Mtambo wa kuendesha mashine ya kunyolea bila uwepo wa umeme wa TANESCO ni mkombozi kwa wajasiriamali wa saluni za kunyoa

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
PhotoEditor_20190720_210543603.jpg
PhotoEditor_20190719_215111052.jpg

PhotoEditor_20190720_210343655.jpg

PhotoEditor_20190720_210451856.jpg

PhotoEditor_20190720_210924634.jpg

Kutokana na changamoto za umeme
kukatika katika au baadhi ya maeneo kutokuwa na umeme

Nimebuni mashine hii ambayo itamwezesha kinyozi kuendelea na shughuri yake ya kunyoa bila kujali umememe upo au haupo.

Mashine hii inatumia nguvu ya jua ambayo inahifadhi umeme katika bank ya umeme iliyojengewa ndani yake,umeme huu unao hifadhiwa baada ya kuvunwa kutoka katika jua hukuzwa na mfumo uliopo ndani ya mashine hii na kutumika katika kuendesha mashine ya kunyolea.

Mashine hii ina uwezo wa kuzitanua na kuzificha panel zake za kuvuna nguvu ya jua hii inasaidia katika usafirishaji wa mashine na utunzaji.

Kupitia mashine hii kinyozi anaweza kwenda katika maeneo yasio na umeme mfano vijiji vya mbali kwa kubeba mashine hii na kwenda kufanya kazi yake ya kunyoa bila shida.Akimaliza konyoa anabeba mashine yake anarudi.

Pia kwa ambao wapo mjini wanaweza kutumia mashine hii kama mbadala wa jenerator kwasababu ukisha kuwa na mashine kama hii hauhitaji tena kununua mafuta kama jenerator.Wakati wote utaimumia bil ghrama ya ziada wala makelele.Nani rahisi kuihifadhi.

MFUMO WA ZIADA WA KIUCHUMI KATIKA MASHINE HII.

Kwa wajasiliamali wanaweza wakamiliki mashine hii na kuwapa vijana kwenda kunyoa sehemu mbalimbali hasa vijijini.

Mashine hizi zimefungwa mfumo wa mita (kama luku),ambayo inapima kiwango cha matumizi.

Hivyo unaweza ukaamua kukodisha mashine yako kwa watu na ukawa unawachaji kulingana na kiasi cha UNIT wanazo kuwa wametumia kwa mwezi.

Kifaa hiki kinaweza kutumika kama mbadala wa generator au kikatumika kama mashine ambayo kinyozi anatembea nayo hasa maeneo ya vijijini na kunyoa watu hasa maeneo ya minada,shule vilabu n.k

Kwa maelezo zaidi tazama video au wasiliana na mbunifu

0629068815

Transistor
 
Je siku jua halipo ni msimu wa mvua na umeme haupo hiyo solar inachajije..
 
Why kunyolea tu na si bidhaa nyinginezo ?, kama inahifadhi nishati je mtu hawezi kutumia bidhaa nyingine za umeme ? au capacity yake inaendana na hio mashine ya kunyolea uliyonayo ambayo inatumia umeme mdogo..

Samahani kwa maswali kama umeweza kubuni storage yenye capacity kubwa kwanini unaishia kwenye mashine tu ya kunyolea ?

By the way Hongera kwa ku-target vinyozi... na kuwapa solution ya kazi yao
 
Lengo lilikuwa ni kwa kuendesha mashine ya kinyozi lakini pia katika ubunifu huu ulizingatia mfumo uwe na uwezo wa kubebeka na kuhamishika hivyo uzito na ukubwa wa box ilukua ni zingatio kubwa.

Kwasababu aliyeomba kutengenezewa mfumo huu alihitaji pia kuitumia mashine hiyo kwa kusafiri nayo katika vijiji mbalimbali kwa ajili ya kunyoa hivyo tulitengeneza ambayo ni rahisi kubebeka.

Uwezo wa kutengeneza kubwa zaidi upo hata ukihitaji ya kuwasha umeme wa Dar nzima upo utatengenezewa mkuu...hapo tulitarget uendeshaji wa mashine ya kunyolea tu,kama ambavyo unavyoweza kuunda kwa ajili ya tv na taa au kwa ajili ya radio.

Japo haimaanishi ukiweka Tv au radio hapo haiwaki vitafanya kazi lakini si kwa matumizi hayo ishu ya discharging time itakuwa affected....

Asante!
 
500,000/- yakuendesha mashine moja
750,000/- ya kuendesha mashine mbili

Muda wa kufanya kazi mashine bila mashine kuisha chaji ni masaa 10 kwa kila mfumo wastani wa kunyoa watu 14 hadi 17
Gharama hizi hazihusishi mashine ya kunyolea ni mtambo peke yake!
 
500,000/- yakuendesha mashine moja
750,000/- ya kuendesha mashine mbili

Muda wa kufanya kazi mashine bila mashine kuisha chaji ni masaa 10 kwa kila mfumo wastani wa kunyoa watu 14 hadi 17
Unaweza ukawa unaikodisha pia kwasababu inasoma kiasi cha matumizi ya umeme kwa unit ukawa unamcharge mtumiaji kulingana na matumizi yake
 
Unaweza ukawa unaikodisha pia kwasababu inasoma kiasi cha matumizi ya umeme kwa unit ukawa unamcharge mtumiaji kulingana na matumizi yake
Mkuu huo mtambo wa sh 500000,hiyo bei ni pamoja na hizo panel 3? Na pia battery yake inayotunza charge ni Ah ngapi?
 
500,000/- yakuendesha mashine moja
750,000/- ya kuendesha mashine mbili

Muda wa kufanya kazi mashine bila mashine kuisha chaji ni masaa 10 kwa kila mfumo wastani wa kunyoa watu 14 hadi 17
Vipi kama nitaitumia huku nikiacha ikule jua muda utaongezeka au itakuwaje hapo?
 
Vipi kama nitaitumia huku nikiacha ikule jua muda utaongezeka au itakuwaje hapo?
Itakua nzuri zaidi huo muda niliotaja ni wakati mashine ipo off sunlight.

Unaweza kuitumia ikiwa inapigwa na jua muda utaongezeka
 
Back
Top Bottom