Okwi pekee ndiye wa kumkubali. Kina chama watazitesa ndanda.
 
Kwani jamani timu zetu zikitokaga nje huwa zinakuaje wanalishwa nini huko? Huwa sielewagi kabisa
 
Kiuhalisia Tanzania Bado uwezo wetu upo chini Sanaa,, lakin mashibiki wa Simba au yang ukiwaambia ukweli hawaelewi,, itachukua mda mrefu sana kuweza kufika level za kuleta ushindani,,ujanja ujanja, siasa ujuaji usio Na maana,ushabiki wa kipumbavu ambao hauna tija hautatusaidia mpira sio maneno tuu,,,
 
Mbona vyura ndio mnashadadia sana huu uzi? Kwani nyie mnacheza lini?

Au bado mko dimbwini pale jangwani mnaogelea matopeni?
huyo anaye kupiga kama nyau yanga tulimkimbiza mwanzo mwisho kama si ujinga wa bahanuzi tungemtoa kwenye mashindano

bora yanga sio nyau
 
Leo nimekumbuka wimbo wa darasa la Kwanza, usemao, napenda kuhesabu namba moja mbili Tatu vidole vya miguu yangu mimi jumla yake kumi,huku Congo 5 na huku misri tano jumla yake kumi, Mbwa wa chini aka underdog kwa nini mteseke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom